Nahisi kama nimefikia hatua ya Kukata Tamaa kiwango cha Mwisho. Naomba msaada wenu Ndugu zanguni

Nahisi kama nimefikia hatua ya Kukata Tamaa kiwango cha Mwisho. Naomba msaada wenu Ndugu zanguni

Status
Not open for further replies.
Mbegu ilipandwa Beijing na imemea kweli kweli. Tunaona matunda yake. Dada zetu wametekwa na dunia. Zile morals za til death part us hawana mpango nazo. Mpango ni "wanawake na maendeleo". Wasomi wengi ndio wahanga.
Hahahah yani hii mbegu itatesa sana raia aisee. Im very keen with women aisee. Wanawake wanataka wao wapewe tu kmmmke. Ndio mwisho siku huna unageuka huna maana kwake.
 
Hapana mie naona atumie gari lake kama fursa ya kumuingizia kipato mkuu, kama ni Noah which i think it likely is atafute sehemu akatege awe anabeba abiria kama kidala dala itamlipa au atafute watoto wa shule awe anawabeba kistaili. Itamsaidia ila akiuza gari na amezoea hela ya kuchota hamna kitu atafanya.

Angekuwa na spirit ya biashara angeshafanya huyu jamaa from the beggining baada tu ya mambo ya kazi kuanza kuyumba.

Option nyengine atafte sehemu ambayo anaweza likodisha gari wakamlipa kwa week week.
kama sijakosea kwenye hili bandiko lake alizungumzia kuwa "gari yake haifai kufanya hata ubber", labda pengine ni mbovu mbovu
 
  • Thanks
Reactions: BRN
kama sijakosea kwenye hili bandiko lake alizungumzia kuwa "gari yake haifai kufanya hata ubber", labda pengine ni mbovu mbovu
Mmh labda kama mbovu ila kuna maeneo yana shida ya usafiri mkuu, kama yupo dar ruti ya gongo la mboto hakosi abiria. Hata akitege gerezani jioni anawaokota okota. Sio lazma uber kama gari ina nafasi hata nje ya uber anapata hela.
 
Pole sana kaka, hakika utanyanyuka...

Ila ulifanya makosa sana kumiliki magari matatu wakati unakaa nyumba ya kupanga. Huyo mkeo pia mwangalie kwa makini, yawezekana ndio wale wanawake wa mjini wanaopenda maisha ya anasa..

Pole sana, Maisha ni mapambano usikate tamaa na huu ndio wakati sahihi wa kuwajua marafiki zako wa kweli..
Ila seems jamaa alikuwa na shavu la uhakika mkuu, he was on the administrative position katika kampuni. Likely pay ilikuwa nzuri na deal za uhakika for years ndio maana hakuwa na wasiwasi na maisha. Its easy kuwa hivyo ukiwa unapata hela nyingi kwa muda mfupi sema tu bro mke hakupata.

Alipata mwanamke mwenye akili kijiko. Wale design wanajua kutanua tu mjini ila strategic planning ni 0! Ni mpaka usanuke wewe kuwa kuna kununua kiwanja na kujenga.
 
Pole ndugu. Ila huyo mke dah!
Hopefully utapata wa kukusaidia hapa jf
 
  • Thanks
Reactions: BRN
Unapoongea haya hivi unafikiri unaweza kum command mwanamke ambaye ana guts za kukimbilia kwao kwa kiburi tu sababu huna maisha. How do you begin convincing her wakati kilichomtoa kwako no dhiki. Jamaa alishakosea kuoa on the first place, hizo ndio consequences zake.

Ili mwanamke arudi ni lazima yale maisha mazuri yajirudie maana ndio ambacho kilimshawishi kuolewa na jamaa.

Pole mdau kiufupi kushuka kimaisha Ni Jambo la kawaida,Ila kikubwa tu maradhi uliyonayo ndo mtihani ulionao ,Cha pili mkeo ndo anazidisha maisha yko yanakua magumu ,kushuka kimaisha ndo mnatengana au ndo uliamua ,inabidi ukubali kwamba umeshuka na uanze kuishi maisha ya chini kabisa ilitakiwa upange vyumba viwili uswahilini ambayo jumla ingekua 50000 ,pia ungeuza hio gari ndogo uanze biashara ,hata wazo la biashara Niko tayari kukusaidia ,Mimi yalinikuta niliposhuka kimaisha nami nilikuali kuanza chini ,lakini kuhusu kuomba kazi utasubili sana kipindi Ni kigumu hiki kazi hamna, na mkeo asikichanganye mwambie mkapange uswazi na Pato lake liwe la familia kabisa nawe ,hakikisha mkeo unammiliki usimuogope
 
Kuna wakati unaweza ukamlilia Mungu sababu ya shida zako ila ukisikia ya wengine utajiona unakufuru[emoji2297][emoji2297]
Pole sana mkuu, Mungu akupitishe katika hilo.

Jamani muwe wema na muwatende mema wake zenu mnapokuwa katika nyakati nzuri ili wasiwatenge katika nyakati mbaya pia.


Sent using Jamii Forums mobile app
Usisahau hii methali "Tenda wema, uende zako". Siku hizi tuna watu kibao wanaotendewa mema lakini hawana shukrani.

Mke wa huyu bwana ni mbinafsi period. Si rahisi mwanaume mnyanyasaji akupe hela ya mtaji ili ufanye biashara msaidiane maisha. Hadi watoto wanalia baba arudi waishi kama zamani, it means walikuwa wanaishi as a happy family (japo changamoto hazikosekani). Afu mke alivyo mjinga anahisi anamkomesha mwanaume, kumbe anawaathiri watoto kisaikolojia. Naamini angeweza kabisa kukaa chini na watoto akatafuta perfect excuse ya kwa nini baba yupo mbali (japo wanajua walifukuzwa), na angedumisha mawasiliano ya baba na watoto. Kumuacha peke yake mtu aliyechanganyikiwa hivi, what if akifa, atakuwa amewasaidia nini watoto wake? As long as uwepo wa mume wake, jasho lake na kila kitu chake kilikuwa na direct impact kwake na kwa watoto; basi angeshikamana tu na mumewe katika kipindi hiki.
 
Pole sana mkuu Sodoku jikite katika maombi usimsahau mungu wako aliyekupa maisha mazuri kwani ndio huyu huyu anayekupitisha katika mtihani huu ili kukufundisha jambo ambalo naamini mpaka sasa hujalifaahamu..

Amini Mungu hakupi mtihani usio uweza. Utashinda ukimtegemea yeye.

Pengine alitaka kukuonyesha ni mke na marafiki wa aina gani ulionao ili ujue jinsi gani ya kuishi nao.

Utarudi katika mstari kwa uwezo wake yeye atutiaye nguvu..
 
Nimesikitika sana. Pole sana Mkuu kwa changamoto unazopitia. Ule msemo wa kosa hela uijue tabia ya Mkeo ni HALISI.

Pole sana Mkuu. Mungu wa Mbinguni atakuvusha katika hili pia.
Atamvushaje bila nauli. Mchangieni mwamba jamani. Naona pole nyingi mi nshanunua daftari hapa la michango.
 
Usisahau hii methali "Tenda wema, uende zako". Siku hizi tuna watu kibao wanaotendewa mema lakini hawana shukrani.

Mke wa huyu bwana ni mbinafsi period. Si rahisi mwanaume mnyanyasaji akupe hela ya mtaji ili ufanye biashara msaidiane maisha. Hadi watoto wanalia baba arudi waishi kama zamani, it means walikuwa wanaishi as a happy family (japo changamoyo hazikosekani). Afu mke alivyo mjinga anahisi anamkomesha mwanaume, kumbe anawaathiri watoto kisaikolojia. Naamini angeweza kabisa kukaa chini na watoto akatafuta perfect excuse ya kwa nini baba yupo mbali (japo wanajua walifukuzwa), na angedumisha mawasiliano ya baba na watoto. Kumuacha peke yake mtu aliyechanganyikiwa hivi, what if akifa, atakuwa amewasaidia nini watoto wake? As long as uwepo wa mume wake, jasho lake na kila kitu chake kilikuwa na direct impact kwake na kwa watoto; basi angeshikamana tu na mumewe katika kipindi hiki.
Huyo mwanamke bila shaka ni mchaga tu tena wa marangu😂
 
Mkuu hizo ndio aina za wanawake wa kuoa sasa. Mamaako angekuwa mbinafsi angemkimbia mshua amini kwamba. Wanawake wa sikuhizi wengi wabinafsi ni mbegu mbaya sana kuoa mwanamke wa hivyo. Usije ukaoa mke ambaye hawezi hata ku spend buku lake kwako! Utakuja kunikumbuka siku moja.
Kuna exceptions na hapa ndipo nakuja kuungana na Espy . Kuna wanaume wakiwa na mafanikio aisee mke ni takataka, familia inatelekezwa, baba anahamishia raha kwa michepuko. Afu anakuja kustaafu na pensheni imeisha, kisukari na presha zimepamba moto, ukute mwingine ndiyo na harara zimeamua kujimwambafy; eti ndiyo mtu anajirudisha kwa mkewe wa ndoa. As long as uwepo wako, jasho lako na raha zako hazikuwa na impacts kwa mkeo na watoto wako; na shida zako zisiwahusu pia, kwa kweli utakula ulikopeleka mboga.
 
Kuna exceptions na hapa ndipo nakuja kuungana na Espy . Kuna wanaume wakiwa na mafanikio aisee mke ni takataka, familia inatelekezwa, baba anahamishia raha kwa michepuko. Afu anakuja kustaafu na pensheni imeisha, kisukari na presha zimepamba moto, ukute mwingine ndiyo na harara zimeamua kujimwambafy; eti ndiyo mtu anajirudisha kwa mkewe wa ndoa. As long as uwepo wako, jasho lako na raha zako hazikuwa na impacts kwa mkeo na watoto wako; na shida zako zisiwahusu pia, kwa kweli utakula ulikopeleka mboga.
Sawa wapo watu wa hivyo ila kwanini tuwe judgmental kana kwamba hamna watu wenye upendo. Hebu nioneshe kosa la jamaa ni lipi hapo mpaka mke amfanyie ushenzi aliofanya. Mwanaume akupe mil.6 tena kwa kuuza asset yake ili ufanye biashara mpate maisha huyo ni mbinafsi?
 
Yaan naweza nisiwe sad kwa changamoto unazopitia ila MKE WAKO MPENDWA hapana mkuu. Amenisikitisha sana.
Kwani pale madhabahuni tunavyoapa kwenye shida na raha ninorally tu hakuna practical ama. Sasa nini maana ama faida ya ndoa? Huyu mkeo unamjua vyema kweli? Ila vielements vya ubinafsi huwa vinaonekanaga hata kipindi cha mahusiano. Tabia mbaya sana hii. Na pia huyu mke wako hakua na mawazo zaidi kiasi cha kuona kumiliki magari matatu ni sawa. Katika maisha yangu simpendi mtu mbinafsi mimi. Jaman tujitahidi tuwalee watoto wetu wawe kwenye njia sahihi. Mungu ni mwema sana.
Zaidi nameomba Mungu nisije kuwa mke mwenye ubinafsi. Anifanye nikawe kimbilio kwa wahitaji. Mwenyezi Mungu ni mwema. Nitakucheck pm mkuu
Mwanamke wa hovyo kabisa. Mkuu nakuombea pia ubinafsi ni roho ya kishetani. Nakuombea sana usije pata mwanamke wa aina hio abadani. Ni bora ufuge mbuzi tu sio kuwa na mwanamke mchoyo na asiye na akili. Usije kuwa miongoni mwa watu waliopata hasara maishani.
 
Shemeji hii ni situation nyingine kabisa (out of topic); ya huyu jamaa nimeielezea hapo juu na umeniquote kabisa
Sawa wapo watu wa hivyo ila kwanini tuwe judgmental kana kwamba hamna watu wenye upendo. Hebu nioneshe kosa la jamaa ni lipi hapo mpaka mke amfanyie ushenzi aliofanya. Mwanaume akupe mil.6 tena kwa kuuza asset yake ili ufanye biashara mpate maisha huyo ni mbinafsi?
 
Shida ya huyu jamaa itakua ataki kuanza upya ,na biashara sio zile za kuuza tu ,pia Kuna ufugaji ,wa nguruwe unapata faida kubwa kwa mala moja pia unaweza Lima zao la bamia na nyanya chungu siku 60 unaanza kula faida ,pia Kuna biashara ya mazao yenyewe kufilisika Ni uzembe wko tu
Kuanza biashara ukiwa huna uzoefu ni risk mara elfu 10! Esp. ukianza na limited amount of money...yani una 3M tu halafu uanze nayo biashara ambayo itakula hela yote? Sijui lakini maybe im over sensitive.

Heri uwe na million 30 uanze kwa trial and error hio biashara ya 3M you will have ten chances kama uko serious on the second or third chance you will likely win.
 
Pole Sana mkuu unajiona upo kwenye shida sababu ulikua na maisha kumiliki magari matatu sio mchezo ushauri wangu shusha pumuzi degree yako iweke pembeni jishushe maisha yako uwe mtu wa chini Kama machinga yaani ishi local life panga chumba ata single jifanye upo kutafuta maisha ndo umetoka mwanza Mara ya kwanza kufika dar ondoa fikira ya watu watanionaje Nina degree na nilikua na kazi nzuri fanya gari yako uwe mtaji au uza vitu vya ndani usikope benki wakati unaanza maisha plani biashara ambayo itakua na mzunguko mzuri na sio ya kutumia nguvu kutokana na mguu wako alafu ukisha fanikiwa ndo tafutaga kazi Apo utapata kiraahisi kazi kumbuka kupata kazi ni ngumu kama huna kazi ata ukija pata kazi utaweka mfanya kazi iweke iyo biashara yako ndo kazi kwa Sasa muombe MUNGU never give up brother
 
Ukweli, hii ndio namna sahihi ya mtu (member) anavyo takiwa kufanya pindi anapo kwama.
Sio Jambo jema na wengi tunakosea sana tunapokuja na ID mpya pindi tunapo kwama.
Member anapokuja na ID yake ilio zoeleke, inawapa wengine nafasi ya kumsaidia kwakua walau wengi wanakua na ufahamu kidogo kuhusu muhusika.
Na hiki huwa ndio kigezo changu no.1 ninapotaka msaidia yeyote anaetokea Ndani ya JF.
 
JPM ulaaniwe kabisa kwa kufanya makampuni binafsi yasipate kazi kutoka serikalini.
Pole sana wa Ng'wise .Njoo PM uniachie number zako nitakutafuta.
Imeniuma sana na degree yako unapewa pesa na house girl aliyemaliza la saba tu.
Sema nikasema mguu pia imesababisha. Otherwise ningekuambia katafute hata kazi ya ulinzi. Degree weka pembeni.
Ila pia wewe na mkeo sijui mkoje. Mkanunua magari matatu hata nyumba yenu hamjamaliza 🙄.Any way katika maisha priorities inatakiwa iwe need. Yaani bila gari nitaishi,ila bila nyumba itabidi nikabebwe.
Pole sana na kila lenye kheri.
 
Nimesoma na naendelea kusoma comments zenu. Hainipi shida majina mbalimbali ambayo wengine wameamua kuniita. I expected yote haya. I will keep on focusing. Kuna ambao wamekuja PM tubadilishane namba za simu.

Nawashukuru. Kidogo nakuwa makini kutosambaza sana namba yangu. Kwa mtu mwenye nia ya kusaidiana nami ataonekana tu. Lengo halikuwa kuomba michango msije nielewa vibaya. Yet najua wengine kwa nia njema wamenioffer msaada huo.

Nawaomba tu kabla hatujafikia hatua ya mbali zaidi ntapenda tufahamiane pia kama mtu hatojali. Siwezi jisikia amani kupokea anything kwa mtu ambaye hanifahami simfahamu. (Hapa naomba mnielewe)

Nimejifunza mengi ktk uzi huu pia. Wapo walionifariji na wapo ambao wameandika kile kilichojaa mioyoni mwao. Jambo lingine. Nsingependa sana kum victimize mke wangu. Tuna watoto 3. Atabaki kuendelea kuwa mke wangu. Naamini kuna siku atajifunza kitu. Je nliwahi mnyanyasa hapo nyuma? Si aina ya watu wa namna hiyo.

Ndo maana bado sipendelei watu wamshambulie. Nimeandika ili muone situation ninayo pita.pengine mjifunze pia. Kuna ambao wamesoma na bado hawakuelewa uzi huu. I am sorry for them.

There are good people wametuma namba zao tuwasiliane. Nimekubali kuwasiliana nao kwa kuwa najua pia natengeneza network na MARAFIKI WA WAKATI WA SHIDA. nahitaji zaidi watu ambao watakuwa radhi kujenga urafiki/undugu nami hasa kipindi hiki.

Its possible nlikosea hapo before.but nimegundua sipaswi ishi katika makosa hayo. Unaweza nihukumu upendavyo utakuwa sahihi. Nitajifunza zaidi kupenda na kumheshimu kila mtu. Hata ambaye atanichukia,atanidharau na kunikebehi.

Nimeona Kuna watu wema wamo humu na wale wengine pia wamo. Wote tupo humu humu. Nawashukuru. Ntaendelea kuwasiliana nanyi na kujifunza. Tuombeane zaidi.
Ushauri wangu kwa hiyo michango kidogo utakayo pata, jaribu ata kusaka vijana ata wawili wa kigogo kutoka dodoma wakuuzie kahawa.
Ina lipa sana ile mkuu, au vijana waku sambazie mayai ya kuchemsha.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom