Nahisi kama nimefikia hatua ya Kukata Tamaa kiwango cha Mwisho. Naomba msaada wenu Ndugu zanguni

Nahisi kama nimefikia hatua ya Kukata Tamaa kiwango cha Mwisho. Naomba msaada wenu Ndugu zanguni

Status
Not open for further replies.
Ushauri wangu kwa hiyo michango kidogo utakayo pata, jaribu ata kusaka vijana ata wawili wa kigogo kutoka dodoma wakuuzie kahawa.
Ina lipa sana ile mkuu, au vijana waku sambazie mayai ya kuchemsha.
Vijana wasumbufu sana wanaweza tembea na mtaji, anatakiwa ayafute shughuli ya kufanya mwenyewe ndio apanue mradi kuajili vijana hata wakitoroka anakijiwe chake cha kudumu.
Mkuu minawazo lingine ufanye udobi wa kuzunguka not stationary office ambapo unaweza fanyia pale kwenye pagale lako, gari itakusaidia kuchota maji na kutafuta nguo majumbani .Hio huduma binafsi nimewahi waza kuifanya ila nilikosa mda.Kama umesoma Hapo dar vyuoni kuna watu hawana mda unaweza kuanzisha hio hudima vyuoni na majumbani.Kuna watu wako busy sana hapo dar.Pita maofisi sambaza vipeperushi huenda ukaokota watu kadhaa.Udobi hautaji mtaji mkubwa ni sabuni na kemikali for dry cleaning ambazo unaweza agiza mtandaoni bei yake sio Kali.Mkuu hili wazo unalionaje?
Nakushauri wazo la kazi ya kuajiliwa achana nalo, think about creating your own empire, it is difficult but fight against all odds!!
 
Pole sana kaka, hakika utanyanyuka...

Ila ulifanya makosa sana kumiliki magari matatu wakati unakaa nyumba ya kupanga. Huyo mkeo pia mwangalie kwa makini, yawezekana ndio wale wanawake wa mjini wanaopenda maisha ya anasa..

Pole sana, Maisha ni mapambano usikate tamaa na huu ndio wakati sahihi wa kuwajua marafiki zako wa kweli..
Kosa kubwa lilifanyika hapa na ndio majuto yanaanzia hapa. Kwa nini wasimalize nyumba kwanza?

Kuna mengi ya kujifunza kwenye hii mada. Mtoa mada usikate tamaa ila kwa Sasa usijute. Nashauri urudi mwanza kwa mzee na ukae huko ukijipanga plan B ila uwe kwa wazazi sio mtu baki. Dunia Ina mapito na yatapita usiuze hiyo site
 
Mimi kwanza nikupe pole halafu nikulaumu kwa kuwa na mawazo mgando na ya kijinga kama hao humu jf huwa mnatiuita ma layman sisi tusioenda shule lakini akili ya mtaa ipo full hiyo kw mfano una gari ukiuza hata 2mil tu ukanunua lone zako tatu za tigo voda na aetel ukatega sehemu yenye watu wengi kwa kibinda cha mpesa wallai kwa maisha ya dar es salamm hukosi hela ya kula wala kodi ya chumba kimoja cha tsh 40 hapo bunju tatizo akili yako imeganda status ile ile ambao leo haipo tena .njoo vijijini mjofunze kwa walimu unakuta mwl ana ajira analima ,anafuga , anafanya biashara ndogondogo na mambo yanaenda safiii kabisa mwisho.HUNA MKE WEWE UNA COVID 19.usiku mwemA.
Umemfokea[emoji15]
 
huu ni UTOPOLO MWINGINE,jamaa kashaseme hivi vitu vyote vimemkuta tu hakutegemea na kajitahidi kuweka sawa ikashindikana sasa wewe unaanza kumuhesabia hivyo vigari ashauza na nyumba sijui kila kitu kapoteza vya nini,NYIE NDO WATU MNA MATUMBO MAKUBWA HUKU AKILI YENU ROBO KILO HAIFIKI

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
To be honest, namshukuru sana Mungu kwa aina ya mke alie nipea.
Najua hajakamilika, lakini hakika ni wakipekee sana nikilinganisha na changamoto ambazo wengi wanapitia na wake zao.
Anyway, pole sana mkuu na hakika ningekua na connection ningekuunganisha kwa bidii zangu zote.
Ebu naomba namba zako PM
Hongera mkuu. Hii kikwazo cha mwenza anayefaa mke/mume ukiona umekivuka kufanikiwa kuna possibility kubwa.
 
Soma tena ujumbe wangu, this is a social platform. Ni ujumbe kwa kila mtu, kama wewe haukufai yupo unaemfaa.

Wanaume mkishika pesa msijisahau tu, kuna kesho na mkeo ndio aweza kuwa msaada wako mkubwa au akakuzidishia depression kulingana na ulivyokuwa unamtreat.

BTW wewe ulivyonitukana ndio umenisaidia? Au hapo hujatumia maneno umetumia maji eeh!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Nadhani wengi tumekuelewa. Kusema alimpa mil 6 haimaniishi alikuwa anamjali sana. Inawezakane kulikuwa na namna aliyokuwa anam-treat wakati ana fedha. Pia inawezekana ni mke mapepe tu hatuwezi kujua kwani hapa tumesikiliza upande mmoja. Kuwa na amani kwani hapa mtu unaweza kushambuliwa kwa kusema ukweli.
 
Kwakweli mkuu, na by nature sisi wanaume tunapo pata utulivu wa ndani, basi hata akili hutulia sana naku focus kwenye mambo ya msingi.
Nakuelewa kabisa. Nakuelewa kwa sababu kinyume chako wewe mimi nilipata asiye na utulivu hivyo najua madhara yake. Hasa unapokuwa kwenye hali mbaya ya kifedha na nyumbani hakuna amani unaweza kuomba poo.
 
Kuna suala moja la kujifunza kwenye mkasa wa huyu bwana,jamani tusidanganyane ukipata nafasi ya kushika hela jenga hata ka nyumba ka chumba na sebule ili likitokea la kutokea uwe na sehemu iitwayo kwako.Nimeshangaa sana ndugu yangu huyu ana gari tatu ila anaishi kwenye nyumba ya kupanga HII NI AIBU KUBWA SANA!!!! Na asilimia kubwa ya vijana ndio aina ya maisha yetu TUNAPENDA TUONEKANE TUNA DRIVE MA NDINGA HUKU UMEPANGA CHUMBA NA SEBULE kibaya zaidi una familia,my friend mambo yakibadilika familia haiwezi kuishi kwenye gari NDIO MAANA MKE ALIAMUA KUKIMBIA NA FAMILIA KWA KUWA ALIONA BABA HANA SEHEMU YA KUISHI NA KWENYE NYUMBA KAFUKUZWA!!!
Hivi unajua kuna watu wengi wamejinyongea kwenye nyumba zao kwa matatizo kama haya? Nachotaka kusema ni kuwa, hata kuwa nyumba kwenye tatizo kama hili inaweza isiwe suluhisho na badala yake ikawa kero zaidi hasa unapokuwa na mke/mume kichwa maji
 
Pambana kijana....mm ilinikuta iyo nipo na bajaj moja na gari tipper moja yakubeba mchanga cjasoma story yako mpaka mwisho ila pambana usisubiri kupata ajira man kazaaa mkubwa mwenzangu
 
Hizi article zako mbili za Jan na Feb 2020 hazi support haya matatizo yako, yanaonyesha unamiliki nyumba na ulikua kazini mpaka Feb,2020
Screenshot_20201201-205244.jpg
Screenshot_20201201-205217.jpg
 
Kama nmekuelewa vizuri bado una gari unalolitumia ambalo lilikataliwa kuwa uber.

Sasa nakushauri uza hilo gari ili hela utayopata uwe ndio mtaji wa kuanzia.
Alafu inakuwaje mtu una magari hadi 3 alafu hunxa nyumba bado umepanga?
 
Kama huna uzoefu wa biashara sikushauri kuuza nyumba. Hiyo iache. Tena iache kabisa hata usichukulie mkopo.IACHE KAMA ILIVYO.NARUDIA NYUMBA HIYO IACHE USIUZE USICHUKULIE MKOPO.

What other option does he have? Desperate times call for desperate measures.

Hakuna mtu anazaliwa ana uzoefu wa kitu fulani. Huwezi kuanza biashara hadi usubiri uwe na uzoefu nayo, uzoefu utaupata mbele kwa mbele.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom