TAI DUME
JF-Expert Member
- Feb 20, 2014
- 9,748
- 26,238
wakuu sjui kama huu uzi ulishawahi kuletwa huku au bado ila kwa anayefahamu anaweza kunishauri.
Ninaweza nikawa nafanya kazi fulani, au niko mahali fulani au nakutana na watu fulani lakini huwa napata hisia halisi kabisa kwamba hicho kitu nilishawai kukifanya katika muda na mazingira yale yale hata kama ndio nafanya kwa mara ya kwanza. Au naweza nikakutana na watu ambao siwafahamu lakini akili inakuwa inalikumbuka hilo tukio kabisa yaani kama ilishawahi tokea kabla. Hii inanitokea katika mambo mengi na ni mara kwa mara. Kwa maana ya kwamba huwa nahisi kuona vitu ambavyo havijanitokea.
Kiukweli hali hii siipendi kwani inanipa hofu na kuumiza sana akili yangu kwa kutaka kujua kwa nini inakuwa hivyo. Mpaka naandika hapa imenitokea tena jana nilipoitwa kwa kiongozi wangu wa kazi na kunipa barua ya promotion, Yani lile tukio lilivyokuwa linatokea nikakumbuka mpaka maneno atayoongea mwishoni na ikawa hivyo,
Mwenye utaalamu na haya mabo tafadhali.