Changanya michezo ya mapigano utanishukuru. Usijikite kwenye mchezo mmoja tu labda iwe Shaolin (Sio Shaolinj).
Nimeanza kujifunza boxing.
Nilipitia karate kiasi. Nikapitia Muaithai kiasi (kiupande wangu hawa majamaa wana mazoezi magumu sana). Sasa najifunza boxing.
Ukiwa unapasha mwenyewe kuna mapigo unachanganya unakuwa unayabuni mwenyewe.
Nimeamua kuchanganya baada ya kuona wale vichaa wa MMA wanavyopigana. MMA mafunzo yao yamechanganya michezo ya aina tofauti.
Cha muhimu zaidi uwe mvumilivu wa mazoezi.
Mae geri Squat/ Squatting Geri. Siku ya kwanza nimepigishwa 100 kwa 100 zote. Nyama za nyuma ya mapaja ziliuma vibaya mno. Ukitembea unasikia kabisa miguu inaita. Ukiamka asubuhi kama haujapiga angalau squats kidogo utatembea kama una mshipa. Kwenye long call utapata tabu kidogo ile ishu ya kuchuchumaa ila mwili ndiyo unajengeka ukiwa mvumilivu.