Nahitaji kupungua Mwili/ Kilo. Naumia sana

First year wakati naishi home nilikua kibonge balaa, ratiba ilikua asubuhi napiga chai na vitumbua/chapati au kipolo cha wali.

Mchana nikiwa chuo napiga wali nyama na juice ama soda. Usiku kabla sijaenda home napitia bar napiga beer 3 au 4 ndo naenda home ambako nako napiga menu nzito usiku, hapo ni saa 4 au 5 hivi then nalala.

Ni siku chache ratiba inachange ila ilikua hivyo, aisee nilikua kibonge hatari.

Nikahamia geto, kipindi cha msoto formula ilikua 101 au 011 nikifeli kabisa ni 001 au 010. Nilipungua mpaka wakahisi natumia unga au bangi.

Tunanenepa kwa kulakula hovyo (mfumo mbaya wa chakula).
Na pia kazi unayofanya huenda hailingani na menyu unayopiga kila siku.

Mtu unakula misosi mitatu yote heavy, morn umepiga supu, mchana nyama choma na chipsi jioni dona na harage au wali wa kushiba na hadage wakati kazi ni kukaa ofisini tu.
Mazoezi hufanyi au unafanya ukiwa umejilaza kitandani.

Pole sana jamaa, zingatia mlo na mazoezi.
 
Fanya fasting ya miezi miwili unstoppable muda wa kufungua uwe una kunywa uji na matunda tu.

Usile chakula chochote unapufungua zaidi ya hivyo nilivyokutajia.

Halafu kila siku asubuhi na jioni piga pushups 50 pair, yani kwa siku uwe unajumla ya pushups 100

Hapo utapungua fasta sana
 
Nilipokuwa na kilo 91 nilianza kupata magonjwa ya kuumwa miguu na kushindwa hata kufunga kamba za viatu. Usiku nililala kwa shida.

Nilikuwa nafanya mazoezi ya kutembea au kukimbia kilometer 6 kila siku lakini ndio nilizidi kuongezeka. Nikagundua kuwa mazoezi hayasaidii mwili kupungua na kweli hayasaidii!

Niligundua kitu kimoja tu kinamfanya mtu aongezeke au apungue zito: CHAKULA.

Nilihama kule nilipokuwa na life style mbaya ya kula vyakula vyenye mafuta mengi, chumvi nyingi, peanut butter, nyama nyingi na bia. Nikakaa kijijini nikawa nakula vyakula vya asili ndizi, ugali maharage, mchicha, wali, makande na vyote hivyo vikiwa na mafuta kidogo.

Ilichukua miezi 2 kutoka kilo 92 hadi kilo 80! Suluhisho sio kitu kingine ni CHAKULA!

Achana na nyama nyingi hasa zenye mafuta

Acha siagi, peanut butter etc

Acha vyakula vyenye sukari nyingi

Acha kuweka mafuta mengi kwenye chakula

Acha kula sana hasa vyakula vyenye wanga

Acha kula vyakula vilivyokobolewa kama mchele au sembe

Acha soda na bia.

Acha kula zaidi ya mara mbili kwa siku.

Dawa ni hiyo tu miezi 2 utakuwa 75-80kg ambayo ni nzuri kwa shepu na afya kwa ujumla. Na hata ndoa itaimarika.
 
Unaweza kula mara moja kwa siku.

Nilifanya hii kitu mimi, kula mara moja kwa siku.
Saa moja jioni nikila ndio imeisha hiyo hadi kesho tena saa moja jioni.

Mwezi mmoja tu suruali zote ziliacha kunitosha.
 
Pole man!

Gta SASA kazi kwako!!

Agiza Tabora asali mbichi ndoo ya lita kumi au lita tano!

Chemsha maji ya moto au chai kama ni chai usiweke sukari!

KILA siku asubuhi na jioni weka vijiko vitatu au viwili kwenye maji Moto au chair YAKO isiyo na sukari koroga kunywa,

Jioni kunywa baada ya kula kiasi usile kupita kiasi HALAFU kunywa SASA mchanganyiko huo,asubuhi kunywa kabla ya kuswaki na kula chochote piga Kikombe kimoja kikubwa cha nusu lita au viwili vitatu vya KAWAIDA!kunywa KWA uwezo wako!!

Utaharisha mwanzoni,baadae utazoea na tumbo litaisha KABISA!UTAKUA normal!ukihisi kuu kunywa maji baridi kama kawa!!!!
 
Ebu tueleze bangi inashida gani katika hayo uliyoyataja mkuu, unaionea bure tu.
 
Suluhisho no 2. Atafute mpenzi akipigwa tukio na stress za mapenzi bhas mwili utapungua within a week
 
Acha kula wanga aina zote (wali, ugali, chapati, maandazi, vitumbua, mihogo, viazi, chipsi, sambusa etc). In short vitu vyote vinavyotokana na ngano, sembe au grains
Acha kula sukari (usitumie sukari kwenye chai au maziwa.)
Acha kunywa pombe, soda, energy drinks, juice etc. Kunywa maji tu.
Usivute sigara
Ukifanya haya ndani ya wiki utakuwa na kilo 70.
Kinachounenepesha mwili ni wanga na sukari. Mwili wa binadamu haukuumbwa kutumia wanga. Ndio maana ukila wanga insulin inazalishwa kwenda kuitoa sukari ile kwenye damu na kuibadilisha kuwa mafuta.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani yamenifika kweli..
 
Anza kwa kuangalia menu yako kisha mazoezi

Japo kuna wale unene upo tu kwenye koo na family zao
Kama na wewe kwenye uzazi wenu mpo hivyo wanene option iliyopo ni kujikubali
Kuna wengine Genetics zinatembea kizazi hadi kizazi
 
Kama unaweza kufanya program ya kufunga na mazoezi itasaidia pia
 
Nitafanya ivi kaka nitakupa mrejesh0...
 
Na kadri unavyonenepa na hamu ya kupenda kulakula inaongezeka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…