Street Hustler
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 2,175
- 4,299
Nipo Dumila juu njia ya kwenda Dodoma kuna kijiji kinaitwa Nyacha kina ardhi nzuri sana kwa ajili ya kilimo na ufugaji, me mwenyewe nimedaka heka kadhaa na naendelea kuongeza maana bei ni chee.Mkuu dumila maeneo gani hapo mi nimefika hadi msowero
Usiweke makadirio ya juu hivyo kwenye maziwa hayoSikupingi mkuu Ila kwa shule na huo mtaji mbn ni mdogo alafu pia nimechaguo huo mradi kutokana na interest zangu nitamudu
Lakini pia hata kimapato naona Kama maziwa italipa zaidi
Lita 1500 kwa siku na lita moja wastani niuze sh 1000 mara lita 1500 naona italipa zaidi japo bado sijajua changamoto zingine ndomana nikaja humu
Ni mahindi na alizet tu wanalima huko sio? Heka wanauzaje?Nipo Dumila juu njia ya kwenda Dodoma kuna kijiji kinaitwa Nyacha kina ardhi nzuri sana kwa ajili ya kilimo na ufugaji, me mwenyewe nimedaka heka kadhaa na naendelea kuongeza maana bei ni chee.
Shukrani mkuu kwa ushauri wako hao ngombe 50 nilitaka kununua Kama ndama niwakukuze MimiNi wazo zuri sana la kibiashara, ila kulifanikisha ni ngumu sana, huu ni mradi unaohusisha uhai wa wanyama kwahiyo changamoto za maradhi na vifo ni setback kubwa ambayo utaenda kukutana nayo
changamoto kubwa ya Kwanza ni kuuziwa wanyama ambao hawana sifa unazozitaka,asilimia kubwa hakuna mfugaji ambae anauza mnyama wake walio Bora, mara nyingi wanauza wanyama wenye changamoto za maradhi/ uzalishaji ukapambane na wewe
Na Sijui kama hiyo 80M ndio budget ya kununua tu Ng'ombe au ni pamoja na ujenzi wa mabanda, maana kama lengo ni uzalishaji wa maziwa Lita 1500 Kwa siku ujue utatakiwa kuwa na miundombinu mizuri na itakugharimu pesa nyingi sana
Na kingine ni kwamba ni ngumu au haiwezekani kupata Ng'ombe wa kutoa Lita 30/day, Tanzania Ng'ombe ambao wanaweza kutoa Lita 30/day itakuwa wanahesabika na hao watakuwa wanapatikana kwenye Ranch za watu binafsi
Kwa bongo Ng'ombe akitoa Lita 15-20 huyo ndio Mwamba, kwahiyo kwenye kundi Lako la Ng'ombe 50 unaweza usipate ata mmoja anaetoa Lita 30, kwahiyo ni bora ukachange hesabu zako ziendane na uhalisia wa wanyama tulionao, weka maximum Lita 20 na of course ni ngumu mtu awe na Ng'ombe anatoa Lita 30 alafu amuuze
Na mwisho kabisa heka 5 hazitoshi kuhudumia Ng'ombe 50 wa maziwa, ni eneo dogo sana, Kwa Hilo eneo Lako yani umezidisha sana ungekuwa unapiga hesabu ya Ng'ombe 20
Duuuuu viwanda wanyonyaji wakati wao wanatuuzia kapakti kadogo kwa mfano tanga fresh ule mtindi 500g ni sh 1500 na hiyo ni nusu lita tuFacts check
Maziwa kwa viwanda bei ni 500-800 sio 1000
Pia ng’ombe wa kukupa maziwa lita 30 consistently ni ngumu kupatikana pigia lita 10-20 per day
Pamoja Mkuu, All the bestShukrani mkuu kwa ushauri wako hao ngombe 50 nilitaka kununua Kama ndama niwakukuze Mimi
Pia kuhusu sehemu ya kununua nilitaka kununua kwenye vyuo vya kilimo na ufugaji Kama sua na vinginevyo au kwenye lunch za serikali maana watu binafsi sio waaminifu
Swala la eneo hizo ekari tano Ni ujenzi tu wa mabanda pamoja na nyumba za za wafanyakazi na maghara ya kuhifadhia chakula
Kuhusu malisho ninaplan ya kununua shamba lingine lenye ukubwa wa eka 10 kunamajani niliyoyafatilia sehemu yanahitwa super Napier grass hybrid hayo majani kwa ekar moja yanakupatia tone 200 kwa mwaka hivyo basi kwa hizo eka 10 nitakua na uhakika wa kupata tone 2000 kwa mwaka
Na kwa mahesabu niliyopewa Ni kwamba ngombe mmoja kwa siku anakula kilo 15 _20 za majani nje ya supplements ambazo nazo anakula kilo 4 Yan 2 asubuhi 2 jioni
Hvy basi kwa hao ngombe 50 kwa siku watatumia tone 1 kila siku kwahio kwa upande wa chakula Sina tatizo juu ya ilo
Dumila ni mahali pa zuri sana kwa shughuli hii. Biashara hii ni zuri sana na itakulipa, wala hutahitaji kuanza na hela yote hiyo, waweza anza kidogo huku ukisoma mzaingira na kuziea mazingira. Nakushauri uanze na kutafuta soko la maziwa ya kiwango hicho cha uzalishaji maana hapo huwa ndo changamoto katika biashara ya maziwa. Pale Kimamba kuna vituo vya kupokelea maziwa yapata kama viine, na huwa wanapokea maziwa kwa wingi na wana cooling mashine kuhifadhia maziwa kabla hayajasafirishwa, wanachukua maziwa yenye ubora kwa wastani shs 800, mengi ya haya maziwa hutoka kwa wafugaji wa kimasai walioko maoneo hayo. Unaweza anzia kwa vituo kama hivyo kupata data za soko na uwezo wao.Nipo Dumila juu njia ya kwenda Dodoma kuna kijiji kinaitwa Nyacha kina ardhi nzuri sana kwa ajili ya kilimo na ufugaji, me mwenyewe nimedaka heka kadhaa na naendelea kuongeza maana bei ni chee.
Nipo Dumila juu njia ya kwenda Dodoma kuna kijiji kinaitwa Nyacha kina ardhi nzuri sana kwa ajili ya kilimo na ufugaji, me mwenyewe nimedaka heka kadhaa na naendelea kuongeza maana bei ni chee.
Kagoma kujibuBei kwa heka ni kiasi gani?