Nafikiri kijana anayejenga katika usawa huu anatakiwa apewe heshima yake

Vipi kama hizo hela alizo jengea ni za wizi, rushwa au magumashi ?! πŸ˜‚πŸ˜‰
 
Kama bado hujaanza ujenzi nakushauri usijenge. Yani kuezeka tu nyumba nimetumia 12m. Ujenzi siyo mchezo jamani
Kwa hiyo kama wewe umetumia 12M kuezeka ndo ushauri watu wasijenge? Hii nayo ni aina nyingine ya ubinafsi. Hupaswi kuwa humu jukwaani maana huna faida yoyote kwa watu wanaojichanga kwa ajili ya kuanza ujenzi wao. Yaani wewe ni memba wa ovyo kabisa
 
Hio kauli ya kusema JF wote madon sio nzuri, umewahi kusoma comment ya Kila mmoja humu? Hujaona Uzi wa jobless kule, watu tunatafuta vibarua hata vya sh 5000 kwa siku na hatupati.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Pole
Tatizo hao hao wa kwenye uzi wa majobless wanawaponza, wakija huku kwenye nyuzi zingine wanasema wao ni wafanyabiashara wakubwa.!!
 
Kwa hiyo kama wewe umetumia 12M kuezeka ndo ushauri watu wasijenge? Hii nayo ni aina nyingine ya ubinafsi. Hupaswi kuwa humu jukwaani maana huna faida yoyote kwa watu wanaojichanga kwa ajili ya kuanza ujenzi wao. Yaani wewe ni memba wa ovyo kabisa
Wewe mwenye faida yoyote humu jukwaani endelea kuwatia moyo kama huo moyo wako ndiyo utakaojenga nyumba zao
 
Mkuu ni kweli unacho kisema vifaavya ujenzi vimepanda bei sana Mfuko wa mmoja wa Cement ni shilingi 17,000 Boksi moja la Tairs ni shilingi 30,000 bado ubebaji. Mchanga gari dogo la bajaji ni shilingi 35,000 Mimi nimetengeneza Milango 2 kwa gharama ya shilingi Milioni moja pamoja na uwekaji na gharama za fundi. Angalia video yangu hiyo hapo chini.


Your browser is not able to display this video.

Mlango mmoja huo umesha kuwa teyari umekamilika .


Your browser is not able to display this video.

Milango ya banda langu hilo limekamilika Limenigharimu kutengeneza hilo banda lenye vyumba 2 pamoja na choo na kuweka umeme na maji karibu Shilingi Milioini 10. Bado kujenga kiwanja cha mbele.Kweli kujenga wakati huu unatakiwa uwe na kiasi cha shilingi Milioini 60 ndio utaweza kujenga nyumba pasipo na hiyo pesa sio rahisi kujenga nyumba.

mlango mmoja tu pamoja na gharama za kuweka umenigharibu shilingi laki 5.




jumla ni milango 2 kwa gharama ya shilingi Milioni 1 haya vijana munaotaka kujenga nyumba jipangeni kipesa kila kitu kimekuwa ni ghali sana nyumba yangu hiyo ipo kigamboni jijini Dar anayetaka kupangisha anione kwa wakati wake ingawa bado kupaka rangi nje na chumba kimoja kumaliza kukweka Tairs na kuweka hapo nje kibaraza. Lakini akitokea mtu anataka kupanga nipo teyari kumpangisha .
 
Hongera kwa kupambana ,ila pale kwenye bati hapavuji kweli ? hebu weka vizuri usije kupata loss ,hapo ukipiga finishing mbona fresh tu
 
Allahu akbar
Kumbe safar yangu ndefu.. mana Nina ramani hapa ya msingi flani hiv mana ndo natafuta hela lakini hoi. Kweli sio poa

Lamomy
 
Bei ya tofali kigambon kias gan
 
Hata hiyo ni hatua kubwa umepiga shem jipongeze, kuna wengine hata hawajui wanakula nini achilia kujua bei ya cement
Hali kwa vijana hasa graduet si nzuri. Mambo yanaenda kas pa kushika hakuna. Na mbaya zaid private sector nazo mishahra yake kwa kipindi hiki bora serikalin tu mana na mkopo unapata.

Sometimes we loose, wengi tumezungukwa na watu ambao sio sahihi. Na umaskinin familia zetu zillivyofungaman na mambo mengi ya ajabu ajabu, nimeona ch kwanza kabisa ni target ya miaka mitatu ijayo kuishi kwangu. Hapa mpaka mwaka uishe nadhan nitakuw na akiba kama ya 5m ila Kaz ngum sio poa
 
Pole jamani shem wangu, Mungu akuonekanie na akufungulie milango ya baraka ufanikishe malengo yako πŸ™
 
Safi sana kanyaga twende kiongozi.piga KAZI ni kipimo cha utu
 
Hiyo mil5 ni choo tu, ukitaka chumba kimoja ni mil 50, ukitaka chumba kimoja na choo andaa at least mil 70
Acheni kupotoshana vijana ujenzi sio gharama kiasi hicho. Milioni 50 unajenga nyumba ya vyumba vitatu master moja na choo cha public sebule, jiko na dining ukuwa wa sqm 120 na inakamilika katika standard quality.

Nimejenga nyumba ya vyumba viwili sebule dining na jiko na nimeipangisha kwa 250,000 nyumba imenigharimu milioni 25 na ina kila kitu mpk mafeni ya Panasonic ndani tiles nzuri gypsum na madirisha ya aluminium
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…