Habari za Ijumaa wana JF.
Mimi leo nimeona nije na hii mada tajwa nahitaji kujifunza mambo ya asili hasa matambiko faida zake pamoja hasara zake kama zikiwepo.
Na vitu gani vinatakiwa katika kukamilisha zoezi hilo la kutambika.
NB: Mimi asili yangu mkurya itapendeza sana kurya iwe case study.
Natanguliza shukrani.
Kamtafute hitoria ya Raisi wa Jamhuri ya Chui
Alipandisha bendera ya ngozi ya chui, nyere mwenyewe alijikojolea na kitete
Akatuma jeshi likaua wakurya wengi sana
Mtu anayejua historia ya mkoa wa mara ambao kuna kipindi ulijitenga ukaanzisha jamuhuri ya watu wa chui aweke hapa
Kipindi cha vita vya Kagera, mwaka 1978 hadi 1979, kulikuwa na mapito magumu sana kwa mikoa iliyo jirani na eneo la Mutukula, eneo mtawalia la uwanja wa vita. Katika kushirikisha umma kwenye vita hivyo, Rais wa Tanzania Mwl. Nyerere alitangaza azimio la "hiyari" kila mtu, nchi nzima, kuchangia vita hivyo kwa hali na mali, udi na uvumba, take usitake. Akatangaza kujitolea kwa kila mtu chochote alichonacho hasa mifugo (ng'ombe, kuku, kondoo, mbuzi, sungura, sili, nguruwe, vikitajwa vichache), kwaajili ya wapiganaji katika vita ya Kagera. Ijapokuwa wapo waliojisikia fahari kuchangia vita hivyo, pia wapo (wacheche) walioona ni uporaji mpya wa mali za wananchi katika taifa lao kwa mgongo wa kuchangia vita ya Kagera.Katika mkoa wa Mara, zoezi hilo lilipata upinzani mkubwa. Makabia ya Wakurya, na koo za Wanchori na Wanchari yalipinga mpango huo, na kwa hakika kwa jiografia ya jeshi la Tanzania, mkoa wa Mara ulikuwa na bado una vijana wengi jeshini. Hili lilikuwa ni la kiasili tangu enzi za ukoloni jeshi lilichukua zaidi makabila yenye nguvu za kupigana na yenye ujasiri wa asili, kama Mara, Iringa, Songea nk.Kuna jamaa mmoja aliyeitwa Gisyari, alikuwa akiishi Kagera, alienda Gibaso, akawambia watu wa Engwe (himaya za kitemi mkoani Mara): Uganda haikuvamia Tanzania bali ilikuwa ni mbinu ya Mwl. Nyerere kumsaidia rafiki yake Obote. Hata lile daraja lilipigwa na jeshi la Tanzania.”Mtemi na Shujaa wa kweli wa mkoa wa Mara, Nyamaghanya, aliposikia hizo taarifa alighafirika sana na kwa kuwa alikuwa akiungwa mkono na vijana wengi majabali, akaitisha mkutano mkubwa eneo la Gwitönga na kuwauliza vijana: “Je, mpo tayari kutetea mifugo na watu wenu?” Ndipo vijana wakajibu kwa kura ya ndiyo, yaani wapo tayari. Siku hiyo hiyo, saa tano na nusu za usiku, wimbo wa taifa tukufu la Engwe ukapigwa na kupandisha bendera ya ngozi ya chui. Taifa la Engwe likajitangazia uhuru na kujiita Jamhuri ya Chui.Ripoti namba D 207 yenye kurasa kumi na sita, iliyowasilishwa na Dr. Hassy Kitine, kwa mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Taifa, Mwl. Nyerere, kabla ya tukio hili ilionesha kuna baadhi ya wanajeshi waliokuwa vitani wamezifikisha silaha na kuficha mikononi mwa vikundi vya jadi. Lakini kinyume na matarajio, ripo hiyo haikuwa na uzito wa kijasusi.Mwaka mmoja baada ya kuitisha mkutano na kutaka kujilinda na kulinda mali zao, yani mwaka 1982, Nyamaghanya alitangaza kujitenga kwa mkoa wa Mara, akauita Jamhuri ya watu wa Chui. Nchi hii mpya makao makuu yakatangazwa kuwa ni Gibaso na mishahara ya watumishi wake ni ng'ombe. Nyamaghanya alikuwa na jeshi hodari sana likiitwa Esaiga ya Gesambiso na vijana wa kati ambao walikuwa hodari wa kupiga mishale. Hali hii iliustua utawala wa Mwl. Nyerere ambao kwa hakika ulikuwa kwenye mapito magumu baada ya jaribio la mapinduzi la mwaka 1982, ndipo akaamua kumwaga Jeshi lake la JWTZ kuzima uasi huo
Kwa hisani ya
Yericko Nyerere