Nafikiria kuanzisha biashara ya kuwauzia maziwa viwanda vinasindika maziwa kama vile Tanga fresh na vinginevyo

Nafikiria kuanzisha biashara ya kuwauzia maziwa viwanda vinasindika maziwa kama vile Tanga fresh na vinginevyo

Kumbuka maziwa ya Kenya (au ya Uhuru) brookside yanauzwa kihalali hapa Tanzania nasio haramu Kama mwaka mmoja nyuma ilivyokuwa hvyo tegemea hzo kampun kufa baada ya miaka mitatu.

Shamba la ufugaji Ng'ombe 50 nunua kuanzia heka 100 nakuendelea mana Hilo wazo lako n either uwe kiwanda kidogo au mtugaji wa kisasa mdogo
 
Sikupingi mkuu Ila kwa shule na huo mtaji mbn ni mdogo alafu pia nimechaguo huo mradi kutokana na interest zangu nitamudu
Lakini pia hata kimapato naona Kama maziwa italipa zaidi
Lita 1500 kwa siku na lita moja wastani niuze sh 1000 mara lita 1500 naona italipa zaidi japo bado sijajua changamoto zingine ndomana nikaja humu
Usiweke makadirio ya juu hivyo kwenye maziwa hayo

Ungeweka hata kati ya 800 na 1000
 
Nipo Dumila juu njia ya kwenda Dodoma kuna kijiji kinaitwa Nyacha kina ardhi nzuri sana kwa ajili ya kilimo na ufugaji, me mwenyewe nimedaka heka kadhaa na naendelea kuongeza maana bei ni chee.
Ni mahindi na alizet tu wanalima huko sio? Heka wanauzaje?
 
Ni wazo zuri sana la kibiashara, ila kulifanikisha ni ngumu sana, huu ni mradi unaohusisha uhai wa wanyama kwahiyo changamoto za maradhi na vifo ni setback kubwa ambayo utaenda kukutana nayo

changamoto kubwa ya Kwanza ni kuuziwa wanyama ambao hawana sifa unazozitaka,asilimia kubwa hakuna mfugaji ambae anauza mnyama wake walio Bora, mara nyingi wanauza wanyama wenye changamoto za maradhi/ uzalishaji ukapambane na wewe

Na Sijui kama hiyo 80M ndio budget ya kununua tu Ng'ombe au ni pamoja na ujenzi wa mabanda, maana kama lengo ni uzalishaji wa maziwa Lita 1500 Kwa siku ujue utatakiwa kuwa na miundombinu mizuri na itakugharimu pesa nyingi sana

Na kingine ni kwamba ni ngumu au haiwezekani kupata Ng'ombe wa kutoa Lita 30/day, Tanzania Ng'ombe ambao wanaweza kutoa Lita 30/day itakuwa wanahesabika na hao watakuwa wanapatikana kwenye Ranch za watu binafsi

Kwa bongo Ng'ombe akitoa Lita 15-20 huyo ndio Mwamba, kwahiyo kwenye kundi Lako la Ng'ombe 50 unaweza usipate ata mmoja anaetoa Lita 30, kwahiyo ni bora ukachange hesabu zako ziendane na uhalisia wa wanyama tulionao, weka maximum Lita 20 na of course ni ngumu mtu awe na Ng'ombe anatoa Lita 30 alafu amuuze

Na mwisho kabisa heka 5 hazitoshi kuhudumia Ng'ombe 50 wa maziwa, ni eneo dogo sana, Kwa Hilo eneo Lako yani umezidisha sana ungekuwa unapiga hesabu ya Ng'ombe 20
Shukrani mkuu kwa ushauri wako hao ngombe 50 nilitaka kununua Kama ndama niwakukuze Mimi

Pia kuhusu sehemu ya kununua nilitaka kununua kwenye vyuo vya kilimo na ufugaji Kama sua na vinginevyo au kwenye lunch za serikali maana watu binafsi sio waaminifu

Swala la eneo hizo ekari tano Ni ujenzi tu wa mabanda pamoja na nyumba za za wafanyakazi na maghara ya kuhifadhia chakula

Kuhusu malisho ninaplan ya kununua shamba lingine lenye ukubwa wa eka 10 kunamajani niliyoyafatilia sehemu yanahitwa super Napier grass hybrid hayo majani kwa ekar moja yanakupatia tone 200 kwa mwaka hivyo basi kwa hizo eka 10 nitakua na uhakika wa kupata tone 2000 kwa mwaka

Na kwa mahesabu niliyopewa Ni kwamba ngombe mmoja kwa siku anakula kilo 15 _20 za majani nje ya supplements ambazo nazo anakula kilo 4 Yan 2 asubuhi 2 jioni

Hvy basi kwa hao ngombe 50 kwa siku watatumia tone 1 kila siku kwahio kwa upande wa chakula Sina tatizo juu ya ilo
 
Facts check
Maziwa kwa viwanda bei ni 500-800 sio 1000
Pia ng’ombe wa kukupa maziwa lita 30 consistently ni ngumu kupatikana pigia lita 10-20 per day
Duuuuu viwanda wanyonyaji wakati wao wanatuuzia kapakti kadogo kwa mfano tanga fresh ule mtindi 500g ni sh 1500 na hiyo ni nusu lita tu
 
Shukrani mkuu kwa ushauri wako hao ngombe 50 nilitaka kununua Kama ndama niwakukuze Mimi

Pia kuhusu sehemu ya kununua nilitaka kununua kwenye vyuo vya kilimo na ufugaji Kama sua na vinginevyo au kwenye lunch za serikali maana watu binafsi sio waaminifu

Swala la eneo hizo ekari tano Ni ujenzi tu wa mabanda pamoja na nyumba za za wafanyakazi na maghara ya kuhifadhia chakula

Kuhusu malisho ninaplan ya kununua shamba lingine lenye ukubwa wa eka 10 kunamajani niliyoyafatilia sehemu yanahitwa super Napier grass hybrid hayo majani kwa ekar moja yanakupatia tone 200 kwa mwaka hivyo basi kwa hizo eka 10 nitakua na uhakika wa kupata tone 2000 kwa mwaka

Na kwa mahesabu niliyopewa Ni kwamba ngombe mmoja kwa siku anakula kilo 15 _20 za majani nje ya supplements ambazo nazo anakula kilo 4 Yan 2 asubuhi 2 jioni

Hvy basi kwa hao ngombe 50 kwa siku watatumia tone 1 kila siku kwahio kwa upande wa chakula Sina tatizo juu ya ilo
Pamoja Mkuu, All the best
 
Nipo Dumila juu njia ya kwenda Dodoma kuna kijiji kinaitwa Nyacha kina ardhi nzuri sana kwa ajili ya kilimo na ufugaji, me mwenyewe nimedaka heka kadhaa na naendelea kuongeza maana bei ni chee.
Dumila ni mahali pa zuri sana kwa shughuli hii. Biashara hii ni zuri sana na itakulipa, wala hutahitaji kuanza na hela yote hiyo, waweza anza kidogo huku ukisoma mzaingira na kuziea mazingira. Nakushauri uanze na kutafuta soko la maziwa ya kiwango hicho cha uzalishaji maana hapo huwa ndo changamoto katika biashara ya maziwa. Pale Kimamba kuna vituo vya kupokelea maziwa yapata kama viine, na huwa wanapokea maziwa kwa wingi na wana cooling mashine kuhifadhia maziwa kabla hayajasafirishwa, wanachukua maziwa yenye ubora kwa wastani shs 800, mengi ya haya maziwa hutoka kwa wafugaji wa kimasai walioko maoneo hayo. Unaweza anzia kwa vituo kama hivyo kupata data za soko na uwezo wao.
Hii biashara mimi nimeifanya maenoe ya pwani pale kongowe, ukweli kama soko likiwa sawa unapata hela nzuri kuliko anyefuga kuku wa mayai au wa nyama, ila mara kadhaa tulilazimika kumwaga maziwa maana collection point walikuwa si wakutegemewa sana.
Faida ya bishara hii sii katika kuuza maziwa tu, bali kama utaendesha shamba kitaalam utauza mitamba yenye ubora kwa bei nzuri sana. mtamba mmoja mwenye mimba ya miezi 5 had 6 kwa sasa yaweza kukugharimu kati ya TZS 2m - 2.5m. ni uwekezaji mzuri sana na kama wewe mwenyewe pia utalazimika kukaa au kuhamishia mazi yako Dumila.
Kila la heri ndugu.
 
Bei kwa heka ni kiasi gani?
Nipo Dumila juu njia ya kwenda Dodoma kuna kijiji kinaitwa Nyacha kina ardhi nzuri sana kwa ajili ya kilimo na ufugaji, me mwenyewe nimedaka heka kadhaa na naendelea kuongeza maana bei ni chee.
 
Ulifanikiwa?? MPINGA UKAWA
Akina Afrifarm nadhani wametoka South Africa wanaleta ng'ombe Bora wa maziwa mkishaelewana. Wana na vifaa vya ufugaji.
Pia why Dumila?
 
Mkuu ningekuwa na eneo ningeifanya hii biashara na pia kuwa na kiwanda cha kusindika maziwa kabisa kwa sababu competitors kama Tanga fresh na ASAS hawatengenezi maziwa ya unga, ghee au siagi
 
Back
Top Bottom