Ni wazo zuri sana la kibiashara, ila kulifanikisha ni ngumu sana, huu ni mradi unaohusisha uhai wa wanyama kwahiyo changamoto za maradhi na vifo ni setback kubwa ambayo utaenda kukutana nayo
changamoto kubwa ya Kwanza ni kuuziwa wanyama ambao hawana sifa unazozitaka,asilimia kubwa hakuna mfugaji ambae anauza mnyama wake walio Bora, mara nyingi wanauza wanyama wenye changamoto za maradhi/ uzalishaji ukapambane na wewe
Na Sijui kama hiyo 80M ndio budget ya kununua tu Ng'ombe au ni pamoja na ujenzi wa mabanda, maana kama lengo ni uzalishaji wa maziwa Lita 1500 Kwa siku ujue utatakiwa kuwa na miundombinu mizuri na itakugharimu pesa nyingi sana
Na kingine ni kwamba ni ngumu au haiwezekani kupata Ng'ombe wa kutoa Lita 30/day, Tanzania Ng'ombe ambao wanaweza kutoa Lita 30/day itakuwa wanahesabika na hao watakuwa wanapatikana kwenye Ranch za watu binafsi
Kwa bongo Ng'ombe akitoa Lita 15-20 huyo ndio Mwamba, kwahiyo kwenye kundi Lako la Ng'ombe 50 unaweza usipate ata mmoja anaetoa Lita 30, kwahiyo ni bora ukachange hesabu zako ziendane na uhalisia wa wanyama tulionao, weka maximum Lita 20 na of course ni ngumu mtu awe na Ng'ombe anatoa Lita 30 alafu amuuze
Na mwisho kabisa heka 5 hazitoshi kuhudumia Ng'ombe 50 wa maziwa, ni eneo dogo sana, Kwa Hilo eneo Lako yani umezidisha sana ungekuwa unapiga hesabu ya Ng'ombe 20