chilumendo
JF-Expert Member
- Oct 26, 2013
- 3,434
- 4,500
Alishawahi pinga hadharani kamati kuu kumuengua lowassaWala hawatofautiani sana, labda elimu na utamaduni tu.
Umewahi kumuona Nchimbi akiwa na msimamo wa jambo lolote kubwa la maana kabla hajawa makamu wa Rais?
Huo ulikuwa ni mchuano wa kuwania ulaji tu, halikuwa jambo lenye maslahi yoyote kwa raia au nchi.Alishawahi pinga hadharani kamati kuu kumuengua lowassa
Mwaliu Nyerere aliwahi kusema kuwa mabadiliko ya kweli yatatokea ndani ya CCM."Ndugu" Emanuel Nchimbi kwa sasa hivi namchukulia kuwa ni mfungwa kama tulivyo wengine wote, waTanzania tusiofurahishwa na mwenendo na mwelekeo wa taifa letu ulivyo kwa sasa.
Sina shaka yoyote, kwamba wapo wengine wengi huko huko aliko Nchoimbi ambao hawajapata ujasiri wa kusema, kama anavyofanya yeye sasa hivi.
Nataka Nchimbi uwe mfano kwa hao waliokaa kimya kwa sababu mbalimbali na wao waseme au waonyeshe mfano kwa njia yoyote waonyeshe kuwa hali iliyopo nchini mwetu sasa hivi haifai kuliko kubaki kimya.
Nchimbi anayezungumza sasa hivi, ni tofauti "kidogo" na Nchimbi aliyekaa kimya na kuwa mshiriki na kutumiwa kuwakandamiza waTanzania.
Pamoja na kwamba wengi tutabaki na wasiwasi juu ya haya anayoyazungumzia, kuwa ni mbinu zilezile zinazotumiwa na hili kundi ovu, yakilenga kuendeleza utawala uleule uliosababisha haya ya leo, inatubidi tumpe fursa ya kumsikiliza na kumwelewa kabla ya kuhitimisha lengo hilo la kuendeleza hila.
Ni muhimu tuelewe tumefika hapa tulipo kwa njia gani, ili tuweze kubadili njia hiyo na kuelekea kwingine.
Ncimbi yupo hapo alipo sasa hivi ili njia iliyopo iendelee. Inaeleweka na hilo ndilo tatizo la yeye kutoaminika kwa wepesi juu ya haya anayoyasema sasa hivi.
Sasa namhimiza na kumshauri, aanze kuzungumzia huko aliko, na mfumo unaoendeleza matatizo haya yanayowakabili waTanzania.
Yoote aliyozungumzia hadi wakati huu, kama haya ya Katiba Mpya na sheria mbalimbali ni maswala yaliyo nje ya mfumo unaoendeleza uovu.
Ili aeleweke bila ya mashaka mengi kwa waTanzania, hana budi ageukie maswala yaliyopo huko ndani ya CCM, chama ambacho kundi limeamua kukinyang'anya na kufanyia uovu wake.
Akielekeza juhudi zake huko, nipo tayari kabisa kufungua masikio yote na kumsikiliza anasema nini.
Emmanuel Nchimbi halii peke yake. Tumemsikia mara kadhaa yule mwingine wa kule Mahakamani akililia nyikani.
Ni nani ajuae, pengine Nchimbi akisikika zaidi kwa mayowe yake, hata akina Camillius Wambura tutaanza kusikia visauti vyao, hata kama vitakuwa hafifu. Akina Generali Mkunda na wengi wengine wa aina hiyo wataanza kujitokeza, na kuungana na juhudi za waTanzania wengine kulikomboa taifa hili toka mikononi mwa hili kundi hatari sana lililoshikilia nchi yetu sasa hivi.
Tumtie nguvu asikike, tusimkatishe tamaa na kumwacha mikononi mwa waovu wazidi kumtumia kwa manufaa yao.
"Ndugu" Emanuel Nchimbi kwa sasa hivi namchukulia kuwa ni mfungwa kama tulivyo wengine wote, waTanzania tusiofurahishwa na mwenendo na mwelekeo wa taifa letu ulivyo kwa sasa.

Mimi sijui urafiki wa Samia na Lisu ulianzia wapi na Uadui wao umekuja kivipi.Hata Samia enzi za Magufuli iliwahi kuzushwa alikuwa akitaka kujiuzulu kutokana na kutokubaliana na ukandamizaji wa boss wake na pia alienda kumsalimia Lissu Nairobi Hospital na kuonana naye Ubelgiji, kiko wapi.
Lissu yuko gerezani, hawezi kusoma ujumbe wako.Mimi sijui urafiki wa Samia na Lisu ulianzia wapi na Uadui wao umekuja kivipi.
Hizi siasa zina mauza uza mingi sana.
Namuoba Antipasi lisu apunguze kutunisha msuli , karibu ataachiwa huru.
Mama anamjali sana, ila nadhani amemuweka ndani kwa Usalma wake. Maana Wauwaji waliompiga risasi enzi za Magu bado wapo mtaani walikuwa wanataka kumalizia kazi.
Naomba Amani kwa wote