Nahisi ndoa yangu inaelekea ukingoni kutokana na tatizo la nguvu za kiume

Nahisi ndoa yangu inaelekea ukingoni kutokana na tatizo la nguvu za kiume

Habarini wakuu!

Wakuu naombeni ushauri wenu juu ya hili linalonikuta ndugu yenu.Najua kutakuwa na kejeli na dhihaka lakini yote nitashukuru.
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 31 ambae nimefunga ndoa na ndoa ndiyo Kwanza ina miezi sita.

Tatizo langu liko kwenye upande wa nguvu za kiume.Nashindwa kabisa kumridhisha mwenzangu sababu ni kwamba siwezi kurudia tendo Kwa mara ya pili na hata hicho kimoja yaani ni haraka kama kuku hata dakika tatu haziishi.

Nimejaribu dawa mbali mbali pasipo mafanikio yoyote.Najua kabisa namtesa mke wangu lakini nimeshndwa namna.

Nimekuja kwenu wanajamvi mpate kunishauri by the way mazoezi na vyakula nazingatia sana mimi sio mtu wa kunywa pombe wala vinywaji kama soda na juice za viwandani sio mpenzi.
komaa tu mambo yatakaa sawa piga mazoezi kula vizuri na maji ya kutosha,wakati wa tendo la ndoa usifikrii kushindwa gemu mapema,usiwaze kuachia wazungu mapema weka akili yako kwenye matatizo ya serikali hii ya awamu ya 5 ya utekaji,demu lazima afike kileleni
 
Najitahidi Sana kujaribu hii kitu lakini nakwama
Mkuu kama uume unasimama vizuri kabisa kabisa, nakushauri u relax! Usitumie madawa, baadala yake ule vizuri vyakula na matunda hasa hasa parachichi, ndizi na tikiti maji kila siku. Usifanye sex kila siku, jipe muda wa kurelex.

Kurudia tendo sio ujanja wala ufahari, ufahari ni kupiga bao la nguvu, tumia dk 8 hadi 20 kwa bao moja, huna haja ya kurudia, kikubwa kumridhisha. Tumia mikono yako vizuri akojoe kabla hujamuingia ili ukiingia unamkojoza moja anakuwa katosheka.

Mpende mkeo, kuwa mwaminifu kwa mkeo, You will be rewarded. Usisahau kijana, punyeto na zinaa ni adui wa ndoa yako
 
1. Piga goti muombe Mwenyezi Mungu akuondolee hii hali (kama huyo ni mke wa halali)
2.Hakikisha chumbani una Jagi la Maji kila jioni na unywe maji ya kutosha mara kwa mara usiku mzima, Uume unahitaji damu ya kutosha, ni lazima uwe hydrated ili kuleta matokeo mazuri.

3. Wewe huna tatizo, una tatizo la uoga, huenda tatizo lilikutokea mara moja likajenga uoga akilini mwako,basi tokea wakati huo ukiwa kwenye tendo kumbukumbu ya hilo jambo inakutokea na wewe unakuwa unapoteza erection.

4. Uoga huambatana na Stress, Stress hormone huzuia Testosterone hormone kufanya kazi yake

5. Solution ni kuongea na mkeo kila kitu, mueleze hofu yako kwamba Tatizo lilipokutokea mara ya kwanza uliogopa, ukaogopa jinsi atakavyokuona, mwambie akusaidie ili tatizo hili liishe!. Utashangaa pale atakapokupokea na kulichukulia kuwa hilo jambo la kawida, THE MOMENT ATAKAPOKUONDOLEA PRESSURE YA KUPERFORM UTASHANGAA UNARELAX NA IMMEDIATELY UNAJIKUTA JAMAA ANAITA!

6. Fanya mazoezi, jitahidi kuwa in good shape, beba vitu vizito (siyo uwe baunsa), kimbia

7. Kula matango, machungwa na tafuna punje ya Kitunguu swaumu [Chungwa na Kitunguu swaumu imethibitika kusaidia kutengeneza Nitrogen oxyide ambayo ni nzuri kwa kusimamisha uume]
8. Kula karanga mbichi
9. Wasikudanganye kuhusu pombe, Pombe siyo nzuri kwa nguvu za kiume, mwanzo unaweza usione athari lakini eventually itakuharibu!. iogope pombe kama UKOMA

10. TATIZO LAKO KUU LIKO KATIKA UBONGO, UNAWEZA USIJUE WALA KUAMINI KUWA HOW, LAKINI HAYA MAMBO YANAWORK BEHIND THE SCENE KWENYE UBONGO!. KILA SIKU UWE UNATAMKA MANENO KUJIAMBIA KUWA "MIMI NI RIJALI, NINAWEZA, TATIZO LILILOTOKEA NI KWA SABABU TU SIKUWA KATIKA MOOD, LAKINI NIKO VIZURI SANA"
 
Anza na physical training, weka afya sawa mzee inasidia sana kupunguza stress. Mazoezi yanasidia kujenga afya ya akili.

Usikamie game, upate kikombe cha kahawa per day at least 5gm per day.

Umri ulionao ni wa kujiamini, jiamini kuwa unao uwezo wa kuwasha moto pale chini kwenye maji na ukawaka na maji kukauka.

Unaweza shauriwa mengi humu ndani, lakini changes start with you.

Pole sana, haya mambo yana changamoto pindi ukikutana na mwenzako ambaye ameshasuguliwa vya kutosha na wahuni.

Cheza show za kibabe, acha na habari za kimungu mungu!
 
Tatizo la nguvu za kiume ni la kisaikolojia tu,... Sasa umeanza kumuogopa mkeo hasa inapokaribia mida ya kwenda kulala...
Umekua hujiamini tena kwamba wewe ni dhaifu huwezi tena,....
Mkeo ndiye mwenye tiba ya jambo hilo..
Kwa kuanzia alipaswa akutie moyo na kukusifia kwa kukuondolea hofu kwamba humfurahishi,.. Akusifie kinafki kwamba amefurahia na umemfikisha vzr sana... Asionyeshe kama anateseka bali akufanye ubadilishe moyo wako wa kujiona huwezi tena, hata pale asipofika kileleni, hii itakupa nguvu ya kujiamini... Hakika ndio tiba yako, dawa hamna hapo
 
Chief Mwenyezi Mungu akubariki Sana yaani! Nimekupata vyema kabisa,kuna jamaa yangu ktk kutafuta ushauri aliniambia mke wake alikuwa bega Kwa bega na yeye ktk kutatua hili tatizo,bahati mbaya mimi mke wangu kuna muda tunakuwa pamoja kuna muda ana panick Sana full misengenyo Ila all in all ni muelewa acha nikae nae chini nilifanye hili zoezi pia.Shukran Sana mkuu
pole sana mzee kikubwa hapo ndugu jifunze kujicontrol mwenyewe kumaliza mchezo yaani haya mambo hata kama ukila kitu gain au ufanye mazoezi ya aina gani kama hutaweza menyewe kucontrol huezi njia ya kujicontorol ni kama wakubwa walivokwisha kusema halafu pia hata ukinunua hiko kidonge ulichoambiwa makeshua unajicontrol kuto kumwaga mapema maana hiko kinakusaidia kusimama tu ila sio kumwaga na shida ni kumwaga...kama ungekua hujaoa ungejaribu kuanya na maemu wengine hiyo ingekupa more experience maana sa hivi unaona sex kama ni kittu kigumu na hiyo ndo sababu
 
Habarini wakuu!

Wakuu naombeni ushauri wenu juu ya hili linalonikuta ndugu yenu.Najua kutakuwa na kejeli na dhihaka lakini yote nitashukuru.
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 31 ambae nimefunga ndoa na ndoa ndiyo Kwanza ina miezi sita.

Tatizo langu liko kwenye upande wa nguvu za kiume.Nashindwa kabisa kumridhisha mwenzangu sababu ni kwamba siwezi kurudia tendo Kwa mara ya pili na hata hicho kimoja yaani ni haraka kama kuku hata dakika tatu haziishi.

Nimejaribu dawa mbali mbali pasipo mafanikio yoyote.Najua kabisa namtesa mke wangu lakini nimeshndwa namna.

Nimekuja kwenu wanajamvi mpate kunishauri by the way mazoezi na vyakula nazingatia sana mimi sio mtu wa kunywa pombe wala vinywaji kama soda na juice za viwandani sio mpenzi.
Hallo
Comment zimetoka nyingi na nzuri sana
Nahis nimechelewa kutoa mchango wangu.
Ila nitakupa principle kadhaa
Sio dawa yankunywa na sio lazima ufuate kila siku ila maintain kwa week 3 tu
Then kajaribu

1.fanya mazoezi
Usiende gim.instal app za home exercise i recomend (push up app)
Anza kama biginer piga pushup kila siku asubuh na jion anza kwa 10 panda kwa ratio ya 5 kila siku.siku 2 adi week 3 utaweza piga pushup 50 adi 70 non stop
Ukiweza kimbia kidogo au tembea mwendo mrefu
2.matunda na mboga za majani
Matunda na mboga za majani iwe sehem ya maisha yako kila siku
Tikiti maji liwe tunda kuu
Kwa kuwa tunapambana na nguvu angalau kila siku asubuh na jion kula kipande kimoja cha tikiti na usiteme mbegu
3.maji
Tumia maji mengi
Has muda umekaa nyumban weka hata lita 3 tumia jion tu
Kuanzia saa 12 adi saa 3 utakuwa umemaliza hopefully utaenda toilet sana ila ndo yanaingia nankutoka na kufanya kazi yake
4.pumzika
Jipe muda wa kupumzika hasa baada ya kazi
5.stress
Ishi maisha ya stress free life kama ni changamoto za kimaisha shirikisha ndugu.jamaa na friends wakusaidie kutatua lengo usiwe na stress
6.mpende mwenza wako
Anza kumpenda upya
Mpe yale maneno ulikuwa unampa wakati una mfikuzia. Mpe vi zawadi kuimalisha mapenzi yenu

Na njia ambazo wametoa ushauri wadau hapo juu
Kimbuka kwa week hizo 3 usipige game na shemeji.
Mpe sababu au mshirikishe hizo njia ili akusaidie ku track progress yako
After
3 to 4 week njoo na utoa feedback
 
safuher,

Myself nime experience hiyo hali baada kula vitunguu saumu punje kadhaa, next day nilianza kuhisi baridi kidogo kidogo kama naumwa malaria, nika lose appetite. Kufika jioni hali ilikuwa mbaya sana.

Mara nyingi huwa na fanya psychological treatment, healing. Kingine mimi ni mtu wa amzoezi alafu sipendi kutumia madawa ya hospitali labda tumbo la kuhara tu mkuu.

Basi nilikomaa, sikuweza hata kula mwili unachemka vibaya mno na vibrate kama tetemeko la ardhi. Cha ajabu nilikuwa sitoki jasho ki ukweli niliteseka mno usiku kucha sikumbuki ni saa ngapi nilipata usingizi.

Kulipokucha nilikuwa 50 kwa 50 mzima ila kichwa kinauma vibaya mno! Next day mzima kabisa!

NB: Sio kwa watu wote lakini, baadhi ya watu huleta shida kama hizi, mmoja wao mimi! Kama unataka kutumia kuwa makini anything can happen usijsema hukujua
 
Juzi nimetumia kitunguu saumu nilichanganya na tangawizi na asali.sasa jana nimeamka yaani najisikia hali kama naumwa Malaria. Nikalala saa 3 nimeamka saa sita hapo mwili kama una homa.
Nimeenda kusali nikiinama kichwa kinabwita bwita kwa kuuma nikiinuka afadhali.

Sasa nikahisi ule mchanganyiko wa juzi ila sio mara moja kutumia ndo mana nikauliza hivyo.

Ntatumia tena zaidi nione kama ile ndo sababu ama vipi Humorous Junior
 
Nimesoma hiyo dawa ya Citalopram, ukieendekeza unaweza ukajimada bora utumie dawa za asili ila zisiwe kali sana maana mtu ukihisi una huo upungufu una paniki kichii unaweza ukaambiwa mafuta ya break ni dawa ukajikuta umetumia.

Screenshot_2019-05-11-13-49-36.jpeg
 
Juzinimetumia kitunguu saumu nilichanganya na tangawizi na asali.sasa jana nimeamka yaani najiskia hali kama naumwa malaria.nikalala saa 3 nimeamka saa sota hapo mwili kama una homa.
Nimenda kusali nikiinama kichwa kinabwita bwita kwa kuuma nikiinuka afadhali.

Sasa nikahisi ue mchanganyiko wa juzi ila sio mara moja kutumia ndo mana nikauliza hivyo.

Ntatumia tena zaidi nione kama ile ndo sababu ama vipi

NAKUSHAURI UACHE MZEE, MAANA HICHO NDICHO NILLICHOKIPATA BAADA YA UTAFITI WANGU
 
Humorous Junior, Mkuu nimekoma kabisaa wala haina haja ya kuniambia.

Ilinipata homa hiyo balaa,mwili hauna nguvu,mpaka nikapelekwa hospitali nimepimwa UTI na Malaria hamna.

Niliporudi tu nikamwaga ule mchanganyiko.

Ila sasa hivi natafuta kwa umakini sana.

Aisee hatari sana.sitosahau.
Nililala nikaota ndoto nawaona watu wakubwa wakubwa
 
Tafuta kitabu kinaitwa sexual reflexology cha Mantak Chia kitakusaidia tatizo lako.
 
Back
Top Bottom