Nahisi siku zangu za kuishi Dunia zinakaribia kuisha, sielewi!

ni kweli nilipo toka si sawa na nilipo...! japo hii sio ndoto yangu... nadhani hichi ndicho kinacho ni maliza siishi maisha ya ndoto zangu...😭😭😭​
Kuna digrii humu.. Kuna watu Wana ndoto za kuonana na Zuckerberg humuhumu... Leo wanauza machungwa mabibo.

Ndoto ziache mkuu, ndoto sio hatma. Plan new destiny, tumia ulicho nacho kikupe vikubwa. Kufeli kwenye maisha kupo! Na amini usiamin kuwa uhai tu peke yake ni hazina.

Habari za ndoto kwa nchi hizi za afrika sio za kuzungumzia. Ni mungu tu akupiganie... Mana hata hao walitusua hawajui mchakato ule ulikuaje! No formula. Wewe ulichonacho kitumie. Kiwanja chako kile Jenga pale fungua duka mpe mkeo auze.
 
"Ninaewatoto watatu na ninawapenda sana" please hao watoto wanakuhitaji sana wewe,ukifanya maamuzi yoyote ni unaacha huzuni kwa hao watoto unaowapenda sana
 
Wewe kaa na kulalama tu. Ndiyo vijana wetu
 
Okoka,
Mpe Yesu maisha Yako, fuatisha Sala ifuatayo;

EE MUNGU KATIKA JINA LA YESU KRISTO, NINAKUKIRI WEWE KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE, NINAOMBA UNISAMEHE, ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU, ULIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA, NIPE UWEZO WA KUISHI MAISHA MATAKATIFU, DHAMBI ISINISHINDE, UOVU USINISHINDE, NINAOMBA HAYO KUPITIA JINA LA YESU KRISTO ALIYE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU. Amen

Baada ya Sala hiyo, Roho mtakatifu ataingia ndani Yako, na utaanza kuyaona maisha katika muono mpya. Hakikisha inasoma BIBLIA Kila mara, ifungue hata sasa soma mstari wowote, utaniambia.

UBARIKIWE πŸ™
 
Na ndo maisha ya watanzania wengi mzee wengi wanapata cha kutumia leo tu kesho itajulikana uko uko,
Mtu anatoka asubuh na nauli tu ya kwenda akirudi ndo watu wale na anafamilia anasomesha na mtu kama huyo ndo kabisaa mbele kiza hana matumanin ya kutoboa na ndo wengi wameangukia ktl betting tumain lao lipo uko wapige mshindo basi,

Ila angalau wewe unakaelimu fulani sikufichi ni vile tu hujatapata unachokipenda kukifanya na ndo ubongo wako umewasha search engine zote kufind what you love na kitakachokusaidia zaid desire ndo inachemka ndani yako mpaka muda mwingine unajihisi kukosa pumzi vizuri
Ata ukilala usingizi hauji utaweweseka tu
 
asante nitajitahidi tuongee hope utanisaidia... nadhani ni mawazo πŸ™ tu ndio yananisumbua...!

historia yangu sio nzuri nina wazazi wote wawili lakini badly nikiwa na miaka 9, 10, 11 nilishawahi kulala nje 😭😭😭

kuna mambo niliwahi kupitia nahisi kwa kiasi fulani yana nichanganya haswa ukizingatia ndoto zangu hakuna hata moja iliyo timia...!

nipo peke yangu kwa mama... now nina zaidi ya miaka 30 licha kuwa ya kupambana sana ila bado maisha yangu yapo mikononi mwa wazazi..!

sina ninacho wasaidia wazazi wangu Zaidi wao ndio wanao nisaidia mimi pamoja na watoto wangu...!

kwakweli nawaza hadi akili inafika mwisho πŸ₯²​
 
kila moja humu JF, na mahala pengine yupo pale alipo kwa Neema na Baraka za Mungu πŸ’

Zawaidi ya uhai, akili, maarifa, afya, nguvu na maisha alizotujaalia Mwenyezi Mungu bure, tuzitumie vizur kwa manufaa yetu binafsi, familia ndungu jamaa na marafiki na sio kutuathiri au kutuhuzunisha πŸ’

Tatizo la Afya ya akili ni pamoja na kufikiri, kuwaza, kujipanga, kuamua na kutenda mambo ambayo yana madhara au yatakayokuathiti wewe mwenywe binafsi lakini pia kuiumiza, kuihuzunisha na kuifedhehesha familia ndugu jamaa na Marafiki πŸ’

Kujiuliza na kujijibu mwenyewe ni chanzo cha kuchukua uamuzi mbaya.
Be free, come out upate relief na mawazo mbadala wa kutoka kwenye hatua hiyo mbaya zaidi ya kukata tamaa πŸ’

By the way,
Mtu mwenye afya,
alie katika hatua za mwisho za uhai wake, anakua smart sana na mwenye bidii sasa katika kukamilisha mipango yake humu duniani. Yuko panctual sana kujifanyia usafi mwenyewe, kula msosi wa kushiba, kunywa, kwenda msalani kupuu, ni muongeaji sana kwaajili ya mipango ya kesho, kumbe hafiki, dah πŸ’

mie naona bado upo hai sana tu kwa Neema na Baraka za Mungu πŸ’
 
hali ni ngumu sana kwakweli 😭😭😭
 
shukrani sana ndugu yangu... πŸ™
 


Hivi kuna kijana amekuja hapa na kusema tayari anajua kijerumani kajitahidi kusoma na hana pesa ya mtihani au ni visingizio kila kitu. Huwezi kulaumu kitu ambacho ujaweka jitihada zozote πŸƒβ€β™‚οΈ. Vijana wenzetu kenya nao wametokea familia masikini lakini hawana lalama kila siku. Mnasubiri mpaka matatizo yanakuwa makubwa ndiyo mnakuja kuomba huruma. Wazee wetu wangekuwa hivi walikulia kwa wakolini wanaondoka kwenye vijiji watoto wao ni sisi wengine tuko Dunia nzima maana walikuwa wanajiendeleza sio kulalama
 
asante sana ndugu yangu πŸ™πŸ™πŸ™
 
kiuchumi siwezi kusema nina tatizo kihivyo kwani nina jishughulisha... japo sina kipato kikubwa cha kumsaidia mwingine ila nina uwezo wa kula milo mitatu...!

kwakweli sielewi kwanini nimewaza hivyo...!​
Hupaswi kuwaza hivyo hata kidogo. Pambana, Songa mbele. Una familia, una mke na watoto watatu wote wanakutizama na kukutegemea. Pambana, Bado kuna mambo makubwa na mazuri mbele
 
Mkuu; wewe unapenda muziki? Yan unasikiliza muziki wa aina gani au kutumia vyombo vya muziki au kuimba ww mwenyewe? Naomba unijibu halafu nitaendelea baada ya jibu lako.
 
nawaza kupauza... mkuu na Tangazo nilishaweka humu humu...kuna member wamenipigia baadhi wameenda kukiona walau naweza kupata ahueni kama wakifika bei... niende kijijini huko nikaanze maisha upya au nijenge nje ya mji huko...!

ila kwasasa hali yangu ni mbaya... kuna mambo siwezi kuyaandika jamii itanicheka😭😭😭​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…