Ndio waumini inabidi watetewe pale dhuluma inapofanyika, lakini kabla ya kufika huko unajua Idara ya habari ya kanisa katoliki inavyofanya kazi?
Ndio Tundulisu alipigwa risasi na jambo hilo ni dhuluma kila mtu analitambua lakini unajua kwamba pale Lisu profile yake ilikuwa inasomeka kama political figure?Unajua kanisa limeelezwa nini when dealing with politics?
Ndio, kanisa ilibidi liseme chochote kwa maana Lisu mbali ya kuwa na profile yake ya kisiasa bado ni muumini na mtanzania mwenzetu.Swali ni kuwa una uhakika kanisa alikusema chochote? au kwasababu hukuwaona wakiita waandishi wa habari?.Ukweli ni kwamba kanisa katoliki lilisema na linaendelea kusema na jambo hili linafanyika katika ibada za kila siku kupitia mafundisho ya Misa