Nahisi wanaokunywa pombe wana furaha zaidi kuliko wanywa soda, juisi na ukwaju

Nahisi wanaokunywa pombe wana furaha zaidi kuliko wanywa soda, juisi na ukwaju

Hiyo mistari miwili ya mwisho nilimanisha hivyo mkuu! Ule utajiri ambao una emergence savings za maana na hela ya kula isikupgie chenga na uishi pazuri basi!..yaan ule utajiri ukitaka kwenda kesho German uende..yan kila unalotaka linakuwa ndani ya uwezo wako
Hapana mkuu Wangari, sio wote wenye hela wanafuraha.. ..wengi wao wanaishi kwa hofu anytime wanahofia watachomoka na kuiacha mali.. ..wengine hupatwa na maradhi makubwa na ndio yanawafanya wakose furaha.. ..wengine madeni yamewajaa mpaka inafikia mahali wanajiuwa.. ..wengine wamepata utajiri kwa njia isiyo ya halali,.. ..Ni heri upate utajiri wa kawaida tena kwa njia ya halali, hapo utaishi maisha ya amani na furaha.. ..
 
Walevi tunaishi nao humu humu na tunawajua mishe mishe zao.

Kwanza siku hizi pesa imekuwa ngumu ndio maana wanakunywa SPIRITS ( Konyagi, Kvant, Double Kick ) ili walewe mapema. Pesa ya kulewa bia tupu hawana.

Wakifulia wanakula Ugoro wa Wamasai[emoji1787]
Hehehe [emoji16][emoji16][emoji1787]

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu kitimoto ni mdau, maana nilibaini wanaokunywa kitimoto hata wivu hawana wa kizembe kizembe,,hivyo inaongeza kuishi kwa furaha.
Mi kitimoto na kawine aah ...asee nina mafuraha mpaka natamani kuwageia nyie wenye stress

Sasa kama hutumii hivi vitu viwili we ulikuja duniani kufanya nini? Kushangaa magorofa??[emoji849]

Aku! Mi siyawezi hayo maisha

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Mi kitimoto na kawine aah ...asee nina mafuraha mpaka natamani kuwageia nyie wenye stress

Sasa kama hutumii hivi vitu viwili we ulikuja duniani kufanya nini? Kushangaa magorofa??[emoji849]

Aku! Mi siyawezi hayo maisha

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Ha ha ha ha wanaokula kitimoto ni maisha ya furuha sana ni miongoni mwa nyama tamuuuiuuuuu sana.

Nikipita eneo nikasikia ile harufu yake na mapigo ya moyo yanabadilika natamani nipite hatakama sikuwa na nia hiyo muda huo.
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji38]
 
Huu uzi ukisoma maoni ya wasiokunywa pombe na jinsi wanavyoijengea negative state nabaki kucheka kitu
Kitu hutumii unajuaje kuwa ni kibaya? Mifano ya marafiki wachache wasiojitambua wanaopelekeshwa na pombe si kigezo cha kusema pombe ni kitu kibaya hivyo
Nina miaka 33 kwenye tungi tena asilimia 90 nakula kali tupu lakini sijawahi kuharibu popote na maisha yangu yanasonga
 
Walevi huwa wanajidanganya eti ili upoteze mawazo unywe pombe.. ..ujinga mtupu..hakuna kitu kama hicho.. ..ukilewa ndio mawazo yanazidi na kupelekea kufanya upumbavu hata kummbaka mzazi/dada yako
Kwahyo wote wanaobaka, wanaorawiti ni wanywa pombe???
 
Huu uzi ukisoma maoni ya wasiokunywa pombe na jinsi wanavyoijengea negative state nabaki kucheka kitu
Kitu hutumii unajuaje kuwa ni kibaya? Mifano ya marafiki wachache wasiojitambua wanaopelekeshwa na pombe si kigezo cha kusema pombe ni kitu kibaya hivyo
Nina miaka 33 kwenye tungi tena asilimia 90 nakula kali tupu lakini sijawahi kuharibu popote na maisha yangu yanasonga
Yaani watu wanavyoiandama pombe utafikiri watenda maovu wote ni wale wanaokunywa pombe tu.

Hawajui kuwa wanywa pombe wanamichongo mingi sana, kupeana madili ya mafanikio ila sio kukupa hela hahaaa[emoji23][emoji23][emoji23] uzuri zaidi wanywaji hawana majungu . nenda sasa kwa wasio kunywa majungu kila leo unakuta mtu kaagiza fanta tangu saa saba mpaka saa kumi na mbili ana kifanta kimoja tu na hakiishi muda wote kuzungumzia watu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Connection nyingi
Marafiki wengi
Kulifahamu jiji na maeneo yake yote
Kujifunza mambo mapya
 
Chochote kile alichokiharamisha Mwenyezi Mungu kina madhara, sio tu kiafya na hata kuporomoka kiuchumia pia n.k. Nyumba zinakua hazina amani, rizki wala furaha n.k, najua watumiaji mtakuja kunipinga, lakini ukweli ndio huu.

40. VINYWAJI VINAVYOLEWESHA (POMBE) NA TOGWA.​

Written by Sh. Hafidh Al-Sawafi

624. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zayd, kutoka kwa Ibn Abbas (R.A.A.) kasema, "Mtu mmoja alimpa zawadi Mtume (S.A.W.) viriba viwili vyenye mvinyo akamwambia, “
«أَمَا عَلِمْتَ أَنَّ اللَّهَ حَرَّمَهَا»
Maana yake, “Jee, hujui kwamba Allah ameharamisha?” Akasema, "Sijui,” akamnong`oneza mtu kwa siri, Mtume (S.A.W.) akamwambia, "
«بِمَ سَارَرْتَهُ»؟
Maana yake, “Jee, umemnong`oneza kitu gani kwa siri?” Akasema, "Nimemwamrisha akauze." Mtume (S.A.W.) akamwambia, "

«إِنَّ الذِي حَرَّمَ شُرْبَهَا حَرَّمَ بَيْعَهَا»
Maana yake, “Hakika Ambaye ameharamisha kuunywa, ameharamisha uuzaji wake”.
625. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zayd, kutoka kwa Ibn Abbas (R.A.A.) kasema, "Mtume (S.A.W.) kasema, "
«لَعَنَ اللَّهُ الْخَمْرَ وَبَائِعَهَا وَمُشْتَرِيَهَا وَعَاصِرَهَا وَحَامِلَهَا وَالْمَحْمُولَةَ إِلَيْهِ وَشَارِبَهَا».
Maana yake, “Allah ameulani ulevi, na mwuzaji, na mnunuzi, na mkamuaji, na mbebaji na anaye pelekewa, na mnywaji”.

626. A-Rrabi`i kutoka kwa Ubaada bin Ssaamit kasema, "Mtume (S.A.W.) kasema, "
«لَيَسْتَحِلَّنَّ آخِرُ أُمَّتِي الْخَمْرَ بِأَسْمَاءٍ يُسَمُّونَهَا بِهَا».
Maana yake, “Watauhalalisha ulevi umma wangu wa mwisho kwa majina watakayouitia”.

627. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zayd, kutoka kwa Abu Said L-Khudriyyi (R.A.A.) kasema, "Mtume (S.A.W.) kasema, "
«مَنْ شَرِبَ الْخَمْرَ فِي الدُّنْيَا ثُمَّ لَمْ يَتُبْ مِنْهَا حُرِمَهَا فِي الآخِرَةِ».
Maana yake, “Atakaeunywa ulevi duniani kisha hakutubu ataharamishiwa Akhera”.

628. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Anas bin Maalik (R.A.A.) kasema, "Siku moja nilikuwa nikimnywesha Abu Dujaana, na Abu Talha, na Ubayyi bin Ka`ab, kinywaji kilichotokana na mchanganyiko wa tende mbichi na zilizoiva, mara akaja mtu mmoja akasema, “Ulevi umekwisha haramishwa!” Abu Talha akasema, "Ewe Anas! Nenda ukakivunje hiki chombo”. Anas akasema, "Nikachukua jiwe letu la kusagia, na nikakivunja kuanzia chini mpaka kikavunjika chote”.

629. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Aisha (R.A.A.H) kasema, "Mtume (S.A.W.) aliulizwa kuhusu ulevi unaotengenezwa kutokana na asali akasema, "
«كُلُّ شَرَابٍ أَسْكَرَ فَهُوَ حَرَامٌ».
Maana yake, “Kila kinywaji kinacholevya ni haramu”.

630. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Abu Said L-Khudriyyi (R.A.A.) kasema,
«نَهَى أَنْ يُشْرَبَ التَّمْرُ وَالزَّبِيبُ جَمِيعًا، وَكَذَلِكَ كُلُّ خَلِيطَيْنِ».
Maana yake, "Mtume (S.A.W.) amekataza kinywaji cha mchanganyiko wa tende na zabibu, na pia kila chenye michanganyiko ya aina mbili”.
A-Rrabi`i kasema, "Abu Ubayda kasema, "Endapo kimechachuka (kuwa kilevi), na kuharibika, lakini ikiwa kinyume na hivyo basi haina neno”.

631. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Abu Said L-Khudriyyi (R.A.A.) kasema,
«نَهَى أَنْ يُنْبَذَ فِي الدُّبَّاءِ وَالْمُزَفَّتِ وَالنَّقِيرِ وَالْحَنْتَمِ».
Maana yake, “"Mtume (S.A.W.) amekataza kufanya nabidh (aina ya siki) katika kibuyu, na chombo kilichopakwa lami, na chombo kilichotengenezwa kutokana na gogo la mti, na chombo cha udongo”. (Sababu yake ni kwamba ikiwa vitatumiwa vyombo hivyo kutengenezea itapelekea kuchachuka kwa kinywaji hicho kwa haraka na kuwa ulevi).

632. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kasema, "Hadithi iliyopokelewa na Abdallah bin Masoud (R.A.A.) ya usiku wa Majini, Mtume (S.A.W.) kumruhusu kutawadha kwa maji ya mchanganyiko wa maji ya zabibu, na tende imetajwa katika…." Hadithi imetajwa katika Mlango wa Udhu
 
Back
Top Bottom