Kuna jamaa mmoja humu huwa anasisitiza kumuomba sana Mungu na kumtegemea yeye especially kama hauna mtu wa kukushika mkono.
Nakumbuka nilishawahi kuwa katika hali kama yako kuhitaji mtu wa kunishika mkono ili niweze kuingia sehemu. Nilisali sana, kila siku nilikuw najitahidi ninavyoenda jogging najog porini na kumuomba Mungu ombi moja kubwa kuwa "aniletee/ ainue watu wa kunishika "mkono.
Kwa imani yangu na kwa maombi yangu, Mungu alitukutanisha na mtu katika hali isiyokuwa na kawaida. Mzee yule alikuw very simple na maisha ya kawaida ila alikuw na connections za ajabu sana. Yani phone book yake akikuonesha unashangaa na kujiuliza huyu mzee kapataje hizo connections na yupo anaendesha zake uber tu.
So since then nimekuwa nikiamini katika Maombi na kumuamin Mungu. Akikupangia sehemu basi itawezekana tu. Kikubwa ni kumuamin yeye. Pia ishi na watu vizur, kuwa mdadisi. Unaweza kuta sehemu unayoishi kuna watu wapo na connections kali tu ila hujui.
Maandiko yanasema tusitegemee akili zetu na tumtumaini yeye na atanyoosha Mapito yetu.
Jumapili njema wapambanaji. Nawatakia heri.