Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hata bange sometimes huleta maono ya jinsi hii
Inaamina dunia ilishaisha sasa wale watu walio ishi ndo wanakumbukia maisha so hata hapo unapoishi ni unakumbukakia tu kama mm ninauwezo wa kuona cku nzima ya leo nikiwa nimelala
wakuu sjui kama huu uzi ulishawahi kuletwa huku au bado ila kwa anayefahamu anaweza kunishauri.
Ninaweza nikawa nafanya kazi fulani, au niko mahali fulani au nakutana na watu fulani lakini huwa napata hisia halisi kabisa kwamba hicho kitu nilishawai kukifanya katika muda na mazingira yale yale hata kama ndio nafanya kwa mara ya kwanza. Au naweza nikakutana na watu ambao siwafahamu lakini akili inakuwa inalikumbuka hilo tukio kabisa yaani kama ilishawahi tokea kabla. Hii inanitokea katika mambo mengi na ni mara kwa mara. Kwa maana ya kwamba huwa nahisi kuona vitu ambavyo havijanitokea.
Kiukweli hali hii siipendi kwani inanipa hofu na kuumiza sana akili yangu kwa kutaka kujua kwa nini inakuwa hivyo. Mpaka naandika hapa imenitokea tena jana nilipoitwa kwa kiongozi wangu wa kazi na kunipa barua ya promotion, Yani lile tukio lilivyokuwa linatokea nikakumbuka mpaka maneno atayoongea mwishoni na ikawa hivyo,
Mwenye utaalamu na haya mabo tafadhali.
Hiyo kitu wanaita deja vu
Kila mtu anayo sio wewe tu
But hakuna scientific explanation inayotosheleza kueleza hiyo kitu
Wala usiogope
Pia Muda mwingine ni ndoto ulizozisahau af zinakuwa kweli
Sent from my iPhone using JamiiForums
Mkuu Kawoli, Kuna mada moja nimezungumzia muda wa ulimwengu na matukio yake naona swali/mada yako linaendana na kipengele fulani cha future katika muda.
Kuna somo moja linapendekeza kuwa kutokana na jinsi tulivyoumbwa tunauona muda kama unakwenda mbele (flowing) na kwamba kuna past present na future. Past inaonekana kama imepita na haiwezi kubadilika na present inaonekana ndio au inahusishwa na reality alafu future ni kama vile haijatokea wala details zake hazijakuwepo. Flow ya muda ni illussion na ni matokeo ya jinsi ubongo wetu ulivyoumbwa.
Matukio yaliyo katika muda uliopita uliopo na unaokuja, yote yako katika mpangilio ambao una uwiano sawa na yaliyopita ni sawa na yanayokuja ila sisi binadamu kwa kawaida tunakumbuka yale yaliyopita (past) zaidi. Kutokana na ukweli huu wa kwa kawaida tunaweza kukumbuka past na siyo future hii inatujengea false impression kwamba muda unapita/unaenda kwa sababu kile ambacho hatukukijua (future) kimekuwa tunachokijua (past).
Kwakuwa future ni real na haiwezi kubadilishwa kama ilivyo past unahisi umekumbuka future? Kuna logical views nyingi zinazolezea kwa nini hatuwezi kukumbuka yale yaliyo mbele yetu ingawa yapo. Najiuliza je kama ungeamua kukataa promotion hiyo unadhani ungekuwa umeingilia mpangilio wa future? - kwa kuwa ulijua mpaka maneno ya mwisho yatakayosemwa na bosi wako.
inapatikana zaidi hapa:
HowStuffWorks "How Déjà Vu Works"
Ni vema kuvumilia makala ndefu na kujifunza zaidi mambo tusiyoyajua.
Daah Mimi huwa zaidi ni ndotoni alafu likija kunitokea nakumbuka picha nzima.sasa hivi huwa Nina naandika kwenye kitabu harafu huwa linatokea kweli daah mbaka naogopa .Kuna jamaa yangu kaniambia kwamba sisi binadamu ni wa toleo jipya kwa hiyo roho zetu zilikuwepo kwa watu wengine wanaofanana kila kitu na wewe uliye sasa wao walikufa matendo yanayojirudia ni yaleyale ijapokuwa ktk mazingira tofauti
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums