Nahitaji kujua faida za ibada za asili/ matambiko

Mimi chimbuko langu ni Tarime ila sijawahi kwenda huko ila baba yupo pwani na ndugu wengine wengi wanaishi dar es salaam.
Natamani sana nifike Tarime nikaone kaburi la babu yangu na ndugu zake wengi
Nenda mkuu ni muhimu sana
 
Nahitaji niijue utamaduni wangu wa kikurya namna ya kutambika. Kama naweza tambika ata eneo nililopo kwasasa au hadi nitakapoenda chimbuko nilipotoka.
Kutambika kwanza muhimu ujue ni mizimu ya aina gani iliyo mbele maana unaweza kutambika kumbe ukajikuta unatambikia mizimu ambayo ina madhara kwako kuliko faida, na kutambika sio lazima uende kwenye chimbuko lako bali unaweza kutambika popote tu ulipo.
 
Unashindwa kuelewa kwamba hizo ibada zenyewe ndio matambiko hizo dini zote zinaabudu watu na Zina matambiko but you guys you know nothing
Kwahiyo matambiko ni ibada?
 
Ibada iwe ya asili au ya kidini, Haina faida yoyote. Ni kujipa matumaini hewa tu.

Hakuna Mungu.
Mungu yupo. Tatizo watu weng hujiuliza Mungu ni nani badala ya Mungu ni nini!
Mungu ni wewe kwa sabab Mungu ni nguvu(energy) iliyoko ndani mwako.
Hayo mengine tulishakubaliana ni kupelekana chaka!
 
Kwenye suala la mizimu sio wote wenye kujihusisha au kuamini mizimu basi wanaamini mizimu ni nafsi za mababu zetu, watu wana imani tofauti tofauti kuhusu masuala ya mizimu na matambiko.
 
Kamtafute hitoria ya Raisi wa Jamhuri ya Chui
Alipandisha bendera ya ngozi ya chui, nyere mwenyewe alijikojolea na kitete
Akatuma jeshi likaua wakurya wengi sana


Kipindi cha vita vya Kagera, mwaka 1978 hadi 1979, kulikuwa na mapito magumu sana kwa mikoa iliyo jirani na eneo la Mutukula, eneo mtawalia la uwanja wa vita. Katika kushirikisha umma kwenye vita hivyo, Rais wa Tanzania Mwl. Nyerere alitangaza azimio la "hiyari" kila mtu, nchi nzima, kuchangia vita hivyo kwa hali na mali, udi na uvumba, take usitake. Akatangaza kujitolea kwa kila mtu chochote alichonacho hasa mifugo (ng'ombe, kuku, kondoo, mbuzi, sungura, sili, nguruwe, vikitajwa vichache), kwaajili ya wapiganaji katika vita ya Kagera. Ijapokuwa wapo waliojisikia fahari kuchangia vita hivyo, pia wapo (wacheche) walioona ni uporaji mpya wa mali za wananchi katika taifa lao kwa mgongo wa kuchangia vita ya Kagera.Katika mkoa wa Mara, zoezi hilo lilipata upinzani mkubwa. Makabia ya Wakurya, na koo za Wanchori na Wanchari yalipinga mpango huo, na kwa hakika kwa jiografia ya jeshi la Tanzania, mkoa wa Mara ulikuwa na bado una vijana wengi jeshini. Hili lilikuwa ni la kiasili tangu enzi za ukoloni jeshi lilichukua zaidi makabila yenye nguvu za kupigana na yenye ujasiri wa asili, kama Mara, Iringa, Songea nk.Kuna jamaa mmoja aliyeitwa Gisyari, alikuwa akiishi Kagera, alienda Gibaso, akawambia watu wa Engwe (himaya za kitemi mkoani Mara): Uganda haikuvamia Tanzania bali ilikuwa ni mbinu ya Mwl. Nyerere kumsaidia rafiki yake Obote. Hata lile daraja lilipigwa na jeshi la Tanzania.”Mtemi na Shujaa wa kweli wa mkoa wa Mara, Nyamaghanya, aliposikia hizo taarifa alighafirika sana na kwa kuwa alikuwa akiungwa mkono na vijana wengi majabali, akaitisha mkutano mkubwa eneo la Gwitönga na kuwauliza vijana: “Je, mpo tayari kutetea mifugo na watu wenu?” Ndipo vijana wakajibu kwa kura ya ndiyo, yaani wapo tayari. Siku hiyo hiyo, saa tano na nusu za usiku, wimbo wa taifa tukufu la Engwe ukapigwa na kupandisha bendera ya ngozi ya chui. Taifa la Engwe likajitangazia uhuru na kujiita Jamhuri ya Chui.Ripoti namba D 207 yenye kurasa kumi na sita, iliyowasilishwa na Dr. Hassy Kitine, kwa mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Taifa, Mwl. Nyerere, kabla ya tukio hili ilionesha kuna baadhi ya wanajeshi waliokuwa vitani wamezifikisha silaha na kuficha mikononi mwa vikundi vya jadi. Lakini kinyume na matarajio, ripo hiyo haikuwa na uzito wa kijasusi.Mwaka mmoja baada ya kuitisha mkutano na kutaka kujilinda na kulinda mali zao, yani mwaka 1982, Nyamaghanya alitangaza kujitenga kwa mkoa wa Mara, akauita Jamhuri ya watu wa Chui. Nchi hii mpya makao makuu yakatangazwa kuwa ni Gibaso na mishahara ya watumishi wake ni ng'ombe. Nyamaghanya alikuwa na jeshi hodari sana likiitwa Esaiga ya Gesambiso na vijana wa kati ambao walikuwa hodari wa kupiga mishale. Hali hii iliustua utawala wa Mwl. Nyerere ambao kwa hakika ulikuwa kwenye mapito magumu baada ya jaribio la mapinduzi la mwaka 1982, ndipo akaamua kumwaga Jeshi lake la JWTZ kuzima uasi huo
Kwa hisani ya Yericko Nyerere
 
Ni yenyewe mizimu ndio ilisema matambiko ni ibada? Kuna watu mbali na kufanya matambiko ila wana sala ya kuabudu kabisa mizimu mbali na tambiko, hivyo hawachukulii kuwa tambiko ni ibada.
 
Ila tambua tu mkuu kwamba huo mtazamo wa kwamba mizimu ni wazee wetu sio mtazamo wa watu wote wenye kuamini kwenye mizimu.
 
We always pray to ansestors, yesu sio ansestor wako ni wa wayahudi, mohamedi vilevile ndo maana kila tunachowaomba kupitia yesu hakuna hata kimoja kinatokea usipofanya juhudi zako.
Inashangaza, kama Yesu ni kwa wayahudi wote mbona sisi waafrika kila ukoo una mizimu yake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…