Nafungua Masikio Kumsikiliza Emmanuel Nchimbi, na Wengine Wooote wa Aina Hiyo Waliopo Huko

Wala hawatofautiani sana, labda elimu na utamaduni tu.

Umewahi kumuona Nchimbi akiwa na msimamo wa jambo lolote kubwa la maana kabla hajawa makamu wa Rais?
Alishawahi pinga hadharani kamati kuu kumuengua lowassa
 
"Ndugu" Emanuel Nchimbi kwa sasa hivi namchukulia kuwa ni mfungwa kama tulivyo wengine wote, waTanzania tusiofurahishwa na mwenendo na mwelekeo wa taifa letu ulivyo kwa sasa.

Sina shaka yoyote, kwamba wapo wengine wengi huko huko aliko Nchoimbi ambao hawajapata ujasiri wa kusema, kama anavyofanya yeye sasa hivi.

Nataka Nchimbi uwe mfano kwa hao waliokaa kimya kwa sababu mbalimbali na wao waseme au waonyeshe mfano kwa njia yoyote waonyeshe kuwa hali iliyopo nchini mwetu sasa hivi haifai kuliko kubaki kimya.

Nchimbi anayezungumza sasa hivi, ni tofauti "kidogo" na Nchimbi aliyekaa kimya na kuwa mshiriki na kutumiwa kuwakandamiza waTanzania.

Pamoja na kwamba wengi tutabaki na wasiwasi juu ya haya anayoyazungumzia, kuwa ni mbinu zilezile zinazotumiwa na hili kundi ovu, yakilenga kuendeleza utawala uleule uliosababisha haya ya leo, inatubidi tumpe fursa ya kumsikiliza na kumwelewa kabla ya kuhitimisha lengo hilo la kuendeleza hila.

Ni muhimu tuelewe tumefika hapa tulipo kwa njia gani, ili tuweze kubadili njia hiyo na kuelekea kwingine.

Ncimbi yupo hapo alipo sasa hivi ili njia iliyopo iendelee. Inaeleweka na hilo ndilo tatizo la yeye kutoaminika kwa wepesi juu ya haya anayoyasema sasa hivi.

Sasa namhimiza na kumshauri, aanze kuzungumzia huko aliko, na mfumo unaoendeleza matatizo haya yanayowakabili waTanzania.

Yoote aliyozungumzia hadi wakati huu, kama haya ya Katiba Mpya na sheria mbalimbali ni maswala yaliyo nje ya mfumo unaoendeleza uovu.

Ili aeleweke bila ya mashaka mengi kwa waTanzania, hana budi ageukie maswala yaliyopo huko ndani ya CCM, chama ambacho kundi limeamua kukinyang'anya na kufanyia uovu wake.

Akielekeza juhudi zake huko, nipo tayari kabisa kufungua masikio yote na kumsikiliza anasema nini.

Emmanuel Nchimbi halii peke yake. Tumemsikia mara kadhaa yule mwingine wa kule Mahakamani akililia nyikani.
Ni nani ajuae, pengine Nchimbi akisikika zaidi kwa mayowe yake, hata akina Camillius Wambura tutaanza kusikia visauti vyao, hata kama vitakuwa hafifu. Akina Generali Mkunda na wengi wengine wa aina hiyo wataanza kujitokeza, na kuungana na juhudi za waTanzania wengine kulikomboa taifa hili toka mikononi mwa hili kundi hatari sana lililoshikilia nchi yetu sasa hivi.

Tumtie nguvu asikike, tusimkatishe tamaa na kumwacha mikononi mwa waovu wazidi kumtumia kwa manufaa yao.
Mwaliu Nyerere aliwahi kusema kuwa mabadiliko ya kweli yatatokea ndani ya CCM.
Huenda ikawa Nchimbi kachimba chini kwa chini hadi kuibuka na Ajenda ya Wapinzani na wanaharakati akiwa ni kiongozi mwandamizi katika Serikali na Kigogo cha CCM alliyekwisha shilia nafasi Kadhaa nyeti ikiwemo Katibu mkuu .

Mimi nadhani sauti za wafu zinamlilia Samia na wenzake ndani ya CCM na kwa hiyo hawana budi kusaalimu amri angalau kwa kule kukubali kuleta mchakato wa katiba kwa nguvu mpya.

La muhimu hapa ni si malumbano tena wala mivutano, bali ni kuwa karibu na wadau wote wa kuandaa mchakato huu ili ujulikane utaanzia wapi na utawashirikisha vipi Wanaharakati na wapinzani,
Bila kufanya maandalizi ya kujisogeza karibu , CCM wanaweza kumonopoly mchakato wenyewe kama walivyo fanya zama zile za Warioba na kikwete..

Natamani katiba mpya zamu hii IANDALIWE NA WANASHERIA WATUPU WA PANDE ZOTE ZA MUUNGANO WAKIWEMO WANASHERIA WAWAKILISHI WA VYAMA VYA SIASA NA WADAU WENGINE WELEDI WA SHERIA NA UTAALAMU WA KATIBA.

Baada ya kuandaliwa rasimu na kuridhiwa huko juu na weledi ndio waletewe wasanii na wauza mahindi na dagaa , watu wa mitaani kwa kura ya maoni tuu.

Pawepo na jukwaa wazi la maoni wakati wa mchakato wa weledi ukiendelea ambalo kila pendekezo liwafikie wataalamu na kulifanyia kazi.

BUNGE LA KATIBA KAMA LILE LA ASHA BAKARI NA JUSA WALIPOKUWA WAKIPIGANA VIJEMBE LISIWEPO TENA.

NAWAKILISHA
 
"Ndugu" Emanuel Nchimbi kwa sasa hivi namchukulia kuwa ni mfungwa kama tulivyo wengine wote, waTanzania tusiofurahishwa na mwenendo na mwelekeo wa taifa letu ulivyo kwa sasa.

Sina shaka yoyote, kwamba wapo wengine wengi huko huko aliko Nchoimbi ambao hawajapata ujasiri wa kusema, kama anavyofanya yeye sasa hivi.

Nataka Nchimbi uwe mfano kwa hao waliokaa kimya kwa sababu mbalimbali na wao waseme au waonyeshe mfano kwa njia yoyote waonyeshe kuwa hali iliyopo nchini mwetu sasa hivi haifai kuliko kubaki kimya.

Nchimbi anayezungumza sasa hivi, ni tofauti "kidogo" na Nchimbi aliyekaa kimya na kuwa mshiriki na kutumiwa kuwakandamiza waTanzania.

Pamoja na kwamba wengi tutabaki na wasiwasi juu ya haya anayoyazungumzia, kuwa ni mbinu zilezile zinazotumiwa na hili kundi ovu, yakilenga kuendeleza utawala uleule uliosababisha haya ya leo, inatubidi tumpe fursa ya kumsikiliza na kumwelewa kabla ya kuhitimisha lengo hilo la kuendeleza hila.

Ni muhimu tuelewe tumefika hapa tulipo kwa njia gani, ili tuweze kubadili njia hiyo na kuelekea kwingine.

Ncimbi yupo hapo alipo sasa hivi ili njia iliyopo iendelee. Inaeleweka na hilo ndilo tatizo la yeye kutoaminika kwa wepesi juu ya haya anayoyasema sasa hivi.

Sasa namhimiza na kumshauri, aanze kuzungumzia huko aliko, na mfumo unaoendeleza matatizo haya yanayowakabili waTanzania.

Yoote aliyozungumzia hadi wakati huu, kama haya ya Katiba Mpya na sheria mbalimbali ni maswala yaliyo nje ya mfumo unaoendeleza uovu.

Ili aeleweke bila ya mashaka mengi kwa waTanzania, hana budi ageukie maswala yaliyopo huko ndani ya CCM, chama ambacho kundi limeamua kukinyang'anya na kufanyia uovu wake.

Akielekeza juhudi zake huko, nipo tayari kabisa kufungua masikio yote na kumsikiliza anasema nini.

Emmanuel Nchimbi halii peke yake. Tumemsikia mara kadhaa yule mwingine wa kule Mahakamani akililia nyikani.
Ni nani ajuae, pengine Nchimbi akisikika zaidi kwa mayowe yake, hata akina Camillius Wambura tutaanza kusikia visauti vyao, hata kama vitakuwa hafifu. Akina Generali Mkunda na wengi wengine wa aina hiyo wataanza kujitokeza, na kuungana na juhudi za waTanzania wengine kulikomboa taifa hili toka mikononi mwa hili kundi hatari sana lililoshikilia nchi yetu sasa hivi.

Tumtie nguvu asikike, tusimkatishe tamaa na kumwacha mikononi mwa waovu wazidi kumtumia kwa manufaa yao.

View: https://vm.tiktok.com/ZSXKo72mQ/ This post is shared via TikTok Lite. Download TikTok Lite to enjoy more posts: TikTok
 
Hata Samia enzi za Magufuli iliwahi kuzushwa alikuwa akitaka kujiuzulu kutokana na kutokubaliana na ukandamizaji wa boss wake na pia alienda kumsalimia Lissu Nairobi Hospital na kuonana naye Ubelgiji, kiko wapi.
Mimi sijui urafiki wa Samia na Lisu ulianzia wapi na Uadui wao umekuja kivipi.

Hizi siasa zina mauza uza mingi sana.

Namuoba Antipasi lisu apunguze kutunisha msuli , karibu ataachiwa huru.
Mama anamjali sana, ila nadhani amemuweka ndani kwa Usalma wake. Maana Wauwaji waliompiga risasi enzi za Magu bado wapo mtaani walikuwa wanataka kumalizia kazi.

Naomba Amani kwa wote
 
Lissu yuko gerezani, hawezi kusoma ujumbe wako.
 
Back
Top Bottom