G'taxi
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 6,625
- 8,639
wakuu sjui kama huu uzi ulishawahi kuletwa huku au bado ila kwa anayefahamu anaweza kunishauri.
Ninaweza nikawa nafanya kazi fulani, au niko mahali fulani au nakutana na watu fulani lakini huwa napata hisia halisi kabisa kwamba hicho kitu nilishawai kukifanya katika muda na mazingira yale yale hata kama ndio nafanya kwa mara ya kwanza. Au naweza nikakutana na watu ambao siwafahamu lakini akili inakuwa inalikumbuka hilo tukio kabisa yaani kama ilishawahi tokea kabla. Hii inanitokea katika mambo mengi na ni mara kwa mara. Kwa maana ya kwamba huwa nahisi kuona vitu ambavyo havijanitokea.
Kiukweli hali hii siipendi kwani inanipa hofu na kuumiza sana akili yangu kwa kutaka kujua kwa nini inakuwa hivyo. Mpaka naandika hapa imenitokea tena jana nilipoitwa kwa kiongozi wangu wa kazi na kunipa barua ya promotion, Yani lile tukio lilivyokuwa linatokea nikakumbuka mpaka maneno atayoongea mwishoni na ikawa hivyo,
Mwenye utaalamu na haya mabo tafadhali.
Mala zote nafsi hua inaweza kujua kijacho.Mungu ametuumba kwa namna ya mfano wake,akili yako inaweza kua na mambo mengi mpaka ikafuta kumbukumbu zote,lakini sio nafsi yako,unapoona mambo hayo inaonyesha uwezo ulio ndani yako kua ni mkubwa sana,tatizo hua ni jinsi gani utaweza kuchochea hiyo nguvu ikatenda kwa uhalisia zaidi ya hapo inapojionyesha na kwa akili zako zilizosongwa na mambo mengi isijue ni kitu gani kinaendelea,kiufupi usemacho ni nafsi iliwahi kujua kuna siku utapitia katika mambo kadhaa ambao ndio kama hayo,walioweza kutumia uwezo huo wapo kama vile wahubili na hata wasoma nyota ambao huitwa ni waongo na matapeli,lakini ukweli ni kwamba hutumia nguvu hizo kama ulizonazo,japo nakushauli ukitaka kujua vyema ni nini nafsi yako inaweza ikasema yajayo mshilikishe Mungu na si mwanadamu.hayo ni mawazo yangu kwa uelewa wangu,usiogope juu ya hilo,hiyo ni nafsi inakukumbusha kua iliwahi kukwambia utapitia hapo ila hukuweza kutunza kumbukumbu kwa sababu akili inabeba vitu vingi
