Nahitaji kujifunza Martial Art

Yes, mafunzo yanaanzia hapa hapa Bongo, binafsi nilijikuta tu naambiwa kwamba ninafaa kulingana na wepesi wangu wa kimwili na uelewa, walianza kunisoma kwanza kisaikolojia (jamaa sometimes wanatumia uchawi)
Nilichukuliwa mpaka Finger Prints na waliniscan, yaani hayo makolo kolo tu unayofanyiwa mwanzoni unajikuta unaanza kuogopa, sema kilichowafurahisha mimi nilikuwa siogopi kitu mpaka sasa siogopi kitu, pia nilikuwa na tabia ya kuuliza kitu mara mbili mbili ili niwe nafanya kwa uhakika
Hivyo hata kabla sijaanza rasmi niliuliza mavipimo yote haya ya nini? Ndo nikajibiwa, 'ili yakitokea mauaji yoyote yale ya utatanishi wa kwanza kufuatiliwa ni sisi", maana siraha yako kubwa ni mwili wako
 
Pia niliambiwa kabisa, unaweza ukawa unapigana na mtu uraiani (tulikuwa tukifundishwa na boksa kidogo ili kubalance mambo yanapozidi) wewe ukawa unafanya kama utani hivi ila mwenzio akataka kushambulia eneo hatarishi bila ya yeye mwenyewe kujua hivyo ikapelekea wewe kupanick na kujikuta unafanya kweli

Mimi walikuwa wakinifundisha Karate Kombat (ambayo inaanzia hapa Bongo), wakawa wanaichanganyia na Taekwondo ila nikawa naipenda na kuielewa zaidi Karate Kombat kuliko TaeKwondo, hivyo ikabidi waache kunifundisha TaeKwondo wakabaki na Karate Kombat kisha wakaniongezea Boxer kama mchezo wa kufanyia utani

Mnapewa option ya mchezo wa ziada ili hata ikitokea ulazima wa kupigana basi utumie hiyo ziada, mimi nilichagua Boxer japo siendani nayo maana nina mwili mdogo ila nilikuwa shabiki mkubwa wa Mike Tyson

Kiufupi mafunzo ni mengi sana, yakiwemo namna ya kudhibiti hasira, kuishi na watu uraiani, kujizuia tamaa za kimwili, yaani mambo ni mengi mno

Hapa Dar nafahamiana na baadhi ya walimu wa Karate ila sijui wanafundishia wapi maana mmoja najua ni mwalimu wa Al Hikma mwingine huwa nakutana nae siku moja moja Town akitoka kufundisha Karate (Sho-to-kan) (sijui ndo wanavyoita maana kwenye Kombat tuna Sho-To-Uke) sema zaidi ya salamu sina story nae
 
Hakika Sanaa hiyo imejumuisha mambo mengi Sana ambayo ngumu mno kuyakuta katika arts ambazo civilian anakuwa trained nazo. Humo ni mwendo wa combination na physical training za maana. Binafsi Tae kwon do sipo interested nayo kivile Kama Muay Boran..
 
Mi nilianza boxing nikiwa mdogo sana ndo ya kwanza kujifunza hata sasa hivi kwenye rings naingia lkn yakutoana mafua sio ya kulipwa kuna miaka nilikuwa nafaika pale amana dar then hayo mengine yakafuata
 
Mkuu ulijifunza lini maana ule uzi wako wa panya road ulisema ulitetemekaπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜‚
 
mbona kama na wewe una dojo lako mkuuπŸ€” au ndo siwezi jibiwa mpaka PM?
 
Yes, upo sahihi, mpaka sasa najivunia kitu kimoja tu, nikiingia anga za wenyewe nasikilizwa sijui bado wana info zangu,
Naamua kuishi maisha ya kawaida sana lakini kuna muda nalazimika kuzima simu
ulijifunzia wapi kombat mtaalam inaonekana kali sana hiyo
 
Yap! Kravmaga! No comment
 
Changanya michezo ya mapigano utanishukuru. Usijikite kwenye mchezo mmoja tu labda iwe Shaolin (Sio Shaolinj).

Nimeanza kujifunza boxing.

Nilipitia karate kiasi. Nikapitia Muaithai kiasi (kiupande wangu hawa majamaa wana mazoezi magumu sana). Sasa najifunza boxing.

Ukiwa unapasha mwenyewe kuna mapigo unachanganya unakuwa unayabuni mwenyewe.

Nimeamua kuchanganya baada ya kuona wale vichaa wa MMA wanavyopigana. MMA mafunzo yao yamechanganya michezo ya aina tofauti.

Cha muhimu zaidi uwe mvumilivu wa mazoezi.

Mae geri Squat/ Squatting Geri. Siku ya kwanza nimepigishwa 100 kwa 100 zote. Nyama za nyuma ya mapaja ziliuma vibaya mno. Ukitembea unasikia kabisa miguu inaita. Ukiamka asubuhi kama haujapiga angalau squats kidogo utatembea kama una mshipa. Kwenye long call utapata tabu kidogo ile ishu ya kuchuchumaa ila mwili ndiyo unajengeka ukiwa mvumilivu.
 
Unajua nini, wengi wanahofia watoto watakua na tabia mbaya, lakini mtoto ukimpeleka kwenye Dojo iliyosajiriwa awezi kuharibika, sana sana kule ndo atanyooka maana kunakuwa kama shule, unalipa ada na michango midogo midogo ya mikanda
😍
 
Dojo kali ilikuwepo upanga zanaki
Unakutana na kina sensei mawala
Etc
Dojo nyingi sahv blhblh tu

Ova
 
Safi Sana,
 
Kuna watu wakiona mtu ana uwezo mkubwa kimapigano wanadhani ile imetokea tu kwa mazoezi haya ya kawaida yanoyoonekana machoni pa wengi. Kuna maumivu utakutana nayo utatamani roho ichomoke upumzike.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…