Asante kuni tag.
Kama alivyosema Mkuu
Mshana Jr ,
Kwa kuongezea,
Nao walipokuwa wakila Yesu alitwaa mkate, akabariki, akaumega, akawapa wanafunzi wake, akasema, Twaeni, mle; huu ndio mwili wangu Akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, Nyweni nyote katika hiki; kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.
Kabla ya ujio wa wakoloni wazungu walioleta dini ya Ukristu, na walitanguliwa na wavamizi, Waarabu walioleta Uislamu, walitukuta Waafrika tuna tamaduni zetu za kiasili na dini zetu za asili, za kuamini mizimu na kufanya matambiko, wakatudanganya kuwa tamaduni zetu ni za kishenzi na dini zetu za asili ni upagani, wakaleta Uislamu ambao wenyewe bado unaendeleza kafara ya kuchinja, na kwa Ukristu, Kristo ndiye Mwana Kondoo, aliyejitoa sadaka kwa kwa kuzibeba dhambi za ulimwengu, hivyo ndio kafara ya mwisho kwa kifo chake msalabani, kwenye ile karamu ya mwisho,
na kila kwenye adhimisho la misa, Wakristu wanakula mwili wake na kuinywa damu yake,
Kwenye ile karamu ya mwisho, nao walipokuwa wakila Yesu alitwaa mkate, akabariki, akaumega, akawapa wafuasi wake, akisema, "Twaeni, mle; huu ndio mwili wangu utakaotolewa kwajili yenu na kwa ajili ya wote, fanyeni hivi kwa kunikumbuka mimi"
Vivyo hivyo, baada ya kula, akatwaa kikombe, akashukuru, akawapa, wafuasi wake akisema, akisema, twaeni mywe wote, hiki ni kikombe cha damu yangu, damu ya agano jipya la milele, itakayo mwagika kwa ajili yenu na kwa ajili ya wote kwa maondoleo ya dhambi, fanyeni hivi kwa kunikumbuka mimi"
Hii ndio tambiko na kafara ya mwisho ya Ukiristo.
Mtu ukiishaupokea Uislamu au Ukiristo, tumedanganywa hatuna tena haja ya kuendelea kufanya matambika ya asili ya mila na desturi, yako mambo kwenye maisha yetu, sala za dini hazifui damu, lone has to go back to his roots kufanya matambiko ya kiasili, yanasaidia sana.
Mdharau mila ni mtumwa.
P