Mkuu!! Sijui Imani yako, lakin naomba nikutie Moyo Kuwa pale ambapo akili zetu zinaishia basi hapo ndo akili za Mungu zinaanzia.
unaweza zunguka kila aina ya hospital, tatzo lisionekane, unajua haya Mambo sometime hayawezi tibika kwa Binadamu Bali kwa Mungu.
ushauri wangu kwako mrudie Mungu wako katika maombi yako nakusihi sana omba rehema kwa mwenyezi Mungu pia akuepushe na Roho za mauti, Roho za kichawi na mengine kadri Moyo utakavyo unakuongoza,
Tafadhari usiende kwa Manabii au Hawa wachungaji wanaotumia vitu mbalimbali kama sehem ya miujiza hao waepuke kabisa.
kama uwezekano upo mtafute Pastor Mwakasege huwa ana Maombi Au fanya hivi Tafuta kanisa la EAGT ingia kwenye maombi Muombe Mungu akurehemu makosa yako yote, yawezekana Mungu ana makusudi na wewe, kwaiy anakupitisha kwenye moto,,
Kingine ukiomba na tatzo Bado likaendeleaa usikate Tamaa Mungu yeye anasema hachelewi Wala Hawaii kwaiy wew endelea kuomba.
Faida ya Kuomba, itakutengenezea ukaribu Na Mungu na kama Kuna vitu vya asili vilipandikizwa ndani yako kama vya kishirikina, maroho ya kurithi, pamoja na Nguvu zote za shetani zitaondolewa kwako. Lakin pia ikitokea siku ya kuish hapa Dunian imeisha basi utapokelewa na malaika wa Mungu. Kingine ukiwa unaomba usichoke najua shetana hatapenda atajutia Roho za uchovu wa kuomba au kuchanganya mambo mbalimbali Ili urudi nyuma ko jitaidi umuombe Mungu akuepushe navyo.
Usikate Tamaa, Kuna mwanamke aliteseka Miaka 12 lakin siku alipokuta na Yesu alipona kabisa na ugonjwa wake ukaisha,
Ezekieli Umri wa Kuishi ulipo Isha alimuomba Mungu na Mungu akasikia kilio chake akamuongezea miaka ya 15 ya Kuishi, Never Give Up Mkuu.
Mungu akusaidie.
Mungu msaidie Huyu Mja wako wewe unasema Kuwa hushindwi kitu Mungu Binadamu tunaweza kushindwa kuona tatzo lakin wew Mungu huwezi shindwa kuona, mponye mtoto wako Kila aina Roho chafu zilizo enda kupandikizwa juu yake Roho za Mauti zinazomtafuta Mungu muepushe na umsaidie apone, jina lako lihimidiwe Amen.