Aah, sasa hiyo mbona sawa tu na gari kama Rav 4 engine code 1AZ, 1ZZ na 2AZ? 1ZZ iko kwenye Kill time Rav 4, Voltz, Premio kutaja baadhi.
Kadri nijuavyo kama mtu anaweza kuendesha RAV 4, Kluger, Harrier za kuanzia 5S, 2AZ Ambazo zote ni 4 cylinder zenye cc 2400, hawezi kushindwa 6 Cylinder hizi za kisasa ambazo zina CC 2500.
Nadharia hapa ni kuwa kuna mtu anajaza tank lake la maji kwa pipe 4 kubwa(boreholes) na mwingine anajaza tank lake lenye ujazo unaoelekea kufanana CC2500 vs 2400 kwa kutumia pipe ndogo 6, tofauti hapo ni kama hamna na kwa kutumia advanced technology yaani usaidizi wa mifumo iliyoboreshwa ya umeme wa gari, utakuta ulaji wa mafuta ni mdogo tu.