Nafasi za kazi Jeshi la Polisi Tanzania

Thank u fam, GOD with us.
 
Mkuu kwanini usiachane na mambo ya mapenzi kwanza usijeumia baadae ukipigwa tukio na uyo manzi
 
mkuu mahusiano ni maisha,ni vipi rijali unaweza jitenga mbali na mahusiano?
Sio kujitenga mazima nachomaanisha unakuwa unatafuta utelezi tu ukiwa high lakini sio kujiwekeza mazima kwa mtoto wa mtu wakati unajua pesa muhim kwenye mahusiano.

Usipokuwa makini utachapiwa uje umtafute mchawi nani ila ni ushauri tu bro..
 
Ndugu zangu, ni wazi kuwa hali ni ngumu sana hasa kupata kazi. Ukiangalia kwa makini utagundua kila mwaka vyuo vinatoa maelfu ya graduates wa level tofauti. Ajira zinazotoka ni chache ukilinganisha na idadi inayotafuta ajira.

Ningependa tushauriane njia mbadala za kutoka kimaisha bila kutegemea hizi kazi. Binafsi naona njia nyingine yakujaribu ni kuomba scholarship nchi zilizoendelea. Ukiwa kule utasoma, utafanya kazi na kutengeneza network ya watu mbali mbali. Target yako iwe network sana maana baada ya kusoma hiyo network itakusaidia sana.

Mwisho kabisa, mimi nimeanza michakato ya kuapply, nitaapply vyuo zaidi ya kumi ili niwe kwenye nafasi nzuri ya kushinda. ASANTENI
 
Upo sahihi kabisa kaka
 
TUSIKATE TAMAA IPO SIKU YA MUNGU, MIMI NIMESHAOMBA SANA KUNA AWAMU NIMEITWA INTERVIEW KUNA AWAMU SIJAITWA KABISA ILA SICHOKA NINA DEGREE ILA NIMEOMBEA FORM 4 AWAMU HII TENA MUNGU KABARIKI JINA LANGU NIPO KWENYE USAILI NA TUNAENDELEA NAAMINI HII NDO ZAMU YANGU YA KUPOKEA BARAKA TUZIDI KUOMBEANA PIA TUSILATE TAMAA AMEN MUNGU NI MWEMA KILA WAKATI
 
Ukipata Full Funded inapendeza zaidi.
 
Upo sahihi kabisa kaka
Hii njia watu wengi wanatoboa, maana utasoma huku unapiga kazi. Kwa week nchi nyingi zinatoa masaa 20 ya kufanya kazi. Hivyo kwa mwezi ni masaa 80. Ukizidisha kwa dola 8 (kima cha chini kabisa japo unaweza pata zaidi) kama malipo ya kazi kwa saa, utakuwa na 640USD. wakati huo umepata full funded scholarship. Utagharmiwa kila kitu mpaka nauli.

Wakuu nimetoa hesabu ya haraka tu. Unaweza pata hela nzuri zaidi ya hiyo. Lakini pia baada ya kumaliza masomo utapewa muda wa kukaa katika nchi husika kwa kipindi cha miezi 18 (siyo kila nchi) kutafuta kazi. Ukifanikiwa kupata, amini kwamba waliokutangulia kupata kazi bongo wengi utawazidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…