Nahisi kama nimefikia hatua ya Kukata Tamaa kiwango cha Mwisho. Naomba msaada wenu Ndugu zanguni

Status
Not open for further replies.
Pole sana ndugu yangu kwa masaibu unayopitia! "Wanaume tumeumbwa, mateso....."!

Kitu kimoja nimekiona katika simulizi yako, wewe ni mpambanaji na unayejielewa. Kama walivyosema baadhi, vema uuze/weka rehani nyumba uliyoanza jenga ili upate mtaji wa kuanzia. Mshirikishe mke wako katika hili kwani isije leta tafrani mbeleni kwani ni nyumba ya
familia. Waweza pia uza gari kwani kwasasa inazidi kutoboa mfuko wako japo najua kuwa unaumwa!

Nimeona wewe ni mpambanaji, kubaliana na hali halisi, ajira ni ngumu kwa sasa maana kampuni nyingi zinapunguza/achisha wafanyakazi! Using'ang'anie kuajiriwa ofisini, buni mradi (kilimo, ufugaji au anzisha kampuni utakayo kuwa unafanya consultancy) ambao unaweza kuumudu. Baba yako ni mstaafu, kwa kilimo chake bado anaweza kumudu kukutumia pesa japo kidogo.....unaonaje kama utaamua kuungana naye (kama ana eneo la kutosha) kuboresha na kukifanya kiwe cha tija? Naomba nikupe kisa kimoja cha rafiki yangu.

Ninaye rafiki yangu mmoja ambaye kimaisha alikuwa juu mno kwani alikuwa anaendasha kampuni fulani ya consultancy ktk mji fulani. Huyu ni mtu aliyemiliki gari kadhaa ikiwemo Vogue, anamiliki nyumba kadhaa na watoto wake wanasoma nchini Marekani. Kwa ujumla yeye na mke wake waliishi maisha ya kifahari sana. Inaonekana huyu ndugu yangu alikuwa akikwepa kulipa kodi ya serikali kwa muda mrefu, hivyo mwaka jana TRA walizifunga akaunti zake zote! Hakubaki hata na senti moja! Nyumba na magari kumbe alikuwa kayaweka reheni....kwa ujumla alipitia kipindi kigumu sana. Ada ya watoto imekuwa shida hivyo wamerudi nchini. Mke japo anajishughulisha na biashara lakini hana msaada wowote kwa mumewe. Rafiki yangu huyu ni jasiri, alikubaliana na hali halisi akaweka umaarufu wake kando, nakuamua kujishusha. Haoni aibu kukwambia uko wapi nije uninunulie Safari moja..... Aliwashirikisha watoto wake hali halisi na wameridhika. Kwasasa amebuni mradi mpya njee kabisa ya Taaluma yake na muda sio mrefu mradu huu utaanza kumlipa.

Jipe moyo, una ndugu na marafiki ambao bado wanakupa support. Jitahidi kuwasiliana na watoto wako mara kwa mara na hasa huyo ambaye hataki kuongea na wewe. Mueleweshe aelewe. Ninauona uchungu unaaoupata kuona watoto wako wako ukweni (kwa mtu wa kanda ya ziwa ni aibu).

Pole sana.....Usimsahau Mungu kwani kwake hakuna lisilowezekana!
 
Angalau wewe familia yako iko sehemu salama na watoto wanaishi bila shida.

Kuna wengine hatujui hatma ya watoto wetu huko waliko maana hata hela ya kununua unga wa uji ni mtihani.

Na unasema kabisa uliuza magari mawili. Yaani unakua na magari zaidi ya moja na huna kwako? Samahani sikusemi vibaya ila huenda ndio maana kampuni yenu ilishindwa kuendelea kwakua inaonekana hamjui kuona mbali
 
Pole sana mkuu, yatapita haya
Hii ndo changamoto ya kampuni binafsi, hiki kisa kinaweza kutupata hata sisi wengine,
Mkuu nakuombea kwa Mwenyezi Mungu

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
 
Ulitaka amchukue ukweni pamoja nae? hata hilo la kuchukua watoto na vitu amemsaidia.
 
Pole ndugu,,, mungu ana makusudi yake jaribu kutambua funzo analokupa leo ili rizki yako ikirudi uwe imara has a katika kuwekeza nguvu zako kwa Mungu.

Nimeona mlikuwa n ujenzi wa nyumba je kwanini msiiuze uanze biashara? Au ukopee mkopo hiyo nyumba?
Hahaha yani unamshauri aongeze urefu wa kaburi lake?!

Basi ungeisema na hiyo biashara anayotakiwa kuifanya.

Binafsi ningesema labda aimalizie hiyo nyumba hata chumba kimoja, kwa hizo pesa za mafuta apate pa kuweka ubavu, kuliko kuchoma pesa kwa kuweka mafuta kwenye gari na huna pa kwenda kuzalisha.
 
Akiuza gari ana mguu mbovu hujamwelewa?
 
Kua na elimu na kukosa kazi isikufanye kukata tamaa hadi kuwaza kumeza vidonge vingi ili kukatisha maisha hapana wewe bado sana mbona mtaani watu waio na elimu wana survive na ukiangalia kazi wanazofanya ni za kawaida sana ila wanapambana hivyo basi usikate tamaa na amini kwa miujiza ya Mungu utainuka tena na utakua pamoja na familia yako, kikubwa ni kutokata tamaa pambana tu.
 
Taatizo vijana mnakariri...eti usikosee kuoa...kwani ukikosea kuoa ndiyo mwisho wa maisha ?Hakuna tatizo lisilo na dawa....mimi niilikosea kuoa ..miaka imepita na sasa nasonga kifua mbele...mambo yananyooka baada ya kutupa kule
 
Una gari, una nyumba haijakamilika una degree bado unafikiria kujiua kweli wasomi waleo ni afadhali ya darasa la saba hivi huyu mlemavu hana nyumba hana gari wala elimu kama yako bado anaishi wewe una raslimali zote hizo eti unafikiria kujiua kweli akili yako ni ndogo tofauti na elimu uliyonayo. Msomi mwenye kiwango cha degree hawezi babaika kama unavyohaha wewe wewe. Uza hicho kigari chako nunua pikipiki uingie uba uishi chenji malizia chumba kimoja hilo pagale lako hamia toka kwa rafiki yako unakuwa mzigo. Changamoto kidogo unababaika kama hukusoma na ukizubaa kweli kwa ujinga wako utajiua na mimi nasema kufa tu na ujinga wako elimu uliyo nayo haijakusaidia wewe wala familia yako unatesa watu bure NASEMA TENA SIUNGI MKONO HOJA YA WEWE KUJIUA ILA KAMA UTATHIBITISHA KUWA WEWE NI FALA HAPO JIUE LAKINI KAMA UNA AKILI TIMAMU HAYO MAWAZO TUPA CHOONI SONGAMBELE TPX JIHADHALI TPX NAFUTIKA BADO MMOJA
 
Sijawahi juta kuwahudumia wazazi wangu,wake zetu ni marafiki zetu na sio ndugu zetu tusiwape mioyo yetu 100%
 
HATA WANAOKUPA POLE WANAKUPUMBAZA UNAJIONA UNA TATIZO KUBWA SANA KULIKO UWEZO WAKO MPAKA UNALIALIA ILA UKWELI HUNA TATIZO KUBWA KAMA UNAVYOLINADI BALI UFAHAMU WAKO NA AKILI YAKO INAKUAMINISHA HIVYO, NAOMBA NENDA MUHIMBILI HOSPITAL UKITOKA HAPO NENDA MAHAKAMANI UKITOKA HAPO NENDA KUTEMBELEA WAFUNGWA GEREZA LOLOTE KISHA RUDI KAAA KWA HUYO RAFIKI YAKO UJIULIZE WEWE NA WALE ULIOKWENDA KUWAONA KWENYE MAJENGO YA SERIKALI NANI ANA MATATIZO KISHA UJE ULETE HAKO KAHADITHI KAKO HAPA JF. TENA MARA MIA USINGESEMA UNA ELIMU KIWANGO CHA DEGREE NINGEKUELEWA LAKINI KAMA WASOMI NDIYO MNAKUWA WAJINGA KIASI HIKI HAKUNA SABABU YA KUSOMESHA WATOTO BORA WACHUNGE MBUZI NA KONDOO WATAKUWA BRIGHT KULIKO KUWA NANGA KAMA WEWE NATUMIA LUGHA KALI ILI NIKU PROVOKE UCHUKIE UTOKE KWA RAFIKI YAKO UNAMTILIA KIWINGU NAYE KWA UJINGA ANAFIKIRI ANAKUSAIDIA KUMBE ANAAKUPUMBAZA. WASOMI WA LEO SIYO CREATIVE MMEKAA NA KUAAMINI KAZI ZA KITUMWA KUJIAJIRI HAMUWEZI ETI MAPA UNAFIKIRIA KUJIUA HAPO NDIYO UMETHIBITISHA KUWA ELIMU ULIYO NAYO HAINA MANUFAA KWA JAMII WALA KWAKO NA FAMILIA YAKO MAANA YA ELIMU NI KUPAMBANUA MAMBO MAGUMU YOTE NA KUYAPATIA MAJIBU NA SIYO KULIALIA MKE ANAPOTEZA FEDHA WEWE UNAKENUA SASA KWA TAARIFA YAKO HUKO ALIKO ANA BWANA MWINGINE NA HANA MUDA NA WEWE NA WAKWEZO WAKO UPANDE WA YULE BWANA HASA MAMA MKWE WAKO. KAA UKILIALIA UTASHANGAA ANA MIMBA IT IS MATTER OF TIME NDIYO UTAJITUNDIKA NA MCHEZO UISHE. MIMI DARASA LA SABA POKEA USHAURI WANGU UZA KIGARI CHAKO NUNUA PIKIPIKI KAMA NI LAZIMA UWE NA USAFIRI KWA SABABU YA MGUU CHENJI IKIBAKI PAUA CHUMBA KIMOJA WEKA GENGE LA NYANYA NA MIHOGO YA KUKAANGA UTOKE KWA RAFIKIO TOFAUTI NA HIVYO UNATAKA KUGOMBANA NA RAFIKI YAKO. NDHANI UTAKUWA UMESOMA ENGLISH MIDIUM WEWE PRODUCT AMBAYO HATA MENDEA AKIINGIA NDANI UNAMUITA JIRANI AJE KUMTOA "TPX JIHADHALI'' "TPX NAFUTIKA'' BADO MMOJA
 
Acha uboya soma vizuri. amesema amejenga nyumba ambayo haijakamilika.kwani hata akiwa ame rent nyumba kuna kosa akisema home ?
Wewe ndio boya kabisa, huoni kasema kafukuzwa ktk nyumba aliyopanga
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…