Nahitaji kujua faida za ibada za asili/ matambiko

Umeandika kitu kikubwa sana braza P, na kwa kuongezea tu kwa wale wanaodharau mila za kwao na kutukuza za wazungu na waarabu basi wajue wanatukuza mababu wa wenzao, hao wakina Adam, Ibrahim, Musa, Yakub, nakadhalika ni mababu wa wayahudi na waarabu je iweje sisi kuwatukuza mababu zetu iwe nongwa iwe maagano sijui uchawi, kwa hakika tunasikitisha sana.
 
Nahitaji niijue utamaduni wangu wa kikurya namna ya kutambika. Kama naweza tambika ata eneo nililopo kwasasa au hadi nitakapoenda chimbuko nilipotoka.
Hayo mambo ni lazima urudi kwenye asili yako, kawatafute wazee wa kimila wakupe maelekezo huwezi kujitambikia ni lazima utambikiwe upate mwanga kwanza, kama upo Dsm nenda pale kijiji cha makumbusho waambie unahitaji kuonana na wahusika wa kikurya waelezee shida yako watakuonesha pa kuanzia,
Good Luck
 
Mtambiko ni Ibada kama Ibada nyingine na ndio Ibada ya kweli halisi
Faida yake inakuunganisha na asili yako inakulinda na kukupa mafanikio
Kikubwa zaidi ukienda kanisani au msikitini kuomba chochote
Kujibiwa ni pole pole sana au usijibiwe kabisa
Ila kwenye tambiko ukifanya vema inavyopaswa kujibiwa ni wakati huo huo kama umeomba mafanikio asili yako ikubali kwazia wakati ule mafanikio unaanza kuyaona
Hasara ukikosea adhabu na muda huo huo mtambiko Yana faida Sana
 
Unashindwa kuelewa kwamba hizo ibada zenyewe ndio matambiko hizo dini zote zinaabudu watu na Zina matambiko but you guys you know nothing
Yaani hizi dini zimetuvuruga kweli kweli,mkristo kwenye maombi yake lazima autaje mzimu wa wayahudi (kwa jina la yesu) Kwa waislamu ndio balaa inabidi uutaje mzimu unaoitwa Muhammad halafu sio pekee yake uwataje pia masela wake,mpaka mababu zake
( allahuma swali ala Muhammad,waala alih Muhammad,kama swallaita ala Ibrahim waala alih Ibrahim) yaani usipoitaja hiyo mizimu yako hayaendi wala swala yako haitokubaliwa,lakini mimi msukuma/mshiraz/mpokomo/mzaramu/mndengereko/muhaya/mmasai/mbwela nikiomba kwa majina ya Mzee wangu Azilongwa eti wananiambia ni dhambi nitaenda motoni πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Nalog off Z
 
Waafrica Akili hawana yaani kwenye ibada zao ni mwanzo mwisho wanataja majina ya elites wao tu waliokufa inashangaza sana halafu ukiwauliza wana kuambia hatuwaabudu wao tuna muabudu mungu 😁😁
 
Waafrica Akili hawana yaani kwenye ibada zao ni mwanzo mwisho wanataja majina ya elites wao tu waliokufa inashangaza sana halafu ukiwauliza wana kuambia hatuwaabudu wao tuna muabudu mungu 😁😁
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Tatizo ni kwamba huyo Mungu ni mshikaji wao, yaani bila kiwataja hao masela wake,anakutosa hakujibu wala nini 😭 Lazima uwataje hao jamaa ndio naye eti anakujibu πŸ˜‚hakuna njia ya mkato.
Nalog off Z
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Tatizo ni kwamba huyo Mungu ni mshikaji wao, yaani bila kiwataja hao masela wake,anakutosa hakujibu wala nini 😭 Lazima uwataje hao jamaa ndio naye eti anakujibu πŸ˜‚hakuna njia ya mkato.
Nalog off Z
Chai sana πŸ˜„
 
Asante mkuu nitafika hapo makumbusho
 
Nimeanza kupata mwanga japo wengi wanadharau vitu vya asili wakidhani ni uchawai hali ya kuwa ndio asili ya uafrika.
Nenda tiktok au instagram search awery naona ndio vitu vyake hiz atakupa elimu
 
We always pray to ansestors, yesu sio ansestor wako ni wa wayahudi, mohamedi vilevile ndo maana kila tunachowaomba kupitia yesu hakuna hata kimoja kinatokea usipofanya juhudi zako.
 
Vakwa sangasu na sangawe na lakuturo hai na hai turingeni vana va mwonu ha mwai tuininge na tsafo mbora, enda bariki kasi tsa mavoko a motu... Hai mangi Ruwa nja mbombe tpuuu tpuuuu
 
Tuanze hapa mara ya mwisho kwenda kwenu lini?. Kwanini hutaki kurudi nyumbani?. Kweli wazazi wamefariki hakuna mtu nyumbani je ardhi walioishi wazazi wako na babu zako nayo imekufa?.

Mara ya mwisho kwenda kwenye kaburi la wazazi wako lini?. Kwanini huendi?. Kuna mtu kakudanganya kwenda kuwasalimia wazazi wako makaburini ni ushirikina ehnee?.

Chukua hii ni ngumu kufanikiwa kama huna mawasiliano ya kiroho na chimbuko lako. Roho hazifi bwana mdogo roho zipo hai na zitaishi paka mwisho wa dunia.

Pengine mashaka na maradhi unayopitia kwasababu wazazi wako wana kinyongo na wewe. Dunia tunayoishi leo ni kudanganyana tu ila ukweli wa dunia lazima upate maelekezo ya watu waliokutangulia.

Ndio maana watu wote waliokuja kusimamia dunia hii kwa mafanikio walienzi wazee wao waliotangulia. Lakini walipata ndoto za babu zao katika kusimamia dola zao na maisha yao. Walivaa nguo za wazazi wao na kutumia vitu vyao ili kuamsha nguvu ya ndani.

Wewe hufanikiwi kwasababu unaishi kama mdudu hukumbuki chimbuko lako na uzao wako. Kasalimie kwenu. Unganisha cheni yako na ya vizazi vyako vilivyotangulia utaona mabadiliko. Nenda kwenye kaburi la wazazi wako safisha na msalimie anakusikia na anakujibu.

Asili kwanza
Asili Ina nguvu
Mdharau asili hufa kikatili
 
Mimi chimbuko langu ni Tarime ila sijawahi kwenda huko ila baba yupo pwani na ndugu wengine wengi wanaishi dar es salaam.
Natamani sana nifike Tarime nikaone kaburi la babu yangu na ndugu zake wengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…