Makamanda habari zenu,
Kwa muda sana nimekuwa mfatiliaji wa huu uzi, nimegundua kuna watu wanafahamu mambo mengi sana na kuna wengine hawafaham kabisa. Nilichopendea hii thread ni ushirikiano mlionao.
Nachoweza kukazia ni kuwa tafuta connection bila kuchoka huku ukimwomba Mungu wako.
Mimi ninavisa viwili nimekutana navyo katika harakati ya kuingia jeshini. Cha kwanza ilikuwa 2018 nilifanyiwa mpango wa kuingia TPDF kutokea uraiani. Mambo yalinyooka lakini uncle Magu akatibua, yani alikataa mtu kuingia chomboni akiwa anatokea uraiani. Kwa kuwa nilikuwa kwenye hatua za mwisho ilibidi nisitishe hilo zoezi na kuendelea na ratiba nyingine. Pia kipindi hicho, kuna watu 12 walichomolewa jeshini kwakuwa nao waliingia kimchongo.
Kisa cha pili ilikuwa 2019, nilisikia kuna saili za kuingia JKT, kwa kuwa nilikuwa ninacheti cha Mujibu nilisema liwalo na liwe, niende JKT nikajitolee ili iwe rahisi kupata chance ya kuingia TPDF maana magu alikaza sana wakati ule. Kuna ndugu yangu mkoa fulani alikuwa anacheo kikubwa PCCB, nilimshirikisha na akaniahidi kunisaidia niingie JKT kwani kwenye usaili angekuwepo.
Aliniambia niandae vyeti vyangu lakini cha JKT nisikiweke then nisafiri kwenda huko mkoani. Nikiwa njiani alinipigia simu kuwa amepata dharura anaenda Dodoma ameitwa kwa dharura. Alinipa maelekezo ya namna ya kufika kwake, nilifanikiwa kufika na sikukuta mtu kwani funguo nilipewa na jirani aliyekuwa ameachiwa maelekezo. Baadae huyo ndugu yangu aliniambia kuna mtu mwingine anatoka dsm kuja kuungana na mimi hivyo tutakuwa wawili. Basi jamaa alifika usiku sana nikampokea. Asubuhi tulijiandaa na mwana tukaelekea uwanja wa vita, aisee acheni. CONNECTION INASAUTI.
Tulienda direct kwa mshauri wa mgambo, akauliza, nyinyi ndio vijana wa X, tukajibu ndio. Akachukua vyeti vyetu then akasema tukajiunge na wenzetu nje tusubiri maelekezo.
Kufupisha story ni kuwa siku iliyofuata watu wa degree tulikuwa watano, wakiume wanne na wakike mmoja. Tulipigwa KO wakiume wote na siku hiyo wakaingizwa wengine kuziba nafasi zetu.
Hiyo siku sikula kabisa maana sikuamini kama yaliyotokea kule ilikuwa ni ndoto au kweli. Tulimpigia ndugu yetu kumweleza yaliyotokea, alishangaa sana maana alidai maelekezo yote aliyaacha ofisini. Mwisho alidai tusiondoke tumsubiri arudi ili aje apambane na hao aĺiowaachia maelekezo kwani alidai itakuwa wamekula rushwa.
Connection inasaidia sana makamanda