Nahisi kama nimefikia hatua ya Kukata Tamaa kiwango cha Mwisho. Naomba msaada wenu Ndugu zanguni

Nahisi kama nimefikia hatua ya Kukata Tamaa kiwango cha Mwisho. Naomba msaada wenu Ndugu zanguni

Status
Not open for further replies.
Na hiki huwa ndio kigezo changu no.1 ninapotaka msaidia yeyote anaetokea Ndani ya JF.
Sasa ID halisi sindio mwanzo wa kufukua makaburi humu maana kuna watu wapo kwa kazi hio.

Utafikiri hukuwahi ishi maisha mengine labda. Shida haina adabu aisee! Unaeza post una majanga, watu wakavuta thread za nyuma ili kupata cha kukusimangia..."oh jamaa si aliwahi kuomba chenchi za paundi huyu" ..."mara jamaa si anamiliki gari huyu auze lile gari"
 
JPM ulaaniwe kabisa kwa kufanya makampuni binafsi yasipate kazi kutoka serikalini.
Pole sana wa Ng'wise .Njoo PM uniachie number zako nitakutafuta.
Imeniuma sana na degree yako unapewa pesa na house girl aliyemaliza la saba tu.
Sema nikasema mguu pia imesababisha. Otherwise ningekuambia katafute hata kazi ya ulinzi. Degree weka pembeni.
Ila pia wewe na mkeo sijui mkoje. Mkanunua magari matatu hata nyumba yenu hamjamaliza [emoji849].Any way katika maisha priorities inatakiwa iwe need. Yaani bila gari nitaishi,ila bila nyumba itabidi nikabebwe.
Pole sana na kila lenye kheri.
Ushaingiza siasa duuh
 
Mwanamke wa hovyo kabisa. Mkuu nakuombea pia ubinafsi ni roho ya kishetani. Nakuombea sana usije pata mwanamke wa aina hio abadani. Ni bora ufuge mbuzi tu sio kuwa na mwanamke mchoyo na asiye na akili. Usije kuwa miongoni mwa watu waliopata hasara maishani.
Ha ha ha Hi... Mambo?
Za masiku? Leo umeamua nigeuza mwanaume mkuu? [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji119][emoji119]


Katika maisha yangu, Mungu anipe... nyumba yangu iwe kimbilio jamani. Nisitenge ndugu, jamaa na marafiki. Najua malipo yake kama si hapa duniani basi hata mbinguni. Na hata pia kwa uzao wangu.
 
Ha ha ha Hi... Mambo?
Za masiku? Leo umeamua nigeuza mwanaume mkuu? [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji119][emoji119]


Katika maisha yangu, Mungu anipe... nyumba yangu iwe kimbilio jamani. Nisitenge ndugu, jamaa na marafiki. Najua malipo yake kama si hapa duniani basi hata mbinguni. Na hata pia kwa uzao wangu.
Wewee 😍😍😍 niko poa best, basi nilisoma bila hata kuangalia title ya member ujue 😂😂😂 nikahisi baharia mwenzangu.
 
" Mimi ni member wa Jamiiforums kwa kipindi kirefu kidogo. Nimekuwa nikishirikiana na kushirikishana nanyi mambo mbalimbali ya maisha na pia ya burudani. Nimewaza kwa muda mrefu sana kabla sijaamua kuandika thread hii.

Nlikuwa nmeajiriwa na Kampuni moja ya Mambo ya IT na usafirishaji pia toka mwaka 2015. Nikifanya kazi katika nafasi mbalimbali Kama Operation Manager, Public Relation Manager na pia nikisaidiana na Managers mbalimbali katika majukumu yao niki coordinate Projects mbalimbali za Kampuni.

Mwaka 2017 Kampuni yetu ilianza kuyumba. Tuliyumba sana kutokana na mambo mbalimbali ya Soko (Wateja wetu wakubwa walikuwa ni kutoka Serikalini na Makampuni Makubwa)

Tukawa kama mtu aliyepata ulemavu wa mguu mmoja. Tulijitahidi sana kupambana na kuzoea hali hiyo ya kutumia mguu mmoja. Hali iliendelea kuwa mbaya. Bahati mbaya mpaka kufika katikati ya mwaka 2019 tukawa hatuwezi hata lipana mishahara.

Tukawa tunapeana posho na hatimaye ikafika hatua hata posho ikawa ngumu. Tuliendelea kujitahidi kupambana hadi ikafikia hatukuwa na uwezo wa kulipwa kitu kabisa. Hivyo mwaka huo kuanzia mwezi wa 9 hatukuwa tunapokea anything in terms of money.na hatimaye Kampuni ikatuomba sisi wengine tuandike barua ya ku resign au tufukuzwe kazi. Binafsi nliona hali ilivyokuwa.sababu before that pia CEO alituomba tuwe free kuacha kazi.

Mimi nlikuwa katika watu wachache ambao niliamini tungepambana tukashinda hali ile.nikaomba niendelee. Nikawa natumia pesa yangu na hatimaye akiba yangu yote kwisha. Nikauza gari moja nipate pesa ya nauli na matumizi nyumbani.

Mke wangu hakuwa kazini. Nilimpa pesa Mil 6. Akafanye biashara. Bahati mbaya sana akapoteza hizo pesa zote katka biashara akichangiwa hasa na Haya makampuni ya GNLD na Q-Net. Mtaji ukaisha.

Tukaamua tena kuuza gari nyingine ili watoto waende shule na pia tujitahidi kumalizia ujenzi. Hapo tulipokuwa tunaishi pia ilibidi tulipe kodi. Hatukukamilisha ujenzi.

Nifupishe habari. Toka mwaka jana mwezi wa 9 nmepambana sana kutafuta kazi.lakini sikufanikiwa pesa hizo nlizokuwa nazo ilibidi pia niingize kwenye matibabu kwa sababu ya ugonjwa nliokuwa nao mguu wa kulia una tatizo la maumivu makali kwenye mfupa na kushoto kiasi.

Nimehangaika sana Aga Khan, Hindu Mandal na Moi. Walinipa ushauri wa kupunguza uzito na kutotembea sana (Ugonjwa unaitwa Heel Spurs) so ikabidi pia nibakize gari moja liwe ndo la kutembelea.so nikabaki na gari dogo.

Maisha yalizidi kuwa magumu na hatimaye kodi ikawa ngumu kulipa.ikapita miezi 2 mwenye nyumba akashindwa kutuvumilia. Akaja tukatoa vitu nje. Watoto wangu wawili walikuwa wanasoma Elimu ya Msingi(mmoja hajaanza bado nina watoto watatu) wakarudishwa nyumbani.

Siku tunalazimika kutoa vitu nje it was a very humiliating day. Mimi, mke,dada wa kazi na watoto wetu watatu.Mke akaamua kuita gari lije chukua vyombo kupeleka kwao. Siwezi sahau siku hiyo.Ndo siku ya mwisho kumwona mke wangu mpaka leo hii hatujaonana tena.

Vitu vilipakiwa kwenye gari ikawa inatakiwa kulipia tsh 150,000 mke wangu akataka nitoe pesa, sikuwa nayo. Wife akapiga simu kwa mdogo wake akamtumia. They left mimi nikiwa sielewi nifanye nini.

Nlitoka na gari nikaenda park sehemu nikakaa mpaka usingizi uliponipitia nlikuja shtuka saa 2 usiku sina pa kwenda kulala.mfukoni nina tsh 7000 tu. Nlitumia 1000 kununua mihogo na 6000 nikaweka kama balance. 1000 nilienda lipia wanapolaza magari.nami nikashusha kiti nikalala kwenye gari mpaka asubuhi.

Kwa siku 3 nlikuwa nahangaika sina cha kufanya. Nilipata wazo la kuwasiliana na rafiki yangu wa shule ya msingi. Nlimweleza tatizo langu akanishauri niende kwake ana chumba cha wageni nikaishi naye.

Kiukweli kwa umri wangu wa miaka 30+ nlijisikia vibaya sana.nlienda ishi naye.sikuwa na namna.

Nashukuru kuna marafiki wachache ambao hawakunitupa ktk jambo hili hata kwa kunitia moyo na mwingine kunisaidia hata pesa ya voucher au usafiri.

Katika kipindi hiki nimepoteza sana marafiki. Wengi walikata mawasiliano kabisa.hata napopiga kuwasalimia.(si kuomba pesa) wamekuwa hawapokei simu zangu.

Nmekuwa hata natuma texts kuwasalimia na sometimes kuwaomba wanikumbuke zinapotokea nafasi za ajira. Wameacha kujibu.

Binafsi nilikuwa ni mtu ninayeshirikiana na kila mtu.sikuwahi bagua mtu au mtendea mtu ubaya. Maisha yangu sikuwahi kunywa pombe au kuvuta sigara.

Nimekuwa na majonzi hasa kutengwa na familia yangu. Mke wangu amekuwa si wa mawasiliano ya karibu nami. Ni kama amesusa. Watoto kila napoongea nao wanalia na kutaka turudi kuishi pamoja. Mmoja ameamua kabisa kutoongea nami hata napoomba kumsalimia.Hataki.

Nashindwa kwenda kwa wakwe kuisalimia familia yangu. Lakini nashindwa zaidi kwenda mikono mitupu kuonana na familia yangu. Wakwe zangu hawakuwahi nisemesha lolote hata baada ya kuona mke amerudi kwao. Nimewaelewa pia kwa hilo.

Mke wangu alifanikiwa kupata kazi sehemu. Lakini bado amekuwa akitaka nimtumie pesa za matumizi hata ndogo ndogo ambazo angeweza saidia mwenyewe.nafahamu anafanya hivi kuniumiza zaidi au kuonesha kuwa ni mwanaume irresponsible.

Naumia sababu wazazi wangu ambao nlipaswa niwe nawasaidia wao ndo wanatuma pesa kiasi wapatacho kuisaidia familia yangu. (Wao wanaishi Mwanza) Baba yangu alishastaafu.hana kazi.mama yangu pia anafanya tu ufugaji mdogo mdogo.

Naishi kwa fadhila za wadogo zangu na rafiki yangu huyu ambaye namwonea huruma pia. Nina Elimu ya Degree (naomba nisitaje ya nini/nisitoe details nyingi isipokuwa kwa mtu ambaye tutawasiliana inbox privately ikiwa atakuwa na namna ya kunisaidia)

Leo nimeandika kwa majonzi thread hii baada ya kutumiwa tsh 5000 kwenye simu na msichana ambaye alikuwa housemaid wetu akiwa huko aliko na wife. Yeye ananikumbuka.

Nmeumia kwa alichoandika (baba najua unaumia huko uliko pokea hiyo hata ya vocha mimi nakuombea ufanikiwe) nmejaribu kumrudishia hiyo pesa ametuma zaidi 7000 na kutaka nitumie.

Juzi nlipata simu kwa mtu ambaye nikiwa kazini aliwahi patwa na tatizo la kikazi alipokuwa ameenda kikazi Kampuni flani na kushawishika kuiba kitu flani. Nikiwa PR nlienda shughulikia jambo hilo.bahati mbaya ushahidi ww CCTV Camera ulimwonesha yule bwna mdogo akitenda jambo hilo. Muda huo akiwa amewekwa chini ya ulinzi na gari ya Kampuni imezuiliwa. Nlimsaidia akatolewa na siku mreport kazini zaidi ya kumwonya na kumshauri.

Alionekana kujutia kosa lake sana. Mwaka na nusu umepita juzi kanikumbuka nikiwa sina hata tsh 500. Mfukoni akanitumia tsh 30,000. Nlishamsahau.akanambia tu "Boss nimekuumbuka naomba hiyo uweke mafuta" nlimshukuru sana. Hajui kama sina kazi.

Haya mambo yananiumiza zaidi na kuona nina deni zaidi kwa familia yangu,rafiki zangu na wanaonizunguka.

Ndugu zanguni. Nipo katika msongo wa mawazo. Naona i have failed my family. I have failed my parents and relatives. Nliwaza kumeza dawa nyingi sana kukatisha maisha yangu. Mara kadhaa yananijia hayo mawazo.

Nashindwa nifanye nini. Nahangaika kuomba kazi na kutafuta kazi.tatizo langu la miguu halinipi nafasi ya kufanya kazi ambayo ntasimama sana, au ntatembea sana.

Nmetengwa nimebaki peke yangu.najiona mzigo kwa huyu rafiki yangu na familia yake.naona pia nmekuwa so humiliated.

Naombeni msaada wa kazi. Kazi katika upande wa kusimamia projects,kusimamia hata madereva pia naweza kuwa dereva wa mtu(gari ndogo) gari nayotumia haiwezekani kuwa Uber najua kuna mtu anaweza nishauri hivyo.ilikataliwa kwa namna ilivyo.

Pia nina uzoefu katika kufundisha ngazi za certificates na diploma masomo ya management, customer care, social skills,communication skills, development studies.

Ni mzuri katika kuongea na kuandika pia english and swahili ( do not consider this article it is informal)

Najua watu wengine wata kebehi,watanidharau na kunikashifu.nitayapokea yote. Kwa mtu ambaye atakuwa radhi kujadiliana nami jambo hili in person nipo radhi. Nahitaji kazi niweze saidia wengine pia. Si vyema nikaendelea pokea misaada toka kwa watu wengine. Nahitaji pia kuishi na familia yangu.

Nipo Dar Es Salaam kwa sasa naishi Bunju. Asanteni"
Sodoku,umewahi kukutana na mtu ambaye yupo kwenye dhiki kuu lakini yeye ndiye anayewatia moyo watu wanaomuonea huruma?.Unadhani nguvu hiyo anaitoa wapi au inatokana na nini?(Ni lazima kuwa mtu wa rohoni ili kuweza kuudhibiti mwili,hii ndio kanuni yake). Mfano mzuri ni pale Yesu alipowajibu wale akina mama waliokuwa wakimuonea huruma na kumlilia aliposema "Msinililie mimi bali jililie ninyi na watoto wenu". Kilichompa nguvu ya kuwaambia haya ni kwa sababu aliuona mwisho wake mwema ambao hao wakina mama walikuwa hawauoni kwa wakati huo.Wakati wao wanaishia kuyaona mateso yake,yeye(Yesu) alikuwa akiona kufufuka kwake,kupaa kwake,kutukuzwa kwake na kupewa jina kuu lipitalo majina yote.Inua macho juu rafiki.Macho juu.

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
 
Ha ha ha Hi... Mambo?
Za masiku? Leo umeamua nigeuza mwanaume mkuu? [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji119][emoji119]


Katika maisha yangu, Mungu anipe... nyumba yangu iwe kimbilio jamani. Nisitenge ndugu, jamaa na marafiki. Najua malipo yake kama si hapa duniani basi hata mbinguni. Na hata pia kwa uzao wangu.
Usijali mungu atakujaalia nyumba tu...Make sure usijisahau tu maana wengi hujisahau kwamba nafasi walizojaaliwa ni kama upendeleo mbele za mungu. About a million women on this world wish to have atleast a man who cares about their existance...ila wapo wanawake ambao wana abuse wanaume bila aibu.😊 and making their families so miserable.
 
kaka usijali sana kuhusu elimu yako, unalalamika sana kiasi kwamba kuna mda huenda huwa unakosa hata hela ya kula, lakini mbona una gari? umeuza magari mengi na umebaki nalo hilo kwann usiliuze ukapata japo mtaji wa kufany japo biashara ndogondogo ukawa haukosi japo hela ya kula na kulipia chumba kimoja?
 
Pole sana! Wasaa utafika utarudia hali ya kawaida dhoruba isikufanye uamini mashua yako lazima izame!
 
Nimesoma na naendelea kusoma comments zenu. Hainipi shida majina mbalimbali ambayo wengine wameamua kuniita. I expected yote haya. I will keep on focusing. Kuna ambao wamekuja PM tubadilishane namba za simu.

Nawashukuru. Kidogo nakuwa makini kutosambaza sana namba yangu. Kwa mtu mwenye nia ya kusaidiana nami ataonekana tu. Lengo halikuwa kuomba michango msije nielewa vibaya. Yet najua wengine kwa nia njema wamenioffer msaada huo.

Nawaomba tu kabla hatujafikia hatua ya mbali zaidi ntapenda tufahamiane pia kama mtu hatojali. Siwezi jisikia amani kupokea anything kwa mtu ambaye hanifahami simfahamu. (Hapa naomba mnielewe)

Nimejifunza mengi ktk uzi huu pia. Wapo walionifariji na wapo ambao wameandika kile kilichojaa mioyoni mwao. Jambo lingine. Nsingependa sana kum victimize mke wangu. Tuna watoto 3. Atabaki kuendelea kuwa mke wangu. Naamini kuna siku atajifunza kitu. Je nliwahi mnyanyasa hapo nyuma? Si aina ya watu wa namna hiyo.

Ndo maana bado sipendelei watu wamshambulie. Nimeandika ili muone situation ninayo pita.pengine mjifunze pia. Kuna ambao wamesoma na bado hawakuelewa uzi huu. I am sorry for them.

There are good people wametuma namba zao tuwasiliane. Nimekubali kuwasiliana nao kwa kuwa najua pia natengeneza network na MARAFIKI WA WAKATI WA SHIDA. nahitaji zaidi watu ambao watakuwa radhi kujenga urafiki/undugu nami hasa kipindi hiki.

Its possible nlikosea hapo before.but nimegundua sipaswi ishi katika makosa hayo. Unaweza nihukumu upendavyo utakuwa sahihi. Nitajifunza zaidi kupenda na kumheshimu kila mtu. Hata ambaye atanichukia,atanidharau na kunikebehi.

Nimeona Kuna watu wema wamo humu na wale wengine pia wamo. Wote tupo humu humu. Nawashukuru. Ntaendelea kuwasiliana nanyi na kujifunza. Tuombeane zaidi.
Okay! Usipaniki kila meseji humu inafunzo kwako na kwa wengine iwe mbaya iwe nzuri inafunzo.Mi ningependa kujua umechagua nini katika michango ya watu pengine unaweza fungua milango zaidi.Jambo la pili kuna mdau kashauri uende kwa wakwe walau ukawasalimie usijitenge kwa kuwa huna kitu pengine ni hisia tu kuwa watakuonaje wale ni wazazi na wameona jua kabla yako nashauri uende no matter what,why,how! Nenda.
 
Baada ya hii tabu unayopitia kuna mpenyo wa ajabu, utakuwa na maisha mazuri kuliko mwanzo. Mungu ni mwema sana
 
Wewee [emoji7][emoji7][emoji7] niko poa best, basi nilisoma bila hata kuangalia title ya member ujue [emoji23][emoji23][emoji23] nikahisi baharia mwenzangu.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji119][emoji119]kunywaaa maji mkuu. Khaa. Hope all is well
 
Usijali mungu atakujaalia nyumba tu...Make sure usijisahau tu maana wengi hujisahau kwamba nafasi walizojaaliwa ni kama upendeleo mbele za mungu. About a million women on this world wish to have atleast a man who cares about their existance...ila wapo wanawake ambao wana abuse wanaume bila aibu.[emoji4] and making their families so miserable.
Yaan jaman me sielewagi kbs. Sijui huwa tunataka nini. Sijawahi kijua asilan abadani
 
Hapo ulipata MUKE, pole sana mkuu. Ukikosea kuoa na matokeo yake ndio kama hivi, mke kaunguza 6mil na kakukimbia. Laiti kama mngetuliza vichwa vyenu kwa assets za hayo magari mawili mngetoboa mkuu. 6mil + assets zingine mnefanya biashara katika kipindi hicho cha mpito maisha yaende.

Again, pole sana mkuu. Utavuka tu kipindi hiki wala usiwaze kujiua, you have kids who need you, usiwaache hao watoto, wapambanie.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom