Chochote kile alichokiharamisha Mwenyezi Mungu kina madhara, sio tu kiafya na hata kuporomoka kiuchumia pia n.k. Nyumba zinakua hazina amani, rizki wala furaha n.k, najua watumiaji mtakuja kunipinga, lakini ukweli ndio huu.
40. VINYWAJI VINAVYOLEWESHA (POMBE) NA TOGWA.
Written by
Sh. Hafidh Al-Sawafi
624. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zayd, kutoka kwa Ibn Abbas (R.A.A.) kasema, "Mtu mmoja alimpa zawadi Mtume (S.A.W.) viriba viwili vyenye mvinyo akamwambia, “
«أَمَا عَلِمْتَ أَنَّ اللَّهَ حَرَّمَهَا»
Maana yake, “Jee, hujui kwamba Allah ameharamisha?” Akasema, "Sijui,” akamnong`oneza mtu kwa siri, Mtume (S.A.W.) akamwambia, "
«بِمَ سَارَرْتَهُ»؟
Maana yake, “Jee, umemnong`oneza kitu gani kwa siri?” Akasema, "Nimemwamrisha akauze." Mtume (S.A.W.) akamwambia, "
«إِنَّ الذِي حَرَّمَ شُرْبَهَا حَرَّمَ بَيْعَهَا»
Maana yake, “Hakika Ambaye ameharamisha kuunywa, ameharamisha uuzaji wake”.
625. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zayd, kutoka kwa Ibn Abbas (R.A.A.) kasema, "Mtume (S.A.W.) kasema, "
«لَعَنَ اللَّهُ الْخَمْرَ وَبَائِعَهَا وَمُشْتَرِيَهَا وَعَاصِرَهَا وَحَامِلَهَا وَالْمَحْمُولَةَ إِلَيْهِ وَشَارِبَهَا».
Maana yake, “Allah ameulani ulevi, na mwuzaji, na mnunuzi, na mkamuaji, na mbebaji na anaye pelekewa, na mnywaji”.
626. A-Rrabi`i kutoka kwa Ubaada bin Ssaamit kasema, "Mtume (S.A.W.) kasema, "
«لَيَسْتَحِلَّنَّ آخِرُ أُمَّتِي الْخَمْرَ بِأَسْمَاءٍ يُسَمُّونَهَا بِهَا».
Maana yake, “Watauhalalisha ulevi umma wangu wa mwisho kwa majina watakayouitia”.
627. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zayd, kutoka kwa Abu Said L-Khudriyyi (R.A.A.) kasema, "Mtume (S.A.W.) kasema, "
«مَنْ شَرِبَ الْخَمْرَ فِي الدُّنْيَا ثُمَّ لَمْ يَتُبْ مِنْهَا حُرِمَهَا فِي الآخِرَةِ».
Maana yake, “Atakaeunywa ulevi duniani kisha hakutubu ataharamishiwa Akhera”.
628. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Anas bin Maalik (R.A.A.) kasema, "Siku moja nilikuwa nikimnywesha Abu Dujaana, na Abu Talha, na Ubayyi bin Ka`ab, kinywaji kilichotokana na mchanganyiko wa tende mbichi na zilizoiva, mara akaja mtu mmoja akasema, “Ulevi umekwisha haramishwa!” Abu Talha akasema, "Ewe Anas! Nenda ukakivunje hiki chombo”. Anas akasema, "Nikachukua jiwe letu la kusagia, na nikakivunja kuanzia chini mpaka kikavunjika chote”.
629. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Aisha (R.A.A.H) kasema, "Mtume (S.A.W.) aliulizwa kuhusu ulevi unaotengenezwa kutokana na asali akasema, "
«كُلُّ شَرَابٍ أَسْكَرَ فَهُوَ حَرَامٌ».
Maana yake, “Kila kinywaji kinacholevya ni haramu”.
630. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Abu Said L-Khudriyyi (R.A.A.) kasema,
«نَهَى أَنْ يُشْرَبَ التَّمْرُ وَالزَّبِيبُ جَمِيعًا، وَكَذَلِكَ كُلُّ خَلِيطَيْنِ».
Maana yake, "Mtume (S.A.W.) amekataza kinywaji cha mchanganyiko wa tende na zabibu, na pia kila chenye michanganyiko ya aina mbili”.
A-Rrabi`i kasema, "Abu Ubayda kasema, "Endapo kimechachuka (kuwa kilevi), na kuharibika, lakini ikiwa kinyume na hivyo basi haina neno”.
631. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kutoka kwa Abu Said L-Khudriyyi (R.A.A.) kasema,
«نَهَى أَنْ يُنْبَذَ فِي الدُّبَّاءِ وَالْمُزَفَّتِ وَالنَّقِيرِ وَالْحَنْتَمِ».
Maana yake, “"Mtume (S.A.W.) amekataza kufanya nabidh (aina ya siki) katika kibuyu, na chombo kilichopakwa lami, na chombo kilichotengenezwa kutokana na gogo la mti, na chombo cha udongo”. (Sababu yake ni kwamba ikiwa vitatumiwa vyombo hivyo kutengenezea itapelekea kuchachuka kwa kinywaji hicho kwa haraka na kuwa ulevi).
632. Abu Ubayda, kutoka kwa Jaabir bin Zaid, kasema, "Hadithi iliyopokelewa na Abdallah bin Masoud (R.A.A.) ya usiku wa Majini, Mtume (S.A.W.) kumruhusu kutawadha kwa maji ya mchanganyiko wa maji ya zabibu, na tende imetajwa katika…." Hadithi imetajwa katika Mlango wa Udhu