Mkuu
Prince Mhando mhando natamani nikuone uso kwa uso niseme na wewe neno .
Ndugu shukuru sasa unao uzao wako , shukuru unao uwezo wa kula milo mitatu na bado unaiona kesho hata kwa kuumia kama hivi kuwa kwanini siwi yule niliyejiona huko .
Ndugu majukwaa haya ni mazuri ni mabaya na ukweli ni kuwa umekata tamaa na pia unahisi mtazamo wa watu walio wengi hapa kwakuhisi bado uko chini rafiki wote tuna shida zetu tunatamani kuongea tumpate walau mtu aseme pole lakini ukikumbuka pole nyingi haziponyi maumivu basi tunavunga .
Rafiki hao watoto wewe ni baba yao , mama yao yupo ila mhimili ni wewe hauwazi kujiua leo ila utawaza kujiua kesho sasa wanao watalelewa na nani? Huko mtaani umebahatika kuwaona watoto wa mtaani lakini ??
Vipo maisha ya single mothers hapa bongo unayona ? Basi lea kizazi chako , simama pambana bado ni asubuhi jioni haijafika itafute nuru maana bado mshumaa wa mapambano haujazimwa .
Iishi leo achana na mambo ya zamani mazuri kwa mabaya uliyotenda focus kwenye zama ya leo
Ni kweli utatumia madawa ya afya ya akili ila usipokaa chini ukaiwaza leo na kesho yako hizo dawa hazitakusaidia rafiki .
Nakupa mfano kidogo , hivi ungejiskiaje huna baba , mama wala mdogo wako na wote walikufa wakakuacha bad enough walikuacha kwenye mikono ya ndugu walafi na wao wakadai weye si mtoto wao ila ni wa nje ukadhulumika kila kitu na hao ndugu ? Usisahau mtaa ulioachwa wote wanajua wewe ni mwathirika kwakuwa hao ndugu zako walikufa na huo ugonjwa ?
Unapambana unapata kazi kwa kudra zake Allah nako mambo moto mpaka unawekwa lupango?
Unarudi mtaani unaanza moja ndiyo unarudi kazini ila tayari ilmu yako ishachafuliwa na bado unaishi maisha ya kuungaunga maana mshahara bado umezuiliwa ? Si ungejiuwa ndugu ?
Binti uliyezaa naye anakuja kudai watoto si wako unakubali maisha yanendelea hivyo unabaki wewe kama wewe .?
Ndugu matatizo ni mengi na kila mtu ana njia zake za matatizo hivyo simama , pambana usiku na mchana usikubali unyonge wa maisha ukutawale ,usikubali shida zijitangaze kichwani mwako unao uwezo wa kusimama leo yako sio jana mdogo wangu .
Achana na hayo matatizo jitafute vyovyote vile palipo na kiza , nuru inakuja ndugu usijikatae wala usijiumize jua ni wakati wako wa kuonesha uwezo binafsi kimtizamo , kimapambano na mwisho kusshinda .
Tunakupenda hapa jamvini usiondoke bado unahitajika na wengi .