Vijana naona kuna baadhi wana mtelo wa usaili wakati wengi wenu mmepita JKT ishu ya mitelo ilishawatoka baada ya zile six week za mkesha labda kwa mliopita JKT Mujibu wa sheria wengi huwa mnatoka mananga ile miezi mitatu yenu ya mafunzo.
Usaili ni mambo makuu mawili tu.
1.usaili wa vyeti vyote kama ni halali
2.utimamu wa mwili-hapa ni huna michoro mwilini,huna ulemavu wowote ule,huna mishono ya operesheni kubwa itayozuia kufanya mafunzo,hujihusishi na vitendo vya ushoga(malinda yapo?) nk.
3.hapa sasa itategemeana na wasaili wa eneo husika wanaweza kuwapa ka mtihani ka maswali kidogo kupima uwezo wenu wa kuchanganua mambo na hasa ishu za current affairs labda na mengineyo na hii inaweza isitokee kabisa au ukasikia mkoa x wamefanyiwa lakini wewe wa mkoa y usipitie hayo.