Mkuu jaribu kufanya hivi,
1. Jifanye unahasira, yaani jifanye ume-mmind kwelikweli kana kwamba kosa ni lake
2. Mwambie ajiandae(Aoge na avae nguo za kutokea) kisha anzeni safari, hakikisha unakahela mfukoni
3. Mkiwa njiani, mwambie "mama Solomon bila shaka unajua kilichotokea jana" basi naomba niambie ni mwanamke gani au mwanamme gani aliyekamili katika njia zake??? Yaani hajawahi kukosea??? Hakika Nikimjua huyo nitamfanyia jambo la ukumbusho
4. Bila shaka hataweza kumtaja, mkiwa mnaendelea na safari yenu, mwambie leo hii umejua siri zangu tena huenda umeijua muda muafaka ili nisiwe mgeni tena kwako bali umenijua katika yote.
5. Mwambie, kama uliweza kuishi na mimi kwa amani miaka yote hii bila kuyajua haya, je si nizaidi ya hayo ukiisha kunijua???
6. Mwisho, mwambie samahani kwa kuujeruhi moyo wako, nakuombea amani iwe pamoja nawe, NISAMEHE na kuniombea niyaepuke haya, kisha ingia dukani mnunulie vyupi, hereni, sidiria n.k kisha mrudi nyumbani kwa amani.