Nafasi ya wananchi/wadau kuwasilisha mapendekezo ya jinsi ya kuboresha taasisi za haki jinai

Nafasi ya wananchi/wadau kuwasilisha mapendekezo ya jinsi ya kuboresha taasisi za haki jinai

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Kwa muda sasa kumekuwa na malalamiko kuhusu wananchi kutoridhishwa na utekelezaji wa majukumu ya Taasisi zinazosimamia haki Jinai nchini kuanzia kwenye ukamataji wa mtuhumiwa, upelelezi,utoaji wa dhamana, uendeshaji wa mashtaka, kesi na eneo ambalo aliyehukumiwa anatumikia kifungu chake.

Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ameunda Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuboresha Mfumo na Taasisi za Haki Jinai Nchini. Tume hii ina jukumu la kufanya tathmini ya Mfumo wa Haki Jinai kwa lengo la kufanya maboresho makubwa ili kukidhi matakwa ya Serikali na Jami kwa ujumla.

Katika utekelezaji wa kazi yake, Tume itafanya tathmini ya kina ya mfumo na Taasisi tano ambazo zinahusika moia kwa moja na mfumo wa Haki Jinai Nchini. Taasisi hizo ni;
Kutokana na hali hiyo Katibu wa Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuboresha Taasisi za Haki Jinai anatoa mwaliko kwa Wananchi na wadau wote nchini kuwasilisha mapendekezo ya namna ya kuboresha Taasisi za Haki Jinai.
Kwa Maelezo zaidi soma ambatanisho katika uzi huu.

1.png
2.png

View attachment 2513919
 

Attachments

  • 3.png
    3.png
    277.9 KB · Views: 7
Back
Top Bottom