Mimi ni kijana ambae nina mshukuru sana Mungu tokea nimezaliwa hadi hapa nilipofikia, watu wamenisaidia na bado wana nisaidia.
Kuna Muda huwa nina kufuru au kukana kutkukubaliana na uwepo wa Mungu😭 hii ni kutokana na asilimia kubwa ya matarajio yangu tokea nikiwa mdogo hayakuwahi kutimia.
Maisha yangu yamekuwa ya mitihani sana, kila nilichojaribu kuanzisha hakikuwahi kufika mwisho 😭😭😭 kwakweli nimeishi nikiwa na huzuni na furaha chache, mpaka hapa nilipofikia nina watoto wa 3 ambao ninawapenda mno.
Vipo vitu vichache ambavyo vinanitokea hivi sasa vinapelekea mimi kuhisi pengine siku zangu hapa Duniani zina karibia kuisha.
Hivi karibuni kichwa changu kimekuwa kizito mno kutoa maamuzi na ni kama kichwa kinanielemea, kimekuwa na maumivu fulani mithili ya kichwa kilicho toka kuuma!
Kwa taaluma mimi ni Mwandishi wa Habari ambaye napenda sana kusoma vitabu na asilimia kubwa ya vitu vingi nimejifunza kutokana na kusoma vitabu, lakini hivi karibuni nimepatwa na hali ya kutokuelewa kila ninacho kisoma.
Vitabu vyote ambavyo nilikuwa navipenda nikivisoma nahisi vinanichanganya, hata baadhi ya mada nilizokuwa nazipenda hapa JAMIIFORUMS nazo pia nimekuwa sizielewi.🥲
Nimepatwa na hofu hata nikikaa karibu na watu ninaowapenda sifurahii uwepo wao, nahisi kujitenga tu nikae peke yangu tu muda wote.
miaka ya nyuma nilikuwa na ndoto pengine za kuwa fulani nikawa naziishi ndoto hizo kwa kuzipambania kwa vitendo lakini siku bahatika kuishi maisha ya ndoto zangu.
siku hizi ni kama siioni future yangu kabisa... muda mwingine mpaka najiona kabisa kama napoteza tuu muda 😭😭😭😭
kama ninge kuwa simu hope ingekuwa kwenye flight mode ✈️🤣🤣🤣
Ikitokea hamjaniona hewani mwezi mzima mfululizo mjue siku zangu niliziona kabisa zinahesabika hivyo malaika mtoa roho atakuwa amesha fanya yake.
Sifikirii kabisa kujiua kwa aina yoyote ile japo kwenye maisha yangu udogoni mwanangu nilishawahi mara 2 kujaribu kujiua. 😭
Mara ya kwanza nilijaribu kunywa sumu haikuniua, hapo nilikuwa na miaka 9 au 10, mwaka mmoja baadae nilijaribu kujinyonga bahati mbaya kile kitanzi pia hakikuondoka na maisha yangu.
Hivyo nichukue fursa hii kuwaaga ndugu zangu wana JAMIIFORUMS ambao tumeishi wote humu ndani kama familia. Kuna member humu nimesaidiana nao bila hata kufahamiana nao big up sana.
Kuna wengine tumekuwa ndugu na hata nje ya JAMIIFORUMS tumekuwa tukionana kwakweli sina cha kuwalipa.
Ushauri wangu kwako fanya unachoona kinakupa AMANI.
Suala la kifo ni kila mtu atakufa, ni suala la muda.
Otherwise , nakushauri Maisha usiyachukulie sana serious , it is just game , so play it
.Wala usiwe na expectations zozote na Maisha, wewe play the game , ukipata sawa ukikosa sawa.
Wala usi expect sana kuwa Mungu atakupa, he might also disappoint you ! Just live . Pigania unachokiweza, usichoweza accept , wala usiforce
Kuna watu wanazaliwa na Cancer , debilitating damage kwenye maisha yao, na wanapambana sana, with no Blame to anyone.
Kwenye hii dunia, no one will save you , hayo maombi ni Comfort zone na insecurity zetu, unajiongelesha mwenyewe na kujijibu mwenyewe.
No one will save you except your self , so be responsible na maisha yako. Kama comfort zone yako ni maombi basi nenda, but maombi won’t help if you are not willing to help your self
Just keep in your mind , no one will get out of this world alive ; NI SUALA LA MUDA; mengine yote ni story za insecurity zetu