Nahisi wanaokunywa pombe wana furaha zaidi kuliko wanywa soda, juisi na ukwaju

Nahisi wanaokunywa pombe wana furaha zaidi kuliko wanywa soda, juisi na ukwaju

Mkuu issue ya madeni na maisha magumu si kwa wanywa pombe tu, pia wewe umegeneralize wote.

Kuna kundi la watu walevi ambao hawa maisha yao yote ni pombe, matapu tapu,gongo hana ramani ya maisha, maisha hayaeleweki kundi hili halifai na limeshapoteza ramani ya maisha.

KUNA KUNDI LA WANYWAJI.

Kundi hili ni watu smart sana, wenye kipato ambao hawanywi pombe kuondoa mawazo, hawa wanakunywa kwa hesabu, na ni watu makini sana, wana maendeleo mazuri hata akinywa anakuwa na kiasi, anabaki anajitambua na yuko smart siyo cha pombe .

Kundi hili linatawala pombe, pombe haiwatawalii wao.

Hili ndiyo kundi linaloenjoy maisha.

Walevi Wana furaha ya muda mfupi na huzuni ya muda mrefu ninaishi nao na ninawaona

Nimefanya utafit walevi wengi ni watu wenye madeni kibao na Ni watu wanaopoteza uaminifu kwa haraka zaidi mlevi akiaminiwa hufanya hiyana.
Na hata unae muamin anaweza akakufanyia tukio badae kisingizio kikawa ni pombe
 
Sorry but huu utafiti ni butu
 
Tofautisha mnywaji na mlevi.. Mnywaji ni mtu anayekunywa na anajitambua,. Mlevi ni mtu ambaye maisha yake ni pombe tu,.
Ulevi ni addiction.

Hata walevi walianza kama wanywaji mpaka pake alcohol ilipokolea kwenye damu. Alcohol ikikolea kwenye damu ndio inayopelekea ulevi, usipokunywa tu unakuwa na arosto kali sana, kuipoza mpaka unywe tena.

Maisha ya Pombe yako katika stages.

1- Kama ndio unaanza, hapa hata bia zinakuwa za kuchagua. Utasikia usinywe Castle, jifunzie kwenye Serengeti Lite.

2- Stage 2, utakuwa unalewa hata bia 2 tena zenye kileo kidogo.

3- Ukiwa chronic hapa hata bia hulewi. Ili ulewe inakubidi kwenye bia uchanganye na Konyagi, K-Vant, Double kick n.k

4- Ukishafika stage ya kulewa mpaka unywe Spirits, maana yake hapo ushakuwa mlevi kamili. Hupitishi siku bila pombe. Ukinywa usiku, asubuhi unaamka na hang over dawa yake unaona ni kuzimua kwa kunywa tena konyagi.

5- Stage mbaya zaidi ni ukikosa hela: Hapa unageuka omba omba wa bia, kama ni mwanamke unaanza kumegwa kwasababu ya pombe. Ukipata buku 10, unakimbilia Konyagi za kupima, kupoza arosto.

Ukikosa pesa mpaka UGORO wa kimasai unakuhusu.

Pombe haijawahi kuwa kitu cha maana hata kidogo. Useless.
 
Asilimia 90% ya watu wenye pesa wanakunywa pombe, ndiyo matajiri pia hapa mjini, anaposema kundi hili ni watu wa shida hajafatilia vizuri.

Pia atofautishe kati ya walevi wa kupindukia na wanaokunywa na wanaojitambua vzr.

Wasomi, matajiri, hawa wote wanakunywa na wanajitambua hata marais pia ni kundi wanaokunywa sasa akisema ni watu wa dhiki na shida.
Hajuwi ukubwa wa kundi hili na nguvu yao.

Wanywa pombe ndio walipa kodi nambari moja nchini na duniani kote
 
Walevi tunaishi nao humu humu na tunawajua mishe mishe zao.

Kwanza siku hizi pesa imekuwa ngumu ndio maana wanakunywa SPIRITS ( Konyagi, Kvant ) ili walewe mapema. Pesa ya kulewa bia tupu hawana.

Wakifulia wanakula Ugoro wa Wamasai🤣
Hawa wanachekesha kweli. Rafiki zangu wengi wanakunywa ila wote wanatamani kuacha ila hawawezi. Wanatamani wawe kama mimi nakaa nao bar hadi saa mbaya na sinywi akija mgeni anaweza kujua Mimi ndio nimekunywa pombe nyingi.
Kuna uzi humu wa majuto ya walevi asubuhi hawa wanaosifia leo kule wanatamani kuacha ILA hawawezi. No self control!
 
Hawa wanachekesha kweli. Rafiki zangu wengi wanakunywa ila wote wanatamani kuacha ila hawawezi. Wanatamani wawe kama mimi balaa nao bar hadi saa mbaya na sinywi akija mgeni anaweza kujua Mimi ndio nimekunywa pombe nyingi.
Kuna uzi humu wa majuto ya walevi asubuhi hawa wanaosifia leo kule wanatamani kuacha ILA hawawezi. No self control!
Walevi wote wanatamani kuacha ila ADDICTION haiachwi kirahisi, ndio maana suluhisho walilonalo ni kupeana moyo kama hivi na kushawishi watu wengine waingie huko ili wawe kama wao.

Wanaanzisha mpaka vita , ooh mnaokunywa soda sijui nini. Mara msiokunywa pombe ni malaya.

Wakati walevi tunawajua walivyo mabingwa wa kuokota ma-barmaid wakishalewa huko Bar. Yaani Bar isiyo na mademu haipati wateja 🤣

Mimi niko 31yrs, pombe haijawahi kugusa mdomo wangu na sijihisi kama kuna kitu chochote Na-MISS.
 
Kuna ndugu yangu mmoja tulikutana kijijini kwetu,bas ckuhiyo akawa amejifunza kunywa pombe aliporudi home akawa analia kwa uchungu sana kitendo hicho kilifanya familia kupatwa na hofu kuuu,majirani tukasogea watu wakaanza kumuuliza unalia nn? Jamaa kasema ningekua na hela ningewajengea nyumba kubwa sana wazazi wangu,watu haaaa hilo tu ndo unalia jamaa.
 
Walevi tunaishi nao humu humu na tunawajua mishe mishe zao.

Kwanza siku hizi pesa imekuwa ngumu ndio maana wanakunywa SPIRITS ( Konyagi, Kvant ) ili walewe mapema. Pesa ya kulewa bia tupu hawana.

Wakifulia wanakula Ugoro wa Wamasai🤣
Hahahaa mkuu bia zinanenepesha... tunakuntwa spirits tuendee kudamshi..tusiwe na mavitambi yaleee😜😜!...tunaambiwa spirits zinakata wese mwilini...haha sema pombe isikuendeshe .ikikuendesha you are finished😪
 
Spirits zinapausha mwili. Ukimuona mtu ngozi imepaukaa utafikiri kalala jikoni kwenye majivu.

Hasa hasa lishe ikiwa duni. Spirits zinaendana na lishe.
 
Back
Top Bottom