Nahitaji kujua zaidi kuhusu kisiwa cha Mayotte

Nahitaji kujua zaidi kuhusu kisiwa cha Mayotte

Wadau wa JF habari?Hivi karibuni kumetokea kimbunga CHIDO katika bahari ya hindi na kuathiri maeneo mbalimbali ikiwemo kaskazini mwa msumbiji,Malawi,Zimbabwe na kisiwa cha Mayotte..katika kufuatilia zaidi nakutana na habari ya kuwa kisiwa cha mayotte ni eneo la Ufaransa na Rais wa Ufaransa Macron alitembelea kisiwa hicho baada ya janga hilo...Naomba kwa wanaofahamu zaidi hii imekaaje kisiwa hiki kuwa milki ya ufaransa?wenyeji wa pale ni watu gani?Population yake ikoje?ukubwa wa eneo n.k
Sio Mayotte tu hata US na british wana teritories kwenye mabara mengine british wana teritories kama 14 hivi na US ana kama 5 hivi
 
Mayotte however became the 101st department of France (Fifth French Republic) on 31 March 2011 and became an outermost associated region of the European Union on 1 January 2014, following a March 2009 referendum with an overwhelming result in favour of remaining in the status of a French department. The issue of illegal immigration became very important in local political life in the 2010s and 2020s which led France to organize Operation Wuambushu.

In 2019, with an annual population growth of 3.8%, half the current population was less than 17 years old. In addition, 48% of the population were foreign nationals.[6] Most of the immigrants come from neighboring Island state of Comoros, many illegally. Despite being France's poorest department, Mayotte is much richer than other neighboring East African countries and has developed French infrastructure and welfare system, making it a tempting destination for Comorans and other East Africans living in poverty in the region.[7] The department faces enormous challenges.

According to an Institut national de la statistique et des etudes economiques (National Institute of Economic Statistics Studies of France - INSEE) report published in 2018, 84% of the population live under the poverty line according to French standards, compared to 16% in metropolitan France, 40% of dwellings are corrugated sheet metal shacks, 29% of households have no running water, and 34% of the inhabitants between the age of 15 and 64 do not have a job.[8] These difficult living conditions mainly concern the large population of illegal migrants who crowd into shanty towns.[9]
Kwani kuandika kiswahili huwezi? Aaah....
 
Kwani kuandika kiswahili huwezi? Aaah....
Kwani kusoma kiinglishi haujui, ebooooh!!!

Wote tulipelekwa shule na serekali yetu ya Sisiemu.

Kidumu chama. Kila mtu asome anachojua kusoma au ale kwa urefu wa kamba yake😎
 
Sio Mayotte tu hata US na british wana teritories kwenye mabara mengine british wana teritories kama 14 hivi na US ana kama 5 hivi
Ikiwa Mayotte ni teritori maskini ya mwisho kwa teritoriiz zote za Ufaransa,, lakini ni tajiri ikilinganishwa na nchi za Afrika mashariki. Shida ni gani hapo? Watawala au watawaliwa? Nahisi ni watawala.... Ikiwa Mayotte wangejitawala wangekuwa sawa na Kenya na Tanzania. Eboooooh.

Mnaonaje na sisi tutafute wa kutufanya teritoriiz zake. Nampendekeza Trump.
 
Msipende kutafuniwa kila kitu mtasaidiwa hadi majukumu ya msingi, yani mtu aende google kuchukua taarifa ambazo ungeweza kugoogle mwenyewe, ni uvivu na ujinga ulioje?

Kuna mtu hapo kaweka taarifa alizotoa Wikipedia, nyie kinawashinda nini kwenda Wiki wenyewe?
Hapa anaweza kupata majibu sahihi zaidi ikiwemo na experience ya waliowahi kwenda huko...

Na ndio kazi ya mitandao ya kijamii kama jf, uliza chochote kinachokupa utata.
 
Ni miliki ya ufaransa, kuingia kisiwa cha mayyote kama hujakamilisha documents ni kazi sana. Wazamiaji wanaingia na boti ila kuna doria kali sana
 
Ikiwa Mayotte ni teritori maskini ya mwisho kwa teritoriiz zote za Ufaransa,, lakini ni tajiri ikilinganishwa na nchi za Afrika mashariki. Shida ni gani hapo? Watawala au watawaliwa? Nahisi ni watawala.... Ikiwa Mayotte wangejitawala wangekuwa sawa na Kenya na Tanzania. Eboooooh.

Mnaonaje na sisi tutafute wa kutufanya teritoriiz zake. Nampendekeza Trump.
😂😂😂 kaka mbona unapanga matokeo tayari eti unamtaka trump kuna wengie pro Russia watakwambia wanamtaka Putin

By the wat umaskini wa mayotte hausababishwi na Ufaransa (watawala) sababu mayotte waliamua kubaki coloni la ufaransa.. ila wana wanajiongoza kwa asilimia 70% na wana uhuru wa kujitoa mda wowote

Kiasili Mayotte ni kama commoro na wao na commoro kiasili ni kama watu wa mombasa na zanzibar sehemu hizo
Zina muingiliano wa kiasili ndo maaana hata commoro wana kiswahili
Chao ambacho kina mchanfanyiko wa lugha yao ya asili ila tamaduni nyingi zinafanana na wapemba.

So ukitaka kujua kwa nini mayotte ni maskini jiulize kwa nini zanzibar na sie bara maskini.. na tuna miaka zaid ya 50

Tena usiseme kuwa sie tuna afadhali maana umaskini ni umaskini na uwiano wa maendeleo na miaka toka uhuru haulingani
 
Hapa anaweza kupata majibu sahihi zaidi ikiwemo na experience ya waliowahi kwenda huko...

Na ndio kazi ya mitandao ya kijamii kama jf, uliza chochote kinachokupa utata.

Population, size, kwanini wapo under France yote yanapatikana kwa one click tu online. Huhitaji mtu aliyeenda huko kukupa hizo info. Kama anataka experience za watu waliofika huko angesema bayana kwenye bandiko lake. Sihitaji kufika TZ kujua TZ Ipo wapi, size na population yake. Na ilipata uhuru toka kwa nani. Wabongo wengi tu hawajui ukubwa na population ya TZ. However naelewa wabongo wanavyopenda utegemezi hili ni swala la kitamaduni na ujamaa. Tunaona wanaotaka connection kwenda nje wakitaka kila kitu uwafanyie ili aseme umempa msaada anything short anasema diaspora hawatoi connection.
 
Mimi mwenyewe nilishangaa sana kusikia hicho kisiwa ni Mali ya ufaransa.kupitia wajuzi wanasema hicho kisiwa kulikuwa chini ya utawala wa kifaransa na baada ya uhuru kisiwa hiki kilikataa kuwa sehemu ya comoro na kubaki kuwa sehemu ya ufaransa Hadi leo.wajuzi zaidi watakuja kuongezea
Na huko ndio ukweli wenyewe. Watu kutoka West Africa hupitia kisiwabi hapo ili kuzamia Ufaransa. Ukifika Mayotte ni imefika Ufaransa
 
Kwani kuandika kiswahili huwezi? Aaah....

Hiyo ni copy&paste ya Wikipedia ndo maana nawaambia wamatumbi acheni uvivu nendeni Wikipedia wenyewe mkajisomee imetafsiriwa kwa lugha zaidi ya 100. Kuna sites zingine as well. Tatizo lenu uvivu.
 
Back
Top Bottom