Nakosa cha kuandika ila itoshe kusema kwa hapa nilipofika nahitaji msaada wa kiroho. Mambo hayaendi kila nachofanya hakiwi, nipo ila sionekani yaani ni kama nimezimwa.
Nini nifanye ili nitoke hapa ? huenda wapo waliopitia hali kama hii je mbinu gani mlitumia kujinasua kwenye kiza kama hiki?
Siumwi na chochote ila changamoto kubwa kipato. Ni kama nimefungwa (nikama nimepigwa pini sio za kawaida) naijiona kabisa sio mimi
Nahitaji mambo yafunguke maisha mengine yaendelee kama wengine wanavyofurahia maisha na mafanikio na mimi nataka kwangu iwe hivyo.
Nawasilisha (karibu kwenye comment &karibu Pm)
Mjomba,
Kwanza acha habari za kuona kuna mtu au kitu kimezuia wewe usitoboe, Jiangalie mwenyewe kwanza. Ukianza kuangalia visababishi vya nje hutaviona visababishi vyako mwenyewe.
2. Jikubali usijilinganishe au kujifananisha na mtu, usitamani kuwa kama fulani, kuishi kama fulani bila kutamani kufanya kama huyo fulani anavyofanya ilo uwe kama yeye, na ukitamani kuwa kama fulani anza kutamani kuanzia mwanzo kule alipoanzia mpaka akafika hapo alipo.
3. Mafanikio na furaha katika maisha ni matokeo ya mapambano ya bila kukata tamaa katika maisha, hamnaga mafanikio ya kupewa au kuletewa.
4. Fahamu utofauti kati ya vitu MUHIMU katika maisha na vitu vya MAANA katika maisha.
Vitu vya maana ni UPENDO,FURAHA, AMANI NA UHURU. Hivi ili uvipate lazma kwanza uwe unavyo. Huwezi pendwa kweli bila kupenda kweli, huwezi kutegemea kupewa furaha wakati wewe hutoi furaha, huwezi kupata amani na uhuru wakati wewe hutoi uhuru na amani. Hivi vitu haviuzwi, vinatafutwa ndani ya watu na vinalelewa na kuambukizwa na kurithishwa na kuendelezwa.
Vitu muhimu ni Fedha, Marafiki, Elimu. Hivi vinatafutwa kwa na kupatikana kwa kuzingatia Utu, Uelewa mzuri, na Subira. Kumbuka, hivi ni vya muhimu lakini sio vya maana. Ikivizingatia sana hivi ukapuuzia vile vya maana bado utakuwa hujakamilika na utahangaika kutafuta tulizo la nafsi kila siku.
3.Tuliza moyo wako,kubali mapungufu yako, rahisisha mahitaji yako, ongeza kipato chako.