Nahisi tunadanganywa sana kuhusu kiasi cha umeme kunachozalishwa nchini

Wakili wa shetani

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2022
Posts
2,188
Reaction score
4,116
TANESCO wamejificha kwenye kichaka cha uzalishaji wa umeme wa gesi ili kupika data za kiasi cha umeme.

Leo hii mvua zimeanza na hali ya umeme imeboreka sana. Inaonekana umeme wetu mwingi ni wa maji. Upatikanaji wa umeme wetu unabadilika kulingana na uzalishaji wa umeme wa maji. Ule wa gesi wanaosema ni asilimia 65 ya umeme wote ni bosheni tu ili kukuzia data za uzalishaji.

Umeme wa maji wa asilimia 30 haungeweza kuwa na athari kiasi hiki katika upatikanaji wa umeme. Bunge lichunguze hali halisi ya uzalishaji wa umeme nchini. Hizi figures tunapewa na shirika la umeme zina ukakasi ukilinganisha na hali halisi.

images (2).jpeg
 
Tunafichwa ukweli kwa manufaa ya wachache.
Mahitaji ya nchi ni kiasi gani?,uzalishaji wa mitambo ya gesi Kinyerezi I na II,tuliambiwa inaenda kuondoa upungufu wa umeme nchini,lakini imekuwa tofauti.

Mitambo ya gesi ikifunga jenereta ya 240MW,unamaliza kero iliyopo lakini ikasimikwa jenereta ya 80MW.

Makaa ya mawe tunayo,lakini hakuna mkakati wa kutumia makaa ya mawe tumalize upungufu wa umeme.

Kuna siri kubwa,ya kukosekana umeme na mikataba ya Shirika la umeme kuuziwa umeme kutoka makampuni binafsi.
 
Umeme unaozalishwa bongo ni mdogo sana no more no less. Hawa kila siku wanajificha kwenye ukame, mvua ikija wanahamisha magoli mambo yale yale.

Tulisema wizara ya nishati ni jumba bovu hata apewe nani litamuangukia tu. Biteko hii wizara itamtoa mchezoni kabisa wakati angebaki kwenye madini angekua na nafasi ya kuja kuwa full PM kama sio Rais kabisa.
 
TANESCO wamejificha kwenye kichaka cha uzalishaji wa umeme wa gesi ili kupika data za kiasi cha umeme.

Leo hii mvua zimeanza na hali ya umeme imeboreka sana. Inaonekana umeme wetu mwingi ni wa maji. Upatikanaji wa umeme wetu unabadilika kulingana na uzalishaji wa umeme wa maji. Ule wa gesi wanaosema ni asilimia 65 ya umeme wote ni bosheni tu ili kukuzia data za uzalishaji.

Umeme wa maji wa asilimia 30 haungeweza kuwa na athari kiasi hiki katika upatikanaji wa umeme. Bunge lichunguze hali halisi ya uzalishaji wa umeme nchini. Hizi figures tunapewa na shirika la umeme zina ukakasi ukilinganisha na hali halisi.

View attachment 2836587
Wapi wamepunguza kukata umeme wakati huku jana na leo umeme hamna
 
Umeme unaozalishwa bongo ni mdogo sana no more no less. Hawa kila siku wanajificha kwenye ukame, mvua ikija wanahamisha magoli mambo yale yale.

Tulisema wizara ya nishati ni jumba bovu hata apewe nani litamuangukia tu. Biteko hii wizara itamtoa mchezoni kabisa wakati angebaki kwenye madini angekua na nafasi ya kuja kuwa full PM kama sio Rais kabisa.
Wanasema tuna installed capacity ya 1800 MW. Unaweza kuta hata 1000 hatufiki. Nadhani tunadanganywa sana kuhusu uzalishaji wa umeme wa gesi.
 
Kama wanatudanganya basi hawafai kuwa madarakani.

WAONGO NI WATU WABAYA KWA TAIFA

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Umeme unaozalishwa bongo ni mdogo sana no more no less. Hawa kila siku wanajificha kwenye ukame, mvua ikija wanahamisha magoli mambo yale yale.

Tulisema wizara ya nishati ni jumba bovu hata apewe nani litamuangukia tu. Biteko hii wizara itamtoa mchezoni kabisa wakati angebaki kwenye madini angekua na nafasi ya kuja kuwa full PM kama sio Rais kabisa.
Loh! Biteko awe PM! Watu mnajidanganya kweli.
 
TANESCO wamejificha kwenye kichaka cha uzalishaji wa umeme wa gesi ili kupika data za kiasi cha umeme.

Leo hii mvua zimeanza na hali ya umeme imeboreka sana. Inaonekana umeme wetu mwingi ni wa maji. Upatikanaji wa umeme wetu unabadilika kulingana na uzalishaji wa umeme wa maji. Ule wa gesi wanaosema ni asilimia 65 ya umeme wote ni bosheni tu ili kukuzia data za uzalishaji.

Umeme wa maji wa asilimia 30 haungeweza kuwa na athari kiasi hiki katika upatikanaji wa umeme. Bunge lichunguze hali halisi ya uzalishaji wa umeme nchini. Hizi figures tunapewa na shirika la umeme zina ukakasi ukilinganisha na hali halisi.

View attachment 2836587

Nunua solar, karne hii huwezi kukaa giza kusubiri umeme wa mgao. Hata baadhi ya viwanda vinaendeshwa kwa umeme wa solar!
 
Maharage alisema Hata bwawa la Nyerere likikamilika, bei ya umeme haitashuka itabaki hihi
 
TANESCO wamejificha kwenye kichaka cha uzalishaji wa umeme wa gesi ili kupika data za kiasi cha umeme.

Leo hii mvua zimeanza na hali ya umeme imeboreka sana. Inaonekana umeme wetu mwingi ni wa maji. Upatikanaji wa umeme wetu unabadilika kulingana na uzalishaji wa umeme wa maji. Ule wa gesi wanaosema ni asilimia 65 ya umeme wote ni bosheni tu ili kukuzia data za uzalishaji.

Umeme wa maji wa asilimia 30 haungeweza kuwa na athari kiasi hiki katika upatikanaji wa umeme. Bunge lichunguze hali halisi ya uzalishaji wa umeme nchini. Hizi figures tunapewa na shirika la umeme zina ukakasi ukilinganisha na hali halisi.

View attachment 2836587
Yule Rais wenu mkweli hawakuwahi kuwaambia?
 
Mbona walifunga biashara zamani hawa na wakauza kama chuma chakavu?
Sijui kwanini wanafanya hivi
Yaani watu wanaiba Transforma
1000022350.png
 
Back
Top Bottom