Nahisi kufa nahitaji msaada wa haraka

Pole sana mkuu, ungejaribu na zile tiba mbadala za kichina huenda ukapata suluhisho la tatizo lako. Naomba usikate tamaa, endelea kujipambania huku ukizidisha na maombi pia.
Mkuu zimegonga mwamba niliendaga pale magomen mapipa walikuwepo pale

Ahsante ubarikiwe mkuu
 
Pole upo mkoa gani yupo docta bingwa wa haya magonjwa atakupa majibu yeye baada ya kupima mungu akuponye
 
Nenda ikonda mkuu usijali maelezo ya huyo mtu. Kule utapata jibu la ukweli.
 
Nimeenda sana mkuu et hawaon tatizo x ray, ct scan na mri nimepigwa sana bado hawakuona tatizo ndo mana natafta mtu alie pitia hali kama yangu

Ahsante kwa ushauri wako ntaendelea kwenda hospitalin nisipokufa hiv karibun
Pole sana, hilo linatibika hapo hospitali jiongeze
 
Kuna mtu alikuwa na tatizo kama hili miaka kadhaa nyuma. Aliponea Ikonda
 
kibiongo ndo nin mkuu?
Kibiongo ni tatizo la kupinda kwa mifupa wa uti mgongo

Sababu ya tatizo hili haijulikani kwa wagonjwa wengi.

Wengi huzaliwa na tatizo hili.Matibabu ya tatizo hili ni upasuaji, na huduma hii inapatikana katika taasisi ya mifupa (MOI)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…