Nafasi za kazi Jeshi la Polisi Tanzania

Nafasi za kazi Jeshi la Polisi Tanzania

Kuna Jamaa zangu hapa Wawili wakike na Wakiume hawajawahi kwenda JKT kwa Mujibu wala kwa kujitolea,sasa wamepata Mkubwa jeshini wanadai nimiongoni mwa Ma Afisa wakuu Jeshini, Wametoa kama Milion kadhaa wapewe hizi nafasi. je..?? Kuna huu uhuni TPDF..???

Kama huu mchezo upo basi watoto wa Maskini mtasota sana huko makambini wengine wanachoropokea majumbani moja kwa moja RTS.
 
Mkuu nafikiri hawa wa kujitolea huwa wanajiona wana ka uspecial fulani hivi kuliko wa mujibu wa sheria, wakati mara nyingi wa kujitolea huishia hivi vyeo vya sergeant maana wengi hawajasoma wameishia form four, halafu hao wa mujibu wakipata nafasi wengi huenda kuwa officers
Ila wakujitolea ndo makamanda wapiganaji wanao itajika katika vita.Wale wasomi huwa sio market Jeshini na ndo maana kuajiriwa kwake ni 10 kwa mmoja.
 
inawezekana ila kama una sifa zote peleka tuu kwa mkono man online ni zitakuwa nyingi sana za wazee wa kujaribu hivohivo wanaweza kupuuzia nyingine
Kupeleka kwa mkono au kutuma kwa njia ya posta.....maana sio wote wapo makao mkuu
 
Unaona uko sahihi au unakosea?
Jitafakari then jibu usikurupuke
Mwisho wewe ni Mjinga sana.
Ameshavuka viwango vya ujinga, huyo ni mpumbavu grade one.

Tulianza kuwapokea wa kujitolea Op Uchumi wa kati mwaka 2020 mwezi wa 12 na walikuwa ni elimu zote la saba hadi elimu ya juu!!

Kumbuka kipindi hicho Op melerani ndio walikuwa wanajiandaa kurudi makwao hivo muitikio wa kuripoti ulikuwa mdogo sana.

Kambi niliyokuwepo ilitakiwa ipokee vijana wa kujitolea 500+, hadi deadline inafika walikuwa wameingia 258 tuu.

Kilichotokea mwanzoni mwa 2021 walisitisha hiyo Op na wote walirudi makwao wakaambiwa kuwa wataitwa tena!

Kikochotokea sasa baada ya kurudishwa huku wanajeshi wakaanza kutafuta ndugu zao ili kuwaongezea waje kujitolea na sifa kuu ilikuwa ni awe wa kidato cha nne.

Baadae ndio ikatangazwa warudi kidato cha nne pekee yao makambini walikopangiwa kabla ya kurudishwa, na hapo jina likabadilishwa wakaitwa op Samia ambao wapo makambini hadi leo kama Seniors wa op Mabeyo.

Wakati huohuo huyu 92 wa mchongo anaowaita waasi walikuwa wakiendelea na ujenzi nao walikuwa ni Op mbili tuu, nazo ni Marelani na Op makao. Hadi pale sakata la uasi lilipo ibuka na baadhi yao kusitishiwa mkataba.

Baadae walisamehewa na kurudishwa mafinga JKT wakisubiri kupelekwa Msata.

Kweli walipelekwa Msata na kule wamechujwa sanaa na wale inaosemekana ni unfit walirudishwa makwao na baadhi yao mmefanya nao saili za PT na MT, naveengine wameenda UT.

Kiujumla hili tangazo linawahusu Op makao, Op malerani na magufuli na kuendelea(kama wapo) wenye vigezo.

Elimu ya juu kuungia kujitolea ni miaka 25 na watu wamekaa miaka 3 na wao wanajua hili na wametaka 27.

Kama upo na miaka 28 na kuendelea nanafsi inakwambia tuma, wewe tuma tuu.. huwezi jua.
 
Mwaka huu kuna mabogi mawili Msata na Oljoro
wa vikosini wanaenda msata pamoja na wazee wa kupiganisha aka baba kantuma
af sasa chama la wana lililolata tamaa wanajua kwa kukutana,rejea op muungano mambo ni yaleyale ya Gn Mwamunyange
Huu ndio ukweli, usio na shaka.
 
Za ndaani kabisa kutoka makao makuu,
Hizi nafasi unaambiwa zimetolewa kisiasa
Unaambiwa baada ya jeshi kufanya uchunguz na kujua panya road ni vijana wao waliorudishwa mtaani na kukosa ajira nakuanza kusumbua mtaani kwakua wana ujuzi wa kutumia silaha,
Basi jeshi likaamua kuwapa nafasi hawa watu ila ktk hizo hizo nafasi amini kuna upachikaji wa watu usiache kuomba na pia kumuomba mungu bila kusahau mbanga😀
 
Za ndaani kabisa kutoka makao makuu,
Hizi nafasi unaambiwa zimetolewa kisiasa
Unaambiwa baada ya jeshi kufanya uchunguz na kujua panya road ni vijana wao waliorudishwa mtaani na kukosa ajira nakuanza kusumbua mtaani kwakua wana ujuzi wa kutumia silaha,
Basi jeshi likaamua kuwapa nafasi hawa watu ila ktk hizo hizo nafasi amini kuna upachikaji wa watu usiache kuomba na pia kumuomba mungu bila kusahau mbanga😀
Daaah ni hatareee sasa
 
Wakuu haya maombi yanatumwaje kwa waliokuwa mtaani....ni kwa njia ya posta au kwa njia ya online....msaada wakuu
 
Mwaka huu kuna mabogi mawili Msata na Oljoro
wa vikosini wanaenda msata pamoja na wazee wa kupiganisha aka baba kantuma
af sasa chama la wana lililolata tamaa wanajua kwa kukutana,rejea op muungano mambo ni yaleyale ya Gn Mwamunyange
Ilikuwaje iyo Op Muungano??
 
Back
Top Bottom