Nahisi baba anataka kugawa urithi bila kunishirikisha. Naombeni msaada

Nahisi baba anataka kugawa urithi bila kunishirikisha. Naombeni msaada

WAKUU, NAOMBENI MPITIE NYUZI ZA NYUMA ZA HUYU JAMAA.

KWANZA HANA HIYO MIAKA ALIYOIANDIKA HAPO. PILI AMEHANGAIKA SANA KUTAFUTA AJIRA PASIPO MAFANIKIO.

HIVYO NI MTU AMBAYE ANAHITAJI MSAADA WA KIMAWAZO ZAIDI KULIKO PESA, NADHANI KUTOKANA NA STRESS ANASHINDWA KUFANYA DECISIONS SAHIHI.

NYIE MDHIHAKINI ILA MSIJE RUDI NYUMA NA KUFUTA COMMENTS HUKU MKIANDIKA RIP BAADA YA KUFANYA YAKE.
Unforgetable

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka 38 ni mtu mzima wewe. Baba anajua akikupa urithi utapeleka kwenye chama cha mboga mboga.

The true revolution comes from inside yourself....!
 
Jf unatakiwa usome maandiko then utumie akili yako kuchambua kilichoandikwa na hapa ndio utaona wenye akili ndogo wanang'ang'ana kutukana na mtoa mada utakuta yuko pembeni anawacheka sana. Hivi unaanzaje kuumia na kutukana kwa mtu usiyemfahamu na kwa habari usiyokuwa na uhakika nayo?

Acheni umburula jamaa kaamua kuwa anawalisha matangopori humu ili aone uelewa wenu ulivo mdogo
Inaweza kuwa kweli au sio kwelj lakini unadhani kilichoandikwa hakipo kwenye jamii?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habarini za siku, mimi ni kijana wa miaka 38 nadhani uko nyuma nilileta uzi wangu mnishauri maana baba alinifukuza kwake nilipokuwa nakaa kisa tu nilimshawishi awe na kadi ya Chama Cha Mapinduzi ambacho mimi ni mwananchama wake mtiifu aligoma na kunifukuza kwake.

Nilichoshangaa baba baada ya kunifukuza na kutafuta mtu wa kukaa mlangoni (mlinzi) kama ili kuzuia yeyote mgeni kuingia ndani bila ruksa nikiwepo mimi, jana jioni nasikia baba ameitisha kikao cha ndugu zangu wengine pasipo kuniita na mimi kwenye kikao kile.

Nasikia baba amegawa mali zake kwa wadogo zangu, naumiaa sana ndugu zangu wana jamiiforum nisaidieni, nahisi kufa naombeni mnishauri njia nzuri ya kwenda kumfungulia jarada mahakamani, mimi ni mtoto wake kabisa, kwanini hanishirikishi kwenye hizo mali, wakati mimi ni mkubwa nina uchungu na hasira sana, naombeni mawazo yenu wakuu.

Kwa sasa nipo kwa rafiki yangu nakaa kwao, sina pa kuanzia wakuu maana pale nilikuwa nimepanga kodi iliisha na kazi sina kabisa, rafiki yangu ameniambia nipigane juu chini nipate na mimi sehemu ya mali ili niweze kuanzisha maisha yangu.

Wataalamu wa sheria, na haki za vijana na urithi nisaidieni, mtoto wenu nataka kuzurumiwa na baba yangu kweupe kabisa
Tafuta mali zako ili nawewe ukitaka kugawa usiingiliwe.Tatizo mnapenda vya bure ndo maana mnolewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sikuvunji moyo lakini wataalamu wa ulimwengu wanasema kuwa ukiisha vuka 35 yrs bila kutoboa huko uendako usijihangaishe tena. Swali la kijinga, Hivi weye 38 una watoto wangapi? Babako ana miaka mingapi?? Umesema weye ndo wa kwanza mwenye 38 Je babako alikuwa na miaka mingapi alipokupata? ; Nadhani amekuona sio rizki. Nenda tu Lumumba ukaombe kukaa mle mle mjengonii
Kwenye kutoboa nàkupinga usiwakariri hao wataalamu wa ulimwengu age is just a number Mengi alitoboa akiwa na 47, mmiliki bilionea wa KFC katoboa akiwa na 60+

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama wakati anajenga ulimchangia hata matofali mawili,mtagawana, kenge we tafuta zako,ukifa watoto wako watakaa wapi?
 
Mwanachama wa CCM mwenye umri wa miaka 38 analilia mgao wa mali....maana sio urithi kwa sababu mzee hajafa. Kama yupo hai anawapa mwenyewe we huna cha kudai. Kausha.
 
Pole sana ila kauli yangu sio nzuri samahani sana kwa kusema ivi.

Miaka 38 unakaa kwa rafiki, ata kodi imekushinda kulipa, baba ako ana akili sana kutokupa ata bakuri ya urithi maana utaviuza kabla hajazikwa.

Ushauri tafuta pesa zako kwa nguvu, akiona tuu umepata ata kiwanja, au geto, mzeee wako atakupa ata nusu ya mali ake maana ana uhakika utaiendeleza ila sio saivi anakuona kaaa ***** vile.
 
Nimepekua nyuzi zako

Yaani roho yako iko kama jina lake... kweli wewe ni kikohozi.

Babako umemdai pesa lakini mali zake unazitaka? Acha ubinafsi.

Na nadhani babako kachukia kwakuwa ulimdai pesa ulizomkopesha muda mrefu, imemuuma kama mzazi. Yaani miaka imepita umepata kazi, umekaa kwake bado umemdai arudishe pesa zako ..kaumia sana...hata Mimi ningeumia sana.

Cha msingi wewe nenda mpigie magoti babako umwombe msamaha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habarini za siku, mimi ni kijana wa miaka 38 nadhani uko nyuma nilileta uzi wangu mnishauri maana baba alinifukuza kwake nilipokuwa nakaa kisa tu nilimshawishi awe na kadi ya Chama Cha Mapinduzi ambacho mimi ni mwananchama wake mtiifu aligoma na kunifukuza kwake.

Nilichoshangaa baba baada ya kunifukuza na kutafuta mtu wa kukaa mlangoni (mlinzi) kama ili kuzuia yeyote mgeni kuingia ndani bila ruksa nikiwepo mimi, jana jioni nasikia baba ameitisha kikao cha ndugu zangu wengine pasipo kuniita na mimi kwenye kikao kile.

Nasikia baba amegawa mali zake kwa wadogo zangu, naumiaa sana ndugu zangu wana jamiiforum nisaidieni, nahisi kufa naombeni mnishauri njia nzuri ya kwenda kumfungulia jarada mahakamani, mimi ni mtoto wake kabisa, kwanini hanishirikishi kwenye hizo mali, wakati mimi ni mkubwa nina uchungu na hasira sana, naombeni mawazo yenu wakuu.

Kwa sasa nipo kwa rafiki yangu nakaa kwao, sina pa kuanzia wakuu maana pale nilikuwa nimepanga kodi iliisha na kazi sina kabisa, rafiki yangu ameniambia nipigane juu chini nipate na mimi sehemu ya mali ili niweze kuanzisha maisha yangu.

Wataalamu wa sheria, na haki za vijana na urithi nisaidieni, mtoto wenu nataka kuzurumiwa na baba yangu kweupe kabisa
Sasa hapo anataka kuku dhurumu kitu gani wakati Mali ni za kwake,ninacho kushauri wewe pambana na maisha bado kijana utapata pa kuanzia au kama vipi toka huo mkoa nenda mkoa mwingine kajichanganye huko achana na kufikiria mambo ya urithi wakati yeye hakurithi alipambana na wewe pambana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hivi unawezaje kukaa unavizia urithi. tafuta zako we ni mtu mzima. katika vitu ambavyo huwa sifikirii ni mgao wa urithi. kwanza we ni CCM mmeiba sana inatosha
 
Back
Top Bottom