Nahitaji kujifunza Martial Art

Nahitaji kujifunza Martial Art

Hii kitu inaua sana nguvu za miguu!

Ashakum si matusi! Sijawahi kufanya mapenzi ila kuna siku niliingiwa na mdudu gani sijui (astaghfirullah) nikajichua halafu jioni nikaenda tizi! Miguu haikuwa na nguvu na inawahi kuchoka.
Kwahiyo sisi tuliooa hatuna chetu hapa ama vipi mkuu?
 
Ahh wapi Mzee!

Huwa sisumbui wanawake ila wao ndiyo wananisumbua. Muonekano wangu una taswira ya mtoto wa mama/bi shoo na wengine wamefika mbali na kudai Hammaz ni HB. Nasumbuliwa na allergy kibao! Tumbo langu kula vyakula vya mtaani haliwezi ni kila tu naendesha. Hivyo nina aina ya vyakula vyangu ninavyokula.

Mazingira hayo wakati nasoma yalinifanya nionekane wa kishua na muonekano wangu daaah ulinigharimu! Ukizingatia huwa sina habari na mambo yasiyonihusu ilikuwa ni balaa! na mapigo yangu yalikuwa ni ya ki-hip hop kisa mimi mweupe wanapagawa kabisa.

Hapo sasa wanawake ndipo walipoanza kunisumbua. Nimekaza mwanangu mpaka basi! Wana wananiona mimi mayai kumbe mwamba makarateka! Ila kuna wawili walinivuruga Mzee Faith na Lulu ni black wa ukweli hivi! Ila aliyenivuruga zaidi alikuwa ni Faith. Tatizo alikuwa ni sister duu na kwa muonekano wangu alidhani mimi ni brother man.

Mwamba nilikaza mpaka basi! Kuna siku yale mambo yamejaa kibubu nikasema huyu "she" nipite nini?! Mbaya zaidi master alikuwa anapenda kufanya demo na mimi zaidi. Kwa vile sikiwahi kukutana na mwanamke yeyote kimwili nikawa muoga! Mungu anisamehe nikajichua bhana! Jioni kwenye mazoezi nilifikisha squat ya 50+ mapaja yakaanza kuita. Nikawahi kuchoka na maumivu ya mwili nikawa nayasikia mapema tu. Master akaniangalia halafu akanipotezea.

Napenda sana mazoezi. Tatizo sasa hivi kazi zinanibana! Inafika kipindi mpaka naweka equation na kuikokotoa ili niangalie uwepesi wa kazi yangu niufanyaje ili nipate muda. Huwa nafanya mazoezi kwa masaa 3 mpaka 4. Sasa nafanya kwa nusu saa najisikia vibaya sana.
Aisee nilisikia squart zinafanya mtu uwe na hamu sana ya ngono sasa kama ulikuwa unapiga nyingi hivyo 50+ ulikuwa unajikontroo vipi. Umewahi kufikusha squart 100? Je ni zipi unapiga.... zile za kubeba kitu flani kizito au zile plain za bila kubeba kitu? Pia je zipi ni nzuri kati ya hizo?
 
Wasalaaaaam wazee.

Ni kwa muda mrefu sana nimekuwa nikipenda kujifunza sanaa za mapigano.

Sasa wadau naamini humu kuna wakongwe na wajuzi wa mambo haya mnaweza kunipa ushauri...

Je ni sanaa ipi ya mapigano iko strong kwa maana ya self defence, sihitaji kuwa mkorofi ila mtu akijichanganya vibaya hilo pigo atakalopewa akasimulie ukoo wao wote.

Nipo Mbeya. Kwa wanaojua mkoa wa mbeya mafunzo hayo nitayapata wapi naomba anijuze.

Kuna ishu iliniitokea juzi siku ya iddi mosi, nikaenda pub moja hivi matata sana kwajili ya kupata ulabu na mbuzu choma kidogo

Sasa nikiwa mule ndani kuna jamaa mmoja tukazinguana vikali tu nikasimama kwajili ya mpambano maana naye alionesha wazi anataka tupigane.....nikajipanga mkao wa vita sasa...... Eebwanaeeee nilikula pigo moja hivi la ajabu kisha akanimalizia na teke moja hivi nikaona sasa huyu simuwezi maana anaonekana anamafunzo ya kupigana wakati mimi sina. Nikataka kumtwisha chupa la kvant wadau wakaja kuzuia pale.

Na mimi nataka kujua kupigana maana sasa tunakoelekea sio kuzuri.
Unataka kujifunza Martial arts kwaajili ya kulipiza kisasi??

Martial arts ni sanaa kama Sana'a.zingine, ikitokea Bahati mbaya sana ndio itabidi uapply kwaajili ya kujilinda sio kuua

Nenda Arusha kuna Dojo nyingi na Trainers wa kutosha
 
Kwahiyo sisi tuliooa hatuna chetu hapa ama vipi mkuu?
Hapana, mtaweza ila hamtakuwa na Perfomance nzuri kama wasiooa au kuendekeza sex, ila kama unaweza kufanya tendo la ndoa kwa wiki mara moja, kwa mwezi mara nne haina shida

Ila pombe na sigara itabidi uachane navyo
 
Shadow boxing ni ipi? Au ndiyo ile ya kina tyson!!!
Unapiga ngumi nyingi hewani,unakwepa,unatumia footwork yako pia,yaani zoezi hili unafanya wewe mwenyewe
Inakutengenezea speed pia na uwepesi
Wakati unatoa punch unatumia mwili wako wote
Alafu inasaidia kupunguza calories mwilini sana
Mimi mtu wa mtungi ila bila vimazoezi ningeshafeli

Ova
 
mwenye connection ya mwalimu mzuri wa martial art, simple techniques, zinazofunzika Kwa haraka... anisaidie.

location : songea town.

nataka nibadili mfumo wa mazoezi naona huku kwenye soccer vijana wataniua bure ......

Ikiwa ni tofauti na shotokan karate itakua poa zaidi ........boxing hapana.
 
mwenye connection ya mwalimu mzuri wa martial art, simple techniques, zinazofunzika Kwa haraka... anisaidie.

location : songea town.

nataka nibadili mfumo wa mazoezi naona huku kwenye soccer vijana wataniua bure ......

Ikiwa ni tofauti na shotokan karate itakua poa zaidi ........boxing hapana.
Ungekuwa Dar ningekuunganisha kwa jamaa zangu, wapo wawili na wote wana Dojo zao
 
Back
Top Bottom