Ahh wapi Mzee!
Huwa sisumbui wanawake ila wao ndiyo wananisumbua. Muonekano wangu una taswira ya mtoto wa mama/bi shoo na wengine wamefika mbali na kudai
Hammaz ni HB. Nasumbuliwa na allergy kibao! Tumbo langu kula vyakula vya mtaani haliwezi ni kila tu naendesha. Hivyo nina aina ya vyakula vyangu ninavyokula.
Mazingira hayo wakati nasoma yalinifanya nionekane wa kishua na muonekano wangu daaah ulinigharimu! Ukizingatia huwa sina habari na mambo yasiyonihusu ilikuwa ni balaa! na mapigo yangu yalikuwa ni ya ki-hip hop kisa mimi mweupe wanapagawa kabisa.
Hapo sasa wanawake ndipo walipoanza kunisumbua. Nimekaza mwanangu mpaka basi! Wana wananiona mimi mayai kumbe mwamba makarateka! Ila kuna wawili walinivuruga Mzee Faith na Lulu ni black wa ukweli hivi! Ila aliyenivuruga zaidi alikuwa ni Faith. Tatizo alikuwa ni sister duu na kwa muonekano wangu alidhani mimi ni brother man.
Mwamba nilikaza mpaka basi! Kuna siku yale mambo yamejaa kibubu nikasema huyu "she" nipite nini?! Mbaya zaidi master alikuwa anapenda kufanya demo na mimi zaidi. Kwa vile sikiwahi kukutana na mwanamke yeyote kimwili nikawa muoga! Mungu anisamehe nikajichua bhana! Jioni kwenye mazoezi nilifikisha squat ya 50+ mapaja yakaanza kuita. Nikawahi kuchoka na maumivu ya mwili nikawa nayasikia mapema tu. Master akaniangalia halafu akanipotezea.
Napenda sana mazoezi. Tatizo sasa hivi kazi zinanibana! Inafika kipindi mpaka naweka equation na kuikokotoa ili niangalie uwepesi wa kazi yangu niufanyaje ili nipate muda. Huwa nafanya mazoezi kwa masaa 3 mpaka 4. Sasa nafanya kwa nusu saa najisikia vibaya sana.