Wakuu habari, nilienda hospitali,
Ila doctor nilivomuelezea kuwa nahisi maumivu upande wa kushoto wa moyo , walifanya x ray, ila haoni kitu, nikapewa dawa za maumivu nitatumia 2 weeks, akasema kam hali itaendelea basi nirudi tena pale.
Ila pia muda mwngine nahisi maumivu hadi upande wa kulia na tumboni.
Wakuu mwenye mawazo zaidi hapa?
Ila pia huwa nina tatizo la asthma haswa kipind cha baridi na upepo , huwa nakuwa naumia kifua, au hii inaweza kuwa sababu?
Mana pia nahisi kifua kizito kwa mbali hivi.
Kuna mambo ya kuelewa hapa;
1: Maumivu upande wa kushoto karibu na sehemu ya ziwa na katikati ya kifua si vyema kubaki au kukaa nayo bila kufikia mwafaka wa ni nini hasa tatizo.
Hii ni kwa sababu wakati mwingine yanabeba ujumbe wa magonjwa ambayo ni dharura/Emegency.
Pia, umri, uzito na magonjwa mwambata kwako na kwenye familia ni vyema kuyafahamu.
2: Aina ya maumivu: ni vyema kujitahidi kueleza jinsi maumivu yanavyouma kwa kusema nini unakisikia mfano: kubana, kufinya, kuchoma nk., dalili ambatanishi kichefuchefu, kutapika, kushindwa kupumua nk.
3: Hali inayoanzisha maumivu na inayokupa nafuu. Ni vitu gani ukifanya maumivu huja, mfano: kuvuta pumzi, kukohoa nk. na vitu gani ukifanya maumivu hupungua mfano: kupumzika, kuinama, kusitisha kazi nk.
4: Muda: maumivu yanapotokea hudumu kwa muda gani?
5: Maumivu yakitokea huyahisi kwenda sehemu yoyote ya mwili zaidi ya pale yalipoanzia?
Haya matano kwa uchache hapa juu yatasaidia ni kipi ukichukue na kipi ukitoe kwenye mawazo ya nini mgonjwa anaumwa.
6: Je mtaalamu wa afya akigusa kifua au tumbo kuna maumivu yoyote?
Hivyo, si vyema kukaa na haya maumivu ukijaribu dawa bali kupata tiba sahihi. Tiba sahihi itahusisha uchukuaji wa: Historia ya mgonjwa vyema, ukaguzi wa mwili na vipimo kulingana na yaliyong'amuliwa. Kuna hali hufanana kwa utokeaji wake hivyo tunahitaji vipimo kutusaidia.
Ukiangalia tiba uliyopewa, naona hakukuwa na majadiliano ya fikra ipi daktari alipata ndo akakuandikia dawa. Kuna vitu vinaelea.
NB: Hakikisha unapata mwafaka wa nini ni tatizo kwa kufuata mtililiko hapo juu na uwe wazi kujadili na mtoa huduma wako/muulize maswali ya maoni yake kabla na baada ya vipimo, kama unaweza kumpata physician/daktari bingwa wa magonjwa ya ndani fanya hivyo.