Nahitaji kujua faida za ibada za asili/ matambiko

Mafeking

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2018
Posts
315
Reaction score
614
Habari za Ijumaa wana JF.

Mimi leo nimeona nije na hii mada tajwa nahitaji kujifunza mambo ya asili hasa matambiko faida zake pamoja hasara zake kama zikiwepo.

Na vitu gani vinatakiwa katika kukamilisha zoezi hilo la kutambika.

NB: Mimi asili yangu mkurya itapendeza sana kurya iwe case study.
Natanguliza shukrani.
 
Ngoja waje usiache kuni tag
 
Faida kuu za ibada za asili na matambiko ni kulinda utambulisho wa utamaduni, kuunganisha jamii, na kudumisha amani na mazingira.

Katika jamii nyingi za Kiafrika, matambiko hayachukuliwi kama imani ya kidini tu, bali kama mfumo mzima wa maisha unaoongoza maadili na uhusiano kati ya binadamu, asili, na walioitangulia mbele ya haki (mizimu).
 
Asante kuni tag.
Kama alivyosema Mkuu Mshana Jr ,
Kwa kuongezea,
Nao walipokuwa wakila Yesu alitwaa mkate, akabariki, akaumega, akawapa wanafunzi wake, akasema, Twaeni, mle; huu ndio mwili wangu Akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, Nyweni nyote katika hiki; kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.
Kabla ya ujio wa wakoloni wazungu walioleta dini ya Ukristu, na walitanguliwa na wavamizi, Waarabu walioleta Uislamu, walitukuta Waafrika tuna tamaduni zetu za kiasili na dini zetu za asili, za kuamini mizimu na kufanya matambiko, wakatudanganya kuwa tamaduni zetu ni za kishenzi na dini zetu za asili ni upagani, wakaleta Uislamu ambao wenyewe bado unaendeleza kafara ya kuchinja, na kwa Ukristu, Kristo ndiye Mwana Kondoo, aliyejitoa sadaka kwa kwa kuzibeba dhambi za ulimwengu, hivyo ndio kafara ya mwisho kwa kifo chake msalabani, kwenye ile karamu ya mwisho,
na kila kwenye adhimisho la misa, Wakristu wanakula mwili wake na kuinywa damu yake,

Kwenye ile karamu ya mwisho, nao walipokuwa wakila Yesu alitwaa mkate, akabariki, akaumega, akawapa wafuasi wake, akisema, "Twaeni, mle; huu ndio mwili wangu utakaotolewa kwajili yenu na kwa ajili ya wote, fanyeni hivi kwa kunikumbuka mimi"

Vivyo hivyo, baada ya kula, akatwaa kikombe, akashukuru, akawapa, wafuasi wake akisema, akisema, twaeni mywe wote, hiki ni kikombe cha damu yangu, damu ya agano jipya la milele, itakayo mwagika kwa ajili yenu na kwa ajili ya wote kwa maondoleo ya dhambi, fanyeni hivi kwa kunikumbuka mimi"

Hii ndio tambiko na kafara ya mwisho ya Ukiristo.

Mtu ukiishaupokea Uislamu au Ukiristo, tumedanganywa hatuna tena haja ya kuendelea kufanya matambika ya asili ya mila na desturi, yako mambo kwenye maisha yetu, sala za dini hazifui damu, lone has to go back to his roots kufanya matambiko ya kiasili, yanasaidia sana.

Mdharau mila ni mtumwa.

P
 
Hakuna faida yeyote, ni Sana Sana uzid kujifunga tu maagano ya giza bila kujua.

Kafanye ibada halisi ya Mungu aliye hai, Acha kuabudu watu or mizimu
Kuwakumbuka waliotangalia mababu zetu
 
Nimeanza kupata mwanga japo wengi wanadharau vitu vya asili wakidhani ni uchawai hali ya kuwa ndio asili ya uafrika.
 
Umetisha Sana to day
 
Nahitaji niijue utamaduni wangu wa kikurya namna ya kutambika. Kama naweza tambika ata eneo nililopo kwasasa au hadi nitakapoenda chimbuko nilipotoka.
Unaweza kufanya but first Inatakiwa uiamshe nguvu Yako ya asili ambayo Ipo ndani Yako

Kisha hiyo nguvu itakuwa Ina kuelekeza Kila kitu Cha kufanya ni ngumu kuweza kusema kwamba matambiko ya wakurya yapo hivi na vile na mtu atakaye kuambia hivyo atakuwa anakupoteza bila ya yeye kujua

Mambo ya mizimu + majini ni mambo ambayo ni magumu sana cause elimu yake ni nzito lakini Kwa watu wenye ufahamu na elimu hiyo ni kitu chepesi sana

Mizimu unaongea + majini wanaongea na Huwa wanatoa maelekezo ya ndoto zao through dreams so unachapaswa kufanyiwa nikuamshwa hiyo nguvu Yako ya ndani uliyonayo ya hao viumbe Kisha wataanza kukupa elimu kama unatokea kwenye ukoo wenye hizo elements ni lazima tu waratakuja nakuanza kukuelekeza Kila kitu

Mpaka jinsi matambiko Yao yanavyo fanyika , ni ngumu sana kujua Tambiko la watu wa jamii Fulani cause vile viumbe Huwa vina chaguzi tofauti tofauti kama watu , Kuna wengine wana kula hiki wengine wana kula kile , so unapo amshwa hiyo nguvu wenyewe watakuja na kukutajia mfumo mzima jinsi ulivyo mpaka vyakula vyao na Kuna wengine Huwa wana wafundisha watu mpaka nyimbo zao wanazo tumia kwenye matambiko Yao and so many
 
Asante sana elimu yako hii fupi ila sijatoka mtupu nimepata kitu cha kuanzia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…