Nafasi za kazi Jeshi la Polisi Tanzania

Samahani wadau nimeitwa usail kesho huku mkoan naombeni ronja tafadhari
 
Wakuu habari zenu mimi nimesoma ivi kwa wale wa form 4 interview yao inakuaje na maswaili yao yanakuaje msaada tunaomba
 
Habarini ....ngoja nitoe nasaha zangu kwa waliokua shortlisted usaili polisi na uhamiaji.


1.Hakikisha kama umeitwa komaa ukapige usaili haijalishi mupo wengi kiasi gani. Na ukifika eneo la tukio jichanganye na wadau upate connection hapo.

2.kwenye wrriten exam mara nyingi maswali wanatoa kulingana na taaluma yako ko usipanic relax mambo ni yaleyale.

3.oral exam jitahid sana uwe na confidence, na unapoitwa jina itikia afandeee,then ingia kwenye room tembea kwa ukakamavu vyeti vyako mkononi,utakuta wamekucholea barabara ifatishe io barabara hadi kwenye box.

4.Hakikisha unabeba vyeti vyako vyote ORIGINAL,LEAVING CERTIFICATE na TRANSCRIPT kama ipo beba.

5.ukifika kwenye box mtizame afande walioko mbele tuu, hawa wa pembeni achana nao kisha kaa mguu sawa salimia JAMBO AFANDE, kisha kaa mguu pande then relax.

6.Nadhan swali la kwanza utaambiwa introduce yourself.,utaeleza kadri ulivoulizwa kama ni kingereza nawewe jibu kingereza, na kama ni kiswahili jibu kiswahili.

7.CONFIDENCE wana asses sana kwahio,hatakama kingereza chako ni cha kuunga wewe unga hivo hivo lakini with confidence.

8.Then ukimaliza zako unashukuru unatoka nje kwa kufuata ile barabara kwahio utageuka nyuma kiukakamavu kwenye lile box then utafata ile barabara hadi unatoka.

9.Jitahid ukitoka ukachukue vyeti vyako vyote nauvikague kabla hujapanda bus kuondoka.

10.usiwe na haraka ya kuondoka,jitahid ujipendekeze kwa mapoti apo uchukue namba sana sana kuanzia nyota1 kwenda juu,ukishindwa basi hata ya askari wa getini wewe chukua namba.

11.hakikisha ukirud home unawasiliana nae mara kwa mara, na ikiwezekana muombe akufanyie mpango jina lipotee hata kwa hela....ANGALIZO: usitoe hela kabla jina halijapita.

12.Na jina likipita kua muaminifu mpe hela kulingana na makubaliano yenu,maana kuna maisha baada ya kutoka depo.

13.Hata kama umeitwa usaili kote komaa upige saili zote ko jitahid uandae hela ya kutosha.

MWISHO:mungu awatangulie kwenye usaili wenu.
 
Usaili kwa watu wa 4m 4 nasikia wanaingia watu wa 5 ama kumi kwenye chumba chausaili
 
Huo Usaili mshapita ...
Nyie wenyewe tu kujiamini kwenu na kujibu maswali Kwa kufuata utaratibu husika.
Japo Kuna vitu vinaangaliwa Kuanzia Utembeaji wakati wa kuingia ukaaji wako kujibu maswali mpk uchukuaji wa Vyeti na uondokaji kwenye Panel...

Zingatieni Sana maelekezo mtakayopewa
Ukijichanganya unaweza kuambiwa rudi tena ukaanze upya na utembee vzr au kutolewa bila hata kusikilizwa ukakosa na nafasi na mibuyu yako ( High Degree of Discipline is of paramount and a mandatory requirement) .Tena Ogopa kuambiwa rudi uanze upya au unatembeaje hvo ...yani tyr washakuchanganya na Akili inaruka unatoka Mchezoni , madogo muache maringa ringa kwenye jambo dogo kwako wao panel ni kubwa na kubwa ni kubwa kuliko, muache maringa ringa vizungu vya kimarekani na viswahili visivoleweka unajitoa mwenyewe. Maisha ni magumu Sana kitaa pia vyomboni mnahitajika ndo Maana mkaitwa.

Wahuni hawatakiwi vyomboni no matter how bright you can be, how educated you are without a discipline you're nothing to us and dangerous to nation at large.

Need to be punctual .
Usaili ni Vita since it's you against them
Haaa haaaa One against ten.
Kazeni inawezekana sana.
 
Madini adimu sana haya.
 
Lonja kali sana.

Barikiwa sana mkuu
 
Wakuu muongozo kwenye kwa usahili wa watu wa tehema ( programming, networking etc) tafadhali
 
Hapo unachukuaje vyeti sasa??[emoji23][emoji23]
 
Kuchukua vyeti unachukuaje...[emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…