Malaika wa Kifo
JF-Expert Member
- Apr 11, 2012
- 4,052
- 4,621
Hatujuani mkuu, pia hujui mimi ni nani zaidi ya fake ID, Hujui maisha niliyopitia, hujui kazi yangu asili ni nini, hujui mpaka sasa nna 35+ nimepitia harakati zipi za maisha, hujui nimenusurika mara ngapi kufaAcha kumdanganya mwenzio mkuu, kwamba wewe unaweza kushinda kwa Kila pambano hapa chini ya jua, Nina wasiwasi na sehemu ulipochukua hiyo Kombat yako.
Kifupi mimi ni cha mtoto bado nahitaji kujifunza, nikikwambia wasifu wa walionifundisha mimi ndo utajua kwamba mimi ni cha mtoto
Pia sijasema kwamba kila pambano nitashinda, ila asili ya kombat ni kuua, kusababisha kilema cha maisha na kuvunja
Na yenyewe haihitaji pumzi sababu haipo kwa ajili ya mashindano ipo kwa ajili ya kujilinda na adui pia unaambiwa kabisa, "KOMBAT HAINA MAJARIBIO".
Sababu yenyewe inahusisha kupiga maeneo hatarishi
Yapo mengi ningeweza kuandika hapa, kifupi nilianza kufundishwa nikiwa nna 19yrs mpaka nafikisha 28yrs, wakati naanza nilikua napenda sana ugomvi ila baadae nikaanza kuogopa nikiona sehemu ina dalili ya ugomvi natafuta njia mapema
Ni sanaa nzuri ya kujilinda ila ukitaka uinjoi usiwe mkorofi, pia hata kama unapenda ugomvi ila kule unaandaliwa kisaikolojia hata kama wewe ni mtukutu ukitoka kule unabadilika sana kitabia
Kifupi unafundishwa mambo mengi sana
Ila sasa natafuta mwalimu wa Kravmaga