Nafikiria kufanya maamuzi haya magumu japo naumia sana

Nafikiria kufanya maamuzi haya magumu japo naumia sana

Sasa we umenuna bila mpangilio kama furushi la nguo chafu[emoji28] nani ana muda wa kuanza kubembelezana muda wa kulala ukifika. Tanua nikurenge
Kurenga kama wale wa kanda maalumu [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wakuu kiufupi nina mke na mtoto mmoja wa miezi 9 sasa. Tumekuwa tunaishi kwa kutegemeana kama mke na mme kwenye mambo mbalimbali. Nilibahatika vibaya kupoteza kazi baada ya kuwa mkataba wangu umeisha mwishoni kwa mwaka jana.

Tangu hapo mke wangu anaonyesha dharau waziwazi. Kiufupi ni dharau ambazo kiukweli chanzo chake ni kupungukiwa kipato japo nafanya bidii za biashara used naingiza pesa kiasi japo sio kama nilivokuwa napata salary. Mke wangu anabiashara yake nimemkuta nayo japo niliingiza pesa kama kutanua biashara iwe kubwa.

Cha kushangaza kafikia hatua hadi baadhi ya pesa nilizompa siku sio nyingi anakatalia ikabidi nimfate ofisini kwake ni chukue alivogoma nika force tukaharibu simu yake akaenda police kunichukulia RB kwamba nimemfanyia fujo japo hawakuja kunikamata na hii ni mara ya tatu kunishtaki kwa mambo ya kipuuzi mara zile mbili alinipeleka kwa mjumbe.

Sina amani na hataki tuachane mfano juzi nikamwambia ngoja nimwachie nyumba au nimtafutie room akae na mwanae mimi nikatafute pesa siku nikipata nitarudi amegoma na hapa tunapoishi kodi imeisha.

Sasa ninafikiria kumtoroka asijue nilikokwenda, najuwa hana hela ya kupanga chumba kwa sasa na hapa tulipo sasa nimesha mwambia mwenye nyumba naondoka. Yaani wakuu kuna madhira kibao hadi nafikiria na kuwaza mambo magumu sana.

Naandika lakini nahisi kama hamtanielewa maana ni mambo magumu sana. Sijawahi kumcheat mke wangu na sina demu mwingine lakini naishi nae ndani kama kaka na dada hata haitaji nimguse.

Ana kiburi kama chote jeuri imezidi hana hekima kabisa sometime hana aibu hata mbele za watu anaweza jibu hovyo tu.

NAMPENDA MWANANGU HIKO NDO KINANIUMA KUMUACHA LAKINI NAHISI NI KIFUNGO KIBAYA SANA KUENDELEA KUISHI NA HUYU MWANAMKE. NADHANI NIKIWA MBALI NAE ANAWEZA ONA UMUHIMU WANGU.

Nimechoka wakuu naomba mawazo uenu pia ikiwa utaguswakunishauri. Hatujafunga ndoa bado ni wachumba najulikana kwao na anajulikana kwetu.

Ahsanteni.
Nimeishia pale tu ulipo andika kua mke wako kakupeleka POLICE, sijaendelea kusoma tena Kwa sababu huyo siyo mke... Hilo ni gume gume tu la mjini na halifai, achana nalo, mke huvumilia yote na mume huvumilia yote.
 
Mke kuchiti ni hatua mbaya sana yani inaboa kinyama maana hata ule upendo haupo tena unabakia na sonona tu.
Hivi unazani wanawake huwa hawaumii ? Hapana huwa wanavumilia maumivu ndiyo siku yakikusanyika pamoja inakuwa Fukushima lakutosha
 
Back
Top Bottom