SEASON 5
JF-Expert Member
- Sep 28, 2020
- 481
- 1,015
we hebu toa maswali yako ya ajabu ajabu kama mwl mkuu wa Mchikichini primaryYa masomo gan?

Mkuu ni ngumu sana trust me, kipindi tuko ma young Pineus mshua alipitia situation ya aina hio.Myulize mwenyewe akujibu
Unajua mtu akizoea maisha ya raha basi ikija shida kidogo tu Analia weee
Hapo kwa cheo chake kazini na maisha ukute hata kuendesha uber anaona aibu
Kuhamisha watoto shule za ada ya kawaida anaona aibu
Kuhamia nyumba yake ikiwa haijaisha hawezi
Kula kwa mama ntilie ubwabwa na maharage anaona aibu..
Anakata tamaa ilhali ana gari,nyumba
Wakati kuna msukuma guta kariakoo ana mke Na watoto wanaishi tandale na haijui million moja,gari wala kiwanja but anafight
Mimi nna matatizo zaidi ya huyu kaka mtoa mada but still sikati tamaa
Aisee" Mimi ni member wa Jamiiforums kwa kipindi kirefu kidogo. Nimekuwa nikishirikiana na kushirikishana nanyi mambo mbalimbali ya maisha na pia ya burudani. Nimewaza kwa muda mrefu sana kabla sijaamua kuandika thread hii.
Nlikuwa nmeajiriwa na Kampuni moja ya Mambo ya IT na usafirishaji pia toka mwaka 2015. Nikifanya kazi katika nafasi mbalimbali Kama Operation Manager, Public Relation Manager na pia nikisaidiana na Managers mbalimbali katika majukumu yao niki coordinate Projects mbalimbali za Kampuni.
Mwaka 2017 Kampuni yetu ilianza kuyumba. Tuliyumba sana kutokana na mambo mbalimbali ya Soko (Wateja wetu wakubwa walikuwa ni kutoka Serikalini na Makampuni Makubwa)
Tukawa kama mtu aliyepata ulemavu wa mguu mmoja. Tulijitahidi sana kupambana na kuzoea hali hiyo ya kutumia mguu mmoja. Hali iliendelea kuwa mbaya. Bahati mbaya mpaka kufika katikati ya mwaka 2019 tukawa hatuwezi hata lipana mishahara.
Tukawa tunapeana posho na hatimaye ikafika hatua hata posho ikawa ngumu. Tuliendelea kujitahidi kupambana hadi ikafikia hatukuwa na uwezo wa kulipwa kitu kabisa. Hivyo mwaka huo kuanzia mwezi wa 9 hatukuwa tunapokea anything in terms of money.na hatimaye Kampuni ikatuomba sisi wengine tuandike barua ya ku resign au tufukuzwe kazi. Binafsi nliona hali ilivyokuwa.sababu before that pia CEO alituomba tuwe free kuacha kazi.
Mimi nlikuwa katika watu wachache ambao niliamini tungepambana tukashinda hali ile.nikaomba niendelee. Nikawa natumia pesa yangu na hatimaye akiba yangu yote kwisha. Nikauza gari moja nipate pesa ya nauli na matumizi nyumbani.
Mke wangu hakuwa kazini. Nilimpa pesa Mil 6. Akafanye biashara. Bahati mbaya sana akapoteza hizo pesa zote katka biashara akichangiwa hasa na Haya makampuni ya GNLD na Q-Net. Mtaji ukaisha.
Tukaamua tena kuuza gari nyingine ili watoto waende shule na pia tujitahidi kumalizia ujenzi. Hapo tulipokuwa tunaishi pia ilibidi tulipe kodi. Hatukukamilisha ujenzi.
Nifupishe habari. Toka mwaka jana mwezi wa 9 nmepambana sana kutafuta kazi.lakini sikufanikiwa pesa hizo nlizokuwa nazo ilibidi pia niingize kwenye matibabu kwa sababu ya ugonjwa nliokuwa nao mguu wa kulia una tatizo la maumivu makali kwenye mfupa na kushoto kiasi.
Nimehangaika sana Aga Khan, Hindu Mandal na Moi. Walinipa ushauri wa kupunguza uzito na kutotembea sana (Ugonjwa unaitwa Heel Spurs) so ikabidi pia nibakize gari moja liwe ndo la kutembelea.so nikabaki na gari dogo.
Maisha yalizidi kuwa magumu na hatimaye kodi ikawa ngumu kulipa.ikapita miezi 2 mwenye nyumba akashindwa kutuvumilia. Akaja tukatoa vitu nje. Watoto wangu wawili walikuwa wanasoma Elimu ya Msingi(mmoja hajaanza bado nina watoto watatu) wakarudishwa nyumbani.
Siku tunalazimika kutoa vitu nje it was a very humiliating day. Mimi, mke,dada wa kazi na watoto wetu watatu.Mke akaamua kuita gari lije chukua vyombo kupeleka kwao. Siwezi sahau siku hiyo.Ndo siku ya mwisho kumwona mke wangu mpaka leo hii hatujaonana tena.
Vitu vilipakiwa kwenye gari ikawa inatakiwa kulipia tsh 150,000 mke wangu akataka nitoe pesa, sikuwa nayo. Wife akapiga simu kwa mdogo wake akamtumia. They left mimi nikiwa sielewi nifanye nini.
Nlitoka na gari nikaenda park sehemu nikakaa mpaka usingizi uliponipitia nlikuja shtuka saa 2 usiku sina pa kwenda kulala.mfukoni nina tsh 7000 tu. Nlitumia 1000 kununua mihogo na 6000 nikaweka kama balance. 1000 nilienda lipia wanapolaza magari.nami nikashusha kiti nikalala kwenye gari mpaka asubuhi.
Kwa siku 3 nlikuwa nahangaika sina cha kufanya. Nilipata wazo la kuwasiliana na rafiki yangu wa shule ya msingi. Nlimweleza tatizo langu akanishauri niende kwake ana chumba cha wageni nikaishi naye.
Kiukweli kwa umri wangu wa miaka 30+ nlijisikia vibaya sana.nlienda ishi naye.sikuwa na namna.
Nashukuru kuna marafiki wachache ambao hawakunitupa ktk jambo hili hata kwa kunitia moyo na mwingine kunisaidia hata pesa ya voucher au usafiri.
Katika kipindi hiki nimepoteza sana marafiki. Wengi walikata mawasiliano kabisa.hata napopiga kuwasalimia.(si kuomba pesa) wamekuwa hawapokei simu zangu.
Nmekuwa hata natuma texts kuwasalimia na sometimes kuwaomba wanikumbuke zinapotokea nafasi za ajira. Wameacha kujibu.
Binafsi nilikuwa ni mtu ninayeshirikiana na kila mtu.sikuwahi bagua mtu au mtendea mtu ubaya. Maisha yangu sikuwahi kunywa pombe au kuvuta sigara.
Nimekuwa na majonzi hasa kutengwa na familia yangu. Mke wangu amekuwa si wa mawasiliano ya karibu nami. Ni kama amesusa. Watoto kila napoongea nao wanalia na kutaka turudi kuishi pamoja. Mmoja ameamua kabisa kutoongea nami hata napoomba kumsalimia.Hataki.
Nashindwa kwenda kwa wakwe kuisalimia familia yangu. Lakini nashindwa zaidi kwenda mikono mitupu kuonana na familia yangu. Wakwe zangu hawakuwahi nisemesha lolote hata baada ya kuona mke amerudi kwao. Nimewaelewa pia kwa hilo.
Mke wangu alifanikiwa kupata kazi sehemu. Lakini bado amekuwa akitaka nimtumie pesa za matumizi hata ndogo ndogo ambazo angeweza saidia mwenyewe.nafahamu anafanya hivi kuniumiza zaidi au kuonesha kuwa ni mwanaume irresponsible.
Naumia sababu wazazi wangu ambao nlipaswa niwe nawasaidia wao ndo wanatuma pesa kiasi wapatacho kuisaidia familia yangu. (Wao wanaishi Mwanza) Baba yangu alishastaafu.hana kazi.mama yangu pia anafanya tu ufugaji mdogo mdogo.
Naishi kwa fadhila za wadogo zangu na rafiki yangu huyu ambaye namwonea huruma pia. Nina Elimu ya Degree (naomba nisitaje ya nini/nisitoe details nyingi isipokuwa kwa mtu ambaye tutawasiliana inbox privately ikiwa atakuwa na namna ya kunisaidia)
Leo nimeandika kwa majonzi thread hii baada ya kutumiwa tsh 5000 kwenye simu na msichana ambaye alikuwa housemaid wetu akiwa huko aliko na wife. Yeye ananikumbuka.
Nmeumia kwa alichoandika (baba najua unaumia huko uliko pokea hiyo hata ya vocha mimi nakuombea ufanikiwe) nmejaribu kumrudishia hiyo pesa ametuma zaidi 7000 na kutaka nitumie.
Juzi nlipata simu kwa mtu ambaye nikiwa kazini aliwahi patwa na tatizo la kikazi alipokuwa ameenda kikazi Kampuni flani na kushawishika kuiba kitu flani. Nikiwa PR nlienda shughulikia jambo hilo.bahati mbaya ushahidi ww CCTV Camera ulimwonesha yule bwna mdogo akitenda jambo hilo. Muda huo akiwa amewekwa chini ya ulinzi na gari ya Kampuni imezuiliwa. Nlimsaidia akatolewa na siku mreport kazini zaidi ya kumwonya na kumshauri.
Alionekana kujutia kosa lake sana. Mwaka na nusu umepita juzi kanikumbuka nikiwa sina hata tsh 500. Mfukoni akanitumia tsh 30,000. Nlishamsahau.akanambia tu "Boss nimekuumbuka naomba hiyo uweke mafuta" nlimshukuru sana. Hajui kama sina kazi.
Haya mambo yananiumiza zaidi na kuona nina deni zaidi kwa familia yangu,rafiki zangu na wanaonizunguka.
Ndugu zanguni. Nipo katika msongo wa mawazo. Naona i have failed my family. I have failed my parents and relatives. Nliwaza kumeza dawa nyingi sana kukatisha maisha yangu. Mara kadhaa yananijia hayo mawazo.
Nashindwa nifanye nini. Nahangaika kuomba kazi na kutafuta kazi.tatizo langu la miguu halinipi nafasi ya kufanya kazi ambayo ntasimama sana, au ntatembea sana.
Nmetengwa nimebaki peke yangu.najiona mzigo kwa huyu rafiki yangu na familia yake.naona pia nmekuwa so humiliated.
Naombeni msaada wa kazi. Kazi katika upande wa kusimamia projects,kusimamia hata madereva pia naweza kuwa dereva wa mtu(gari ndogo) gari nayotumia haiwezekani kuwa Uber najua kuna mtu anaweza nishauri hivyo.ilikataliwa kwa namna ilivyo.
Pia nina uzoefu katika kufundisha ngazi za certificates na diploma masomo ya management, customer care, social skills,communication skills, development studies.
Ni mzuri katika kuongea na kuandika pia english and swahili ( do not consider this article it is informal)
Najua watu wengine wata kebehi,watanidharau na kunikashifu.nitayapokea yote. Kwa mtu ambaye atakuwa radhi kujadiliana nami jambo hili in person nipo radhi. Nahitaji kazi niweze saidia wengine pia. Si vyema nikaendelea pokea misaada toka kwa watu wengine. Nahitaji pia kuishi na familia yangu.
Nipo Dar Es Salaam kwa sasa naishi Bunju. Asanteni"
Usithubutu hata kum bipu huyo kibaka mzoefu.Dah, hii habari imefanya ni delete namba za mwanamke ninaemfukuzia.
Amenidharau na kuniita bahili[emoji23][emoji23]
Dah ndomana kwenye swala la kuoa huwa nawaza sana.
Ee Mwenyezi Mungu nisaidie
Huu ndo ushauri wangu uliokuja nikiwa nasoma huu uzi.Pole sana mkuu, makampuni mengi hayafanyi vizuri sokoni na watu wengi wanapunguzwa mimi nikupe moyo, wewe bado ni kijana na una nguvu ma safari ndefu ya kwenda, kwa vyovyote kama kuna uwezekano wa kuuza hilo gari na isikuathiri sana uza, fanya mambo mengine, au kama una aina ya gari ambayo hauwezi kufanyia biashara ya uber, fanya mchakato ubadilishane na ambayo utaweza kufanyia biashara hiyo hata kama ni kwa hasara ila itaku boost, kisha ufanye mchakatk uhame hapo kwa rafiki yako, kabla naye hujampoteza
Hii ni one side story, sidhani kama huyo mwanamke ni mbaya kiasi hicho. Hapo nakataa kabisa.Usisahau hii methali "Tenda wema, uende zako". Siku hizi tuna watu kibao wanaotendewa mema lakini hawana shukrani.
Mke wa huyu bwana ni mbinafsi period. Si rahisi mwanaume mnyanyasaji akupe hela ya mtaji ili ufanye biashara msaidiane maisha. Hadi watoto wanalia baba arudi waishi kama zamani, it means walikuwa wanaishi as a happy family (japo changamoyo hazikosekani). Afu mke alivyo mjinga anahisi anamkomesha mwanaume, kumbe anawaathiri watoto kisaikolojia. Naamini angeweza kabisa kukaa chini na watoto akatafuta perfect excuse ya kwa nini baba yupo mbali (japo wanajua walifukuzwa), na angedumisha mawasiliano ya baba na watoto. Kumuacha peke yake mtu aliyechanganyikiwa hivi, what if akifa, atakuwa amewasaidia nini watoto wake? As long as uwepo wa mume wake, jasho lake na kila kitu chake kilikuwa na direct impact kwake na kwa watoto; basi angeshikamana tu na mumewe katika kipindi hiki.
Acha kabisa mzee, hasa uwe na mke chuchunge na mbinafsi..Unaweza tamani israel apite na roho yako chap uamkie kuzimu.😂Mkuu umeongea point kubwa sana.
Hapo mungu amempa majaribu tu apate kujifunza marafiki wa kweli ni akina nani na wanafki ni akina nani.
Imagine leo hii anapata msaada hadi kwa housegirl inamaanisha ukarimu wake ndio umemsaidia otherwise kama angemnyanyasa asingeupata msaada wake.
Hii hali iliwahi kunikuta aisee usiombe kabisa ikukute yaani utahisi kama dunia imepinduka.
AiseeMkuu ni ngumu sana trust me, kipindi tuko ma young Pineus mshua alipitia situation ya aina hio.
Alikuwa very educated and exposed young man akala u GM Cotton board, kijana mdogo hela za kumwaga akija home kila jioni briefcase imejaa mipunga yani kama movie, gari enzi hizo ni Niva TX maisha yetu yalianzia almost City center Palm beach ndio sehemu ya recreation jioni miaka ya 80's hio. Wote Mshua na bi.mkubwa ni ma Lifeist kinyama young and very generous patners. Nyumba haikauki wageni on weekends ni kuku kwa kwenda mbele.
93" meza zikapinduka mzee akapigwa kadi nyekundu. Ghafla tukahamia Tabata porini sana enzi hizo uzuri alishajenga 2 houses na viwanja kadhaa alikuwa navyo. Alipitia kipindi kigumu sana 4 young kids and wife, bi. mkubwa hakuwa mbinafsi akapambana sana hadi kuja kukaa sawa on early 2000's ndio mshua akaanza mishe mishe upya. Almost puzzled and really fucked up for 7 yrs ndio kuja kuikubali hali. Too bad on 2001 we lost Mom and one bro! Ilikuwa pigo sana.
Maisha ni fumbo kubwa sana hujui ya kesho cha msingi getting prepared tu for the odds. Hii situation ilinifunza kitu.
Kweli kabisa yani, siku hela zimekata hutamuona Juma wala Uledi kmmmke zao. Na shughuli itakuwa ni kukuponda huko walipo na pedeshee mwengine.😂😂😂Pole sana brother. Ukitaka kumjua mke, marafiki ni pale utapokuwa huna kipato. Ndio maana nikiona mtu anaendekeza ulevi na marafiki na offer za ajabu ajabu najua hayajamfika!
Kuna watu walikuwa na marafiki mji mzima ila yalipowafika ndio walijua dunia iko vipi.
Usikate tamaa, hili tukio ndio litakuja kuimarisha ndoa na familia yako. Endelea kupambana ukiomba Mungu
Ndio msimu wao huu, xmas ndio hio ishaingia yani. 😂😂😂 Wale wahongaji mjiandae. Mi namuhonga mke wangu tu.[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Eti prettylicious.
Halafu huu ndio mwezi wao wa "baby nikwambie kitu" ungejuta sana mkuu
Maisha hayo mzeeAisee
mkuu pole sana, ndio ukubwa huo[emoji52]Mkuu ni ngumu sana trust me, kipindi tuko ma young Pineus mshua alipitia situation ya aina hio.
Alikuwa very educated and exposed young man akala u GM Cotton board, kijana mdogo hela za kumwaga akija home kila jioni briefcase imejaa mipunga yani kama movie, gari enzi hizo ni Niva TX maisha yetu yalianzia almost City center Palm beach ndio sehemu ya recreation jioni miaka ya 80's hio. Wote Mshua na bi.mkubwa ni ma Lifeist kinyama young and very generous patners. Nyumba haikauki wageni on weekends ni kuku kwa kwenda mbele.
93" meza zikapinduka mzee akapigwa kadi nyekundu. Ghafla tukahamia Tabata porini sana enzi hizo uzuri alishajenga 2 houses na viwanja kadhaa alikuwa navyo. Alipitia kipindi kigumu sana 4 young kids and wife, bi. mkubwa hakuwa mbinafsi akapambana sana hadi kuja kukaa sawa on early 2000's ndio mshua akaanza mishe mishe upya. Almost puzzled and really fucked up for 7 yrs ndio kuja kuikubali hali. Too bad on 2001 we lost Mom and one bro! Ilikuwa pigo sana.
Maisha ni fumbo kubwa sana hujui ya kesho cha msingi getting prepared tu for the odds. Hii situation ilinifunza kitu.
ExactlyHuu ndo ushauri wangu uliokuja nikiwa nasoma huu uzi.
Pale kampuni yake ilivyokuwa inasuasua 2017, angeacha kazi akakomaa na uber.
Sahivi angeshapiga hatua kubwa sana tu.
Tena alikuwa na gari 3, zote angezigeuza uber sahivi asingeteseka kwa kiwango hiki.
Kwenye maisha inabidi uwe flexible sana. Usisubiri ikawa "too late".
Sahivi namshukuru mungu tumekuwa sasa. Tunajitegemea mzee yupo freshi! Mungu ni mwema.mkuu pole sana, ndio ukubwa huo[emoji52]
Maumivu unayopitia yasikutoe kwenye reli ndugu.Wengi wamejikwaa pindi wanapopitia magumu maishani mwao.Wengine hufikia hatua ya kuzikabidhi nafsi zao kwa yule mwovu na kuamua kujitenga kabisa na neema ya Mungu muumba wao.Jifunze kuwa positive kwenye kila hali maishani.Usiishie kuyasikiliza maumivu tu,ukaacha kutambua thamani kubwa iliyobebwa na maumivu hayo.Kipindi unachopitia kina faida kubwa maishani mwako kuliko unachoona kuwa ni hasara. Faida mojawapo iliyo wazi kabisa ni kwamba umeweza kuwajua watu wako wa karibu kwa uhalisia wao. Binadamu wengi ni waigizaji. Wengi huficha uhalisia wa nia zao ili wapate wayatakayo kwa ajili yao wenyewe. Imagine umekuwa ukiishi na umezaa na mke ambaye haoni shida kukufanyia hayo anayokufanyia sasa. Na si ajabu alikuwa anakutamkia maneno matamu matamu pindi ukiwa "mambo safi". Pili,umejifunza maana halisi ya Upendo na Thamani yake katika maisha.Kupitia hilo umejua kwamba miongoni mwa hitaji muhimu kabisa kwa binadamu ni kupendwa. Umeweza kuwatambua wakupendao kwa dhati na wale wakupendao kwa hati.Nakusihi sana kwamba hali hii ikuweke karibu zaidi na Mungu especially kama kabla ulikuwa unamchukulia poa(Hii ni faida kubwa kwako tena ya milele,itakufaa ukiwa hai na hata baada ya kufa.Mahusiano yako binafsi na Mungu ni muhimu zaidi kuliko chochote na wakati mwingine Mungu huruhusu haya yatokee ili kukurudisha mikononi mwake). Umeshindwa kutambua kwamba moto huu unaoupitia sasa si kwa ajili ya kukuangamiza bali kukung'arisha zaidi na kukuandaa kwa future iliyo bora zaidi ndio maana ukafikiria hata kujiua ingawa Mungu kaingilia kati ili kukupa fursa ujifunze kusudi lake jema maishani mwako. Unachopaswa kujifunza ni kwamba katika maisha wakati mwingine mbegu ya kale haina budi kufa ili kuipa nafasi mbegu mpya kumea. Jifunze kuishi kwa kumtumaini Kristo Yesu katika maisha yako ili uwe na uhakika na maisha yako ya sasa na yajayo pia. Mungu angeweza kuzuia haya yasikupate kabisa lakini jiulize kwa nini kayaruhusu?. Ukipata jibu sahihi na kamili la swali hili amini nakuambia huzuni yako itageuka furaha ambayo hata kabla hujapatwa na taabu hizo hujawahi kuipata.Inua macho juu." Mimi ni member wa Jamiiforums kwa kipindi kirefu kidogo. Nimekuwa nikishirikiana na kushirikishana nanyi mambo mbalimbali ya maisha na pia ya burudani. Nimewaza kwa muda mrefu sana kabla sijaamua kuandika thread hii.
Nlikuwa nmeajiriwa na Kampuni moja ya Mambo ya IT na usafirishaji pia toka mwaka 2015. Nikifanya kazi katika nafasi mbalimbali Kama Operation Manager, Public Relation Manager na pia nikisaidiana na Managers mbalimbali katika majukumu yao niki coordinate Projects mbalimbali za Kampuni.
Mwaka 2017 Kampuni yetu ilianza kuyumba. Tuliyumba sana kutokana na mambo mbalimbali ya Soko (Wateja wetu wakubwa walikuwa ni kutoka Serikalini na Makampuni Makubwa)
Tukawa kama mtu aliyepata ulemavu wa mguu mmoja. Tulijitahidi sana kupambana na kuzoea hali hiyo ya kutumia mguu mmoja. Hali iliendelea kuwa mbaya. Bahati mbaya mpaka kufika katikati ya mwaka 2019 tukawa hatuwezi hata lipana mishahara.
Tukawa tunapeana posho na hatimaye ikafika hatua hata posho ikawa ngumu. Tuliendelea kujitahidi kupambana hadi ikafikia hatukuwa na uwezo wa kulipwa kitu kabisa. Hivyo mwaka huo kuanzia mwezi wa 9 hatukuwa tunapokea anything in terms of money.na hatimaye Kampuni ikatuomba sisi wengine tuandike barua ya ku resign au tufukuzwe kazi. Binafsi nliona hali ilivyokuwa.sababu before that pia CEO alituomba tuwe free kuacha kazi.
Mimi nlikuwa katika watu wachache ambao niliamini tungepambana tukashinda hali ile.nikaomba niendelee. Nikawa natumia pesa yangu na hatimaye akiba yangu yote kwisha. Nikauza gari moja nipate pesa ya nauli na matumizi nyumbani.
Mke wangu hakuwa kazini. Nilimpa pesa Mil 6. Akafanye biashara. Bahati mbaya sana akapoteza hizo pesa zote katka biashara akichangiwa hasa na Haya makampuni ya GNLD na Q-Net. Mtaji ukaisha.
Tukaamua tena kuuza gari nyingine ili watoto waende shule na pia tujitahidi kumalizia ujenzi. Hapo tulipokuwa tunaishi pia ilibidi tulipe kodi. Hatukukamilisha ujenzi.
Nifupishe habari. Toka mwaka jana mwezi wa 9 nmepambana sana kutafuta kazi.lakini sikufanikiwa pesa hizo nlizokuwa nazo ilibidi pia niingize kwenye matibabu kwa sababu ya ugonjwa nliokuwa nao mguu wa kulia una tatizo la maumivu makali kwenye mfupa na kushoto kiasi.
Nimehangaika sana Aga Khan, Hindu Mandal na Moi. Walinipa ushauri wa kupunguza uzito na kutotembea sana (Ugonjwa unaitwa Heel Spurs) so ikabidi pia nibakize gari moja liwe ndo la kutembelea.so nikabaki na gari dogo.
Maisha yalizidi kuwa magumu na hatimaye kodi ikawa ngumu kulipa.ikapita miezi 2 mwenye nyumba akashindwa kutuvumilia. Akaja tukatoa vitu nje. Watoto wangu wawili walikuwa wanasoma Elimu ya Msingi(mmoja hajaanza bado nina watoto watatu) wakarudishwa nyumbani.
Siku tunalazimika kutoa vitu nje it was a very humiliating day. Mimi, mke,dada wa kazi na watoto wetu watatu.Mke akaamua kuita gari lije chukua vyombo kupeleka kwao. Siwezi sahau siku hiyo.Ndo siku ya mwisho kumwona mke wangu mpaka leo hii hatujaonana tena.
Vitu vilipakiwa kwenye gari ikawa inatakiwa kulipia tsh 150,000 mke wangu akataka nitoe pesa, sikuwa nayo. Wife akapiga simu kwa mdogo wake akamtumia. They left mimi nikiwa sielewi nifanye nini.
Nlitoka na gari nikaenda park sehemu nikakaa mpaka usingizi uliponipitia nlikuja shtuka saa 2 usiku sina pa kwenda kulala.mfukoni nina tsh 7000 tu. Nlitumia 1000 kununua mihogo na 6000 nikaweka kama balance. 1000 nilienda lipia wanapolaza magari.nami nikashusha kiti nikalala kwenye gari mpaka asubuhi.
Kwa siku 3 nlikuwa nahangaika sina cha kufanya. Nilipata wazo la kuwasiliana na rafiki yangu wa shule ya msingi. Nlimweleza tatizo langu akanishauri niende kwake ana chumba cha wageni nikaishi naye.
Kiukweli kwa umri wangu wa miaka 30+ nlijisikia vibaya sana.nlienda ishi naye.sikuwa na namna.
Nashukuru kuna marafiki wachache ambao hawakunitupa ktk jambo hili hata kwa kunitia moyo na mwingine kunisaidia hata pesa ya voucher au usafiri.
Katika kipindi hiki nimepoteza sana marafiki. Wengi walikata mawasiliano kabisa.hata napopiga kuwasalimia.(si kuomba pesa) wamekuwa hawapokei simu zangu.
Nmekuwa hata natuma texts kuwasalimia na sometimes kuwaomba wanikumbuke zinapotokea nafasi za ajira. Wameacha kujibu.
Binafsi nilikuwa ni mtu ninayeshirikiana na kila mtu.sikuwahi bagua mtu au mtendea mtu ubaya. Maisha yangu sikuwahi kunywa pombe au kuvuta sigara.
Nimekuwa na majonzi hasa kutengwa na familia yangu. Mke wangu amekuwa si wa mawasiliano ya karibu nami. Ni kama amesusa. Watoto kila napoongea nao wanalia na kutaka turudi kuishi pamoja. Mmoja ameamua kabisa kutoongea nami hata napoomba kumsalimia.Hataki.
Nashindwa kwenda kwa wakwe kuisalimia familia yangu. Lakini nashindwa zaidi kwenda mikono mitupu kuonana na familia yangu. Wakwe zangu hawakuwahi nisemesha lolote hata baada ya kuona mke amerudi kwao. Nimewaelewa pia kwa hilo.
Mke wangu alifanikiwa kupata kazi sehemu. Lakini bado amekuwa akitaka nimtumie pesa za matumizi hata ndogo ndogo ambazo angeweza saidia mwenyewe.nafahamu anafanya hivi kuniumiza zaidi au kuonesha kuwa ni mwanaume irresponsible.
Naumia sababu wazazi wangu ambao nlipaswa niwe nawasaidia wao ndo wanatuma pesa kiasi wapatacho kuisaidia familia yangu. (Wao wanaishi Mwanza) Baba yangu alishastaafu.hana kazi.mama yangu pia anafanya tu ufugaji mdogo mdogo.
Naishi kwa fadhila za wadogo zangu na rafiki yangu huyu ambaye namwonea huruma pia. Nina Elimu ya Degree (naomba nisitaje ya nini/nisitoe details nyingi isipokuwa kwa mtu ambaye tutawasiliana inbox privately ikiwa atakuwa na namna ya kunisaidia)
Leo nimeandika kwa majonzi thread hii baada ya kutumiwa tsh 5000 kwenye simu na msichana ambaye alikuwa housemaid wetu akiwa huko aliko na wife. Yeye ananikumbuka.
Nmeumia kwa alichoandika (baba najua unaumia huko uliko pokea hiyo hata ya vocha mimi nakuombea ufanikiwe) nmejaribu kumrudishia hiyo pesa ametuma zaidi 7000 na kutaka nitumie.
Juzi nlipata simu kwa mtu ambaye nikiwa kazini aliwahi patwa na tatizo la kikazi alipokuwa ameenda kikazi Kampuni flani na kushawishika kuiba kitu flani. Nikiwa PR nlienda shughulikia jambo hilo.bahati mbaya ushahidi ww CCTV Camera ulimwonesha yule bwna mdogo akitenda jambo hilo. Muda huo akiwa amewekwa chini ya ulinzi na gari ya Kampuni imezuiliwa. Nlimsaidia akatolewa na siku mreport kazini zaidi ya kumwonya na kumshauri.
Alionekana kujutia kosa lake sana. Mwaka na nusu umepita juzi kanikumbuka nikiwa sina hata tsh 500. Mfukoni akanitumia tsh 30,000. Nlishamsahau.akanambia tu "Boss nimekuumbuka naomba hiyo uweke mafuta" nlimshukuru sana. Hajui kama sina kazi.
Haya mambo yananiumiza zaidi na kuona nina deni zaidi kwa familia yangu,rafiki zangu na wanaonizunguka.
Ndugu zanguni. Nipo katika msongo wa mawazo. Naona i have failed my family. I have failed my parents and relatives. Nliwaza kumeza dawa nyingi sana kukatisha maisha yangu. Mara kadhaa yananijia hayo mawazo.
Nashindwa nifanye nini. Nahangaika kuomba kazi na kutafuta kazi.tatizo langu la miguu halinipi nafasi ya kufanya kazi ambayo ntasimama sana, au ntatembea sana.
Nmetengwa nimebaki peke yangu.najiona mzigo kwa huyu rafiki yangu na familia yake.naona pia nmekuwa so humiliated.
Naombeni msaada wa kazi. Kazi katika upande wa kusimamia projects,kusimamia hata madereva pia naweza kuwa dereva wa mtu(gari ndogo) gari nayotumia haiwezekani kuwa Uber najua kuna mtu anaweza nishauri hivyo.ilikataliwa kwa namna ilivyo.
Pia nina uzoefu katika kufundisha ngazi za certificates na diploma masomo ya management, customer care, social skills,communication skills, development studies.
Ni mzuri katika kuongea na kuandika pia english and swahili ( do not consider this article it is informal)
Najua watu wengine wata kebehi,watanidharau na kunikashifu.nitayapokea yote. Kwa mtu ambaye atakuwa radhi kujadiliana nami jambo hili in person nipo radhi. Nahitaji kazi niweze saidia wengine pia. Si vyema nikaendelea pokea misaada toka kwa watu wengine. Nahitaji pia kuishi na familia yangu.
Nipo Dar Es Salaam kwa sasa naishi Bunju. Asanteni"
Pole sana mzee maisha kukutana changamoto na misukosuko ni moja ya mitihani ktk maishaNashukuru sana ndugu yangu.
Hawa qnet sjui gnld wamewatia sana umaskini watu anyway watu wenyewe ni wagumu kuelewaPole.
Tunapowekeza mahali pamoja pakaticki tusijisahau kuwekeza na pengine tofauti tofauti.maana kimoja kinaweza anguka,kingine kikabaki na kukushika
Mkeo ni mjinga na hana busara,million sita ni pesa nyingi sana kuwekeza ya kaenda katafuta mteremko QNet kaliwa ni mjinga!.kapata kazi bado anakuumiza ilhali anajua kazi huna na unaumwa hana busara!
Kwanini usiuze vitu ulivyonayo baadhi vyenye thamani vikusongeshe kuliko vikikaa tu vinachakaa ukweni?
Ulisema mna nyumba mnamalizia kujenga kwanini usiuze angalau utapata hata million 20-40 uanze upya?
Ama uza hili gari kisha hamia nyumba mnayojenga ikiwa hata pagala juu bati madirisha ya nyavu muanze maisha huku unaendelea kutafuta kazi?
Ni ushauri tu maana huwezi jua Hiki kilio kitachukua mda gani..so ujiongsze kwanza.